Mbali na kuzungumzia suala la hisa leo, wajasiriamali wanashauriwa kusoma baadhi ya vitabu ambavyo waandishi wameandika mada mbalimbali za ujasiriamali ikiwamo uwekezaji katika hisa.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 84 ya Watanzania wakiwamo wasomi na wengine ambao hawajabahatika kusoma hawajui au hawana elimu kuhusu kuwekeza katika hisa.
Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba mada hii haijawekwa katika mitaala mbalimbali ya elimu. Kama ipo basi wale wanaostahili kuifundisha ama hawana uelewa mpana na uzoefu wa kuwawezesha wanafunzi wao kufahamu umuhimu wake katika medani za kiuchumi.
Hisa inaelezeka kwa namna mbalimbali, kwa ujumla wake hisa ni mali, rasilimali, kitegauchumi, hati miliki, biashara, dhamana ya mkopo, ni akiba, ni fedha iliyohifadhiwa, na ni mtaji.
Katika mtazamo wa kibiashara, hisa ni uwekezaji wa mtaji au fedha ambayo imewekezwa na mfanyakazi, mkulima, mfanyabiashara au mtu mwingine ambaye ameamua kununua hisa kutoka katika kampuni fulani kwa lengo la kupata faida kupitia gawio na ongezeko la bei ya hisa husika.
Uwekezaji katika hisa kama biashara nyingine unahitaji umakini na upembuzi yakinifu. Kufanya upembuzi wa wapi uwekeze fedha zako na wapi ununue hisa kwa msingi wa kupata faida.
Mjasiriamali au watu wengine wanaweza kufanya upembuzi yakinifu, lakini kama watu makundi niliyoyataja hapo juu wana uelewa wa kutosha na mbinu za kusoma taarifa mbalimbali za kampuni ambayo unakusudia kununua hisa. Kwa mfano, unapaswa kufanya upepenuzi yakinifu wa taarifa za fedha na hali halisi ya kampuni husika.
Uwekezaji katika hisa unachangamoto zake ikiwzmo kushuka kwa bei ya hisa, kukosa gawio, mfumuko wa bei, viwango vya riba, kukosa wanunuzi kutokana na ukwasi na hitilafu mbalimbali.
Kwa hali ya kawaida uwekezaji katika hisa una faida nyingi kuliko changamoto kwa mfano, kupata gawio baada ya kampuni kutengeneza faida, ongezeko la thamani ya hisa, punguzo la kodi ya zuio kwenye gawio.
Katika masuala ya hisa, hakuna kodi kwenye ongezeko la thamani, urahisi wa kuuza na kununua hisa, na ukiwekeza katika hisa unapata muda wa kufanya shughuli nyingine. Kwa upande mwingine hisa ni dhamana ya kupata mkopo, hisa ni urithi mzuri, ukijiwekea utaratibu wa kutenga asilimia fulani ya pato lako kutoka kwenye mshahara ama biashara kwa ajili ya kununua hisa ni uamuzi mzuri, na hisa pia ni utajiri.
Nawashauri na kuwakaribisha kuwekeza na Vodacom
Tembelea ofisi za Vodacom kwa Maelezo zaidi.
[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG]