Faida za kumiliki hisa za Vodacom

Mkuu biashara ya hisa haiko hivyo kuwa akwambie eti baada ya mwaka mmoja utakuwa umetengeneza faida kiasi gani?!! Hiyo sio fixed deposit ambayo faida inajulikana!! Biashara ya hisa inatakiwa elimu ys kutosha sana kabla hujaingia kichwa kichwa!! Gawio linategemea na faida iliyopatikana kwa mwaka!! Mnaweza kaa miaka hata 4 hakuna gawio lolote lile!! Kila mwaka ni hasara tu
 
unaongea too technical,waweken watu wazi kua kampuni ikipata hasara hata miaka mi5 mfululizo bas hata na gawio kwa kipindi hicho chote hakuna.Mbona hicho hukizungumzii?eleza yote faida ni zipi 1,2,3 ....6,7 na hasara ni hizi 1,2,3,4,5,.....10 then mwananchi yeye ndio ataamua anunue au aache.Lakin sio kumwambia anunue then unamuorodheshea faida tu huku upande mwingine ukiuminya.Wengine tumekua tukiona watu waliowekeza kwenye hisa wakitegemea gawio wakiishia kunung'unika tu . sasa epukeni hicho kitu kwa kutoa elimu bora kabisa na sio bora elimu.
 
FAIDA ZA KUMILIKI HISA ZA VODACOM.

ukitaka kununua hisa lazima ujiulize maswali ambayo utaweza kuridhika kwa kiwango cha kutosha kununua Hisa za Vodacom ni rahisi kwani kampuni yenye huduma bora na zanye ubununifu wa kiwango cha juu;

-•M-Pesa; Vodacom ni waanzilishi wa huduma ya kutuma hela kwa kutumia mtandao wa simu kupitia M-Pesa, huduma inayosaidia kutuma na kupokea hela kutoka kila pande ya nchi.

-•M-Pawa; huduma ya kujiwekea akiba, na kuweza kukopa kwa njia rahisi bila kuwa na dhamana.

-Biashara ya uwekezaji ndani ya Vodacom ni rahisi na inayoeleweka katika makundi mbalimbali ya Jamii.

-Vodacom ina historia nzuri katika uendeshaji wake tangu ilipoanzishwa haijawa kubadili jina lake kama makampuni mengine yalivyofanya.

-Kampuni ya VODACOM mipango yake ni mizuri kwa kipindi cha muda mrefu yenye kulenga kufikia makundi yote nchi nzima.

-Menejimenti ya Vodacom imekuwa ikifanya kazi kwa uweledi na ufanisi kibiashara katika kutanua mipaka ya kutanua soko lake na kulinda wateja wake.

- Kampuni ya Vodacom imekuwa na mahusiano mazuri na share holders wake.

- Vodacom imekuwa ikijijengea faida kupitia wateja wake na biashara bora ya huduma yenye kuaminika tangu kuanzishwa kwake nchini.

-Vodacom ni mtandao ulioaminiwa zaidi na watanzania kwa miaka zaidi ya 17, na unaendelea kuaminiwa, Uaminifu kwa wateja umeifanya kuwa kampuni bora ya mawasiliano, Ubora huu unafanya kuwa sehemu salama ya uwekezaji wako.

Wekeza na Vodacom.
 
Ukiwekeza kwa kuweka hela yako ni kwa namna gani nitanufaika?

Kwa muda gani ntakuwa napata hio faida?

Hasa kama nimewekeza lets say 1 mil tshs
 
Mfano mzuri kwa apa Tanzania.
Kama makampuni haya haya ya simu yanapata faida lakini yanadanganya kwamba yanapata hasara, mna washawishi vip? Wananchi wanunue izo hisa na wakati wanajua janja janja ya makampuni mengi yaliyowekeza apa Tanzania.
Mfano mzuri kampuni ya Celtel, Zain, Airtel
Izo zote ni janja janja za kukwepa kodi na kujifanya awapati faida, sasa upuuzi kama huuu mmejipangaje kuuondoa, ili kushawishi watu wengi kununua izo Hisa
 
Moderators huyu kapost tangazo la biashara, alipie kwanza.
 
Mkuu inaonyesha una uelewa mkubwa na mambo ya hisa, kwa faida ya wengi hebu tupe tofauti ya ORDINARY na PREFERENCE shares, Faida na hasara ya kila moja pamoja na gharama za kila moja(Kama zinatofautiana).
 
Nami nimeshangaa sana.
 
ORDINARY SHARE ni umiliki wa Share katika kampuni ambapo shareholders watapewa gawiwo lao baada ya preferential shareholders kupewa gawiwo(DIVIDEND) lao.

Wamiliki wa ordinary shares/common shares huwa wanapewa kipaumbele kidogo au cha chini sana katika kupewa gawiwo. Hii inamaanisha kwamba kampuni ikipata faida wanaoanza kupewa gawiwo ni wale wanaomiliki wa preference shares halafu wanafuatia hawa wamiliki wa ordinary shares endapo tu gawiwo litabakia.

Wamiliki wa shea za kawaida(ORDINARY SHARES) katika kampuni huwa hawa kiwango dhahiri cha gawiwo lao. Hawa gawiwo lao hutolewa kulingana na DIRECTORS watakavyo amua.

PREFERENCE SHARES -ni umiliki wa shares ambapo preferential shareholders anapewa kipaumbele cha kwanza katika kupewa gawiwo.Hawa preferential shareholders wanapata gawiwo pale tu kampuni inapopata faida.

Katika Preference shares, hapa wana kiwango dhahiri cha gawiwo lao(Specific Dividend Rate).
 
Reactions: efn
Ukiwekeza kwa kuweka hela yako ni kwa namna gani nitanufaika?

Kwa muda gani ntakuwa napata hio faida?

Hasa kama nimewekeza lets say 1 mil tshs
Kutokana na waraka uliotolewa kila hisa itanunuliwa kw sh.850. Kwa mwaka 2017 kila hisa itazalisha sh. 28 ambayo ni 3% ya bei ya hisa na mwaka 2018 kila hisa itazalisha sh.42 ambayo ni 5% ya bei ya kununulia. Kwahiyo uamuzi ni wako.
 
Tofauti kati ya hawa ordinary na Preference ipo katika nini hasa mbali na magawio yao....? Yani ni kiasi cha share wanazomiliki au...?
 
Mkuu kuna njia nyingi za kumiliki hisa katika kampuni.

1.Unaweza ukanunua kutoka kwa mmiliki wa hisa katika kampuni fulani mfano kuna mtu anamiliki hisa kwenye kampuni ya VODACOM na anataka kuuza hizo hisa zake unaweza ukazinunua mkuu(TRANSFER OF SHARES)

2.Kampuni yenyewe huwa inatangaza hiza zake na kuwaalika watu kununua hisa zao(ALLOTMENT OF SHARES)


Nielekezen namna ya kumiliki hisa
 
Kwaio ikizalisha sh 28, na sh 42, 2018 faida ipo wapi hakuna biashara ya kijinga kama hii aiseee mfano 850 x 10,000 = 8,500,000 baada ya mwaka ambayo itakua kwa sh 42 nitakua na hisa yenye thamani ya 892 x 10,000 = 8,920,000 kwaio mwaka mzima unasubiria faida ya sh 492,000....
 
Biashara kichaa hii...
Critical thinkers hawawezi kufanya upuuzi km huu...
 
Kwanza kwa kifupi huyo mtoa Uzi ni mwongo mwongo vodacom now ni kama ttcl tu...atuambie kwanza kwann hii 074.. Imerudi ..unatangaza kuuza hisa wakati kampuni imeanza kupoteza muelekeo
 
Ninavyoelewa utofauti wao unatokana na classes of shares you own in a particular company na siyo wingi wa hisa unazomiliki.

Kampuni katika utoaji au uuzaji wa hisa zao inakuwa imeweka matabaka ya hisa( classes of shares) ORDINARY SHARES NA PREFERENCE SHARES na na kila tabaka lina kuwa na haki zao.

Mfano katika preference shares, hapa shares ni redeemable lakini katika tabaka la ORDINARY SHARE, Hisa siyo redeemable.


Tofauti kati ya hawa ordinary na Preference ipo katika nini hasa mbali na magawio yao....? Yani ni kiasi cha share wanazomiliki au...?
 
Wakuu samahani naomba kujua zaidi kuhusu hii offer ya kununua hisa na vodacom....... Naomba u shee chochote unachokijua kuhusu hii offer..... Kwa mfano what should i expect nikinunua hisa 100 zenye thamani ya tsh 85k na mengine karibuni
 
Reactions: efn
Kutokana na waraka uliotolewa kila hisa itanunuliwa kw sh.850. Kwa mwaka 2017 kila hisa itazalisha sh. 28 ambayo ni 3% ya bei ya hisa na mwaka 2018 kila hisa itazalisha sh.42 ambayo ni 5% ya bei ya kununulia. Kwahiyo uamuzi ni wako.
hakuna kitu kama hiki mkuu,inazalishaje jio 28 na 42?hivi hufatilii soko ls hisa kuona bei za jisa zinavyopanda na kushuka?unaweza kununua hisa kwa 850 na baada ya muda kutokana na ufanisi wa kampuni,bei ya hisa ikashuka hata hadi kufikia 500...watanzania wengi hili hawalijui,wao wanajua tu faida itapatikana kitu ambacho si kweli,khna hasara pia,unatakiwa jjue vyote viwili faida na hasara kuna kimoja wapo hua kitatokea.Sas ili bei ya hisa za kampuni zipande thaman yani kutoka 850 kuja 900,kuja 1000 na kuendelea kuna mambo ya kufanyika.
1.Demand ya hizo hisa inatakiwa iwe kubwa kuliko supply yake sokon,yan watu wengi wawe na uhitaji wa kununua hizo hizo kutoka kwa wamiliki wake lakin na wamiliki nao wagome kuziuza au wauze kwa kiwango kidogo ...hapo bei lazima itapanda na kua kubwa hivyo thman ya hisa itaimarika
2.Management inatakiwa kujali wanahisa wake kama kuwapayia taarifa muhimu za kiuwekezaji,kuwapatia gawio kwa wakat muafaka kitu ambacho kitawajengea confidence wanahisa wake hivyo kutokuuza hisa zao hovyo kwa watu wengine na hivyo thaman yake kuongezeka
3.Kampuni inatakiwa kua wawazi,kulipa kodi stahiki,kujihusisha na shughuli za kijamii,kuyojihusishs na biashara haramu au kashfa ili ijenge uaminifu kwa wateja wake maana kama uaminifu hakuna na hiza mtu anaweza kuxiuza muda wowote bas wanahisa wengi wataikimbia kampuni kitu kitakochopelekea thaman ya hisa kudhuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…