shirima-wa-pili
Member
- Jan 1, 2013
- 23
- 21
tusubirie jua lizame kwenye matope ndo majina myapate.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana mkuu bado haujafika mwisho,Vipi huu uzi umefika mwisho?
Cc. Rakims
Sema hivi "nisubiri jua lizame ndio nipate hayo majina"tusubirie jua lizame kwenye matope ndo majina myapate.
Mkuu unaweza fanya upendeleo ukani PM japo majina machache? TafadhaliTupo pamoja wakuu najaza charge tu hapa
kabla ya kuijadili hoja yako lazima tujue umeiandika kwa Misingi ipi hasa?Kabla ya kuanza kusoma thread hii ifanyie Subscribe na kuifuatilia kila siku kuweza kuitambua vizuri elimu ya miujiza ya mungu na Maajabu ya dunia kwa ukaribu zaidi,
Hayo ni machache tu bado list inakuja na faida zake
Rakims
Hapana mkuu, mimi hapa nakupa muongozo tu wewe yatafute utakapo yapata basi mwenyezi mungu kakupa, na waandishi wa vitabu hivi wanakwambia usitumie kwa yasiompendeza mungu na usimpe asiyekuwa na hekima either ataumia au kuumiza wengineMkuu unaweza fanya upendeleo ukani PM japo majina machache? Tafadhali
Hii sio hoja mkuu hoja zipo jukwaa la hoja na siasa nenda katafute huko hojakabla ya kuijadili hoja yako lazima tujue umeiandika kwa Misingi ipi hasa?
Hoja yako imesimama katika msingi upi ?,
1.Msingi wa DINI (UKRISTO au UISLAM?)
2.Msingi wa HISTORIA?
3.Msingi wa SAYANSI?
4.Msingi wa SIASA?
ok kumbe ni FICTION hadithi za kufikirika tu,nilitaka nimbane kwenye NUTSHELL mtoa hoja bahati umesema sio hoja ni tamthilia za kusadikika tu! then mnaweza kujadiliana makinikia yenuHii sio hoja mkuu hoja zipo jukwaa la hoja na siasa nenda katafute huko hoja
Rakims
Sent using Jamii Forums mobile app
...Mkuu Rakims, unaposema hayo majina sio ruhusa kuyaweka hadharani na hapa sio hadharani ni familia moja ya JF, huoni faida iliyotarajiwa kutokana na somo hili inakuwa haifikiwa?Mkuu sio majina ya watu ni ya mwenyezi mungu na nguvu yaliyonazo,
Jamaa ni mzinguaji.Analeta mada alafu anaficha baadhi ya mambo....Mkuu Rakims, unaposema hayo majina sio ruhusa kuyaweka hadharani na hapa sio hadharani ni familia moja ya JF, huoni faida iliyotarajiwa kutokana na somo hili inakuwa haifikiwa?
Na je ruhusa ya kuyataja majina haya inatoka wapi?
Mimi kama mimi nikitaka kuyafamu ninamuomba nani ruksa??
Nitakushukuru kwa majibu mema...
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Acha uganga.Kabla ya kuanza kusoma thread hii ifanyie Subscribe na kuifuatilia kila siku kuweza kuitambua vizuri elimu ya miujiza ya mungu na Maajabu ya dunia kwa ukaribu zaidi,
Yatakayo jadiliwa:
1: majina ya kuamsha walinzi wa mbingu zote na faida zake
2: majina yaliyokuwapo kwenye fimbo ya Mussa na Nabii (Issa/Yesu) kufufulia wafu na kuponya na kauli alizotumia baba yetu Adam kuombea msamaha na faida zake
5: Majina ya kuamsha malaika wa Huruma
6: Majina yaliyopo kwenye Paji la uso wa malaika Jibril (Gabriel)
7: Majina yaliyofundishwa kwa malaika Mikail (Michael)
8: Majina yaliyofundishwa kwa malaika Izrail (Azrael)
9: Majina ya nguvu ya mbingu ya saba
10: Majina ya nguvu ya mbingu ya sita
11: Majina ya nguvu ya mbingu ya tano
12: Majina ya nguvu ya mbingu ya nne
13: Majina ya nguvu ya mbingu ya tatu
14: Majina ya nguvu ya mbingu ya pili
15: Majina ya nguvu ya mbingu ya kwanza
16: Majina ya nguvu ya sayari ya Saba (JUA)
17: Majina ya nguvu ya sayari ya sita (SUMBULA/JUPITER)
18: Majina ya nguvu ya sayari ya tano (MARIKH/Mars)
19: Majina ya nguvu ya sayari ya nne (Satan)
20: Majina ya nguvu ya sayari ya 3,2 na 1
Kwa kufupisha thread lisiwe refu zaidi majina yanayotumiwa na kila malaika wa ardhini na mbinguni in short ni majina mengi nitakayojaliwa nitayajadili ili muweze kupata elimu,
Kwa kuanza na majina ya kuamsha malaika watukufu wa mbinguni:
Majina yenyewe ni ********************
Siwezi kuyadhihirisha hapa kwa sababu si ruhusa kuyaweka public,
Maombi yake:
Ewe muumba, Mwenyezi mungu mmoja, wewe tu ndiye na unayestahiki kuabudiwa; wewe ni wa mwanzo na wa mwisho mwenye utawala wa kila kitu, wewe uliye hai bwana wa mabwana, mungu wa vyote muweza wa yote,mjuzi wa vyote, hakuna kisichotenda ila kwa mizani yako, wewe ndio unayepima tunayoona na tusiyoona...
Faida Zake:
Tambua kwamba mwenyezi mungu akikujaalia kupokea maombi yako kwa majina hayo niliyoyaficha hapo basi ukiyasema hali ya kuwa mwili wako ni msafi,nguo na mazingira yako na moyo mmoja malaika wa mwanga/roho takatifu watakutokea mbele yako na kila kitu mbinguni na ardhini vitatetemeka kwa hofu ya mwenyezi mungu mmoja..
Na unaweza kuyatumia majina hayo kwa kuita nafsi yoyote unayotaka, kuingia kwa mkuu yoyote bila matatizo na kuskilizwa,kukubaliwa utakacho,kufunga midomo ya watu,kupokelewa posa na kukubaliwa hata kama kwa mtoto wa mkubwa yoyote,kukidhiwa haja utakayo,kutolea mapepo kwenye miili ya watu,kuita yoyote au kumrudisha unaemtaka,kukinga,kuponya maradhi yasiyotibika na chochote utakacho omba kitakubalika kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi
Hii ni siri kubwa basi usiwafunfishe wasiokuwa na dini wala wasiona huruma wala imani wakatumia vibaya na kunyonyea watu, hivyo katika kujifunza funza kwako ukiyapata majina haya ya kumuombea mungu basi siri hii ifiche sio kila anayekuzunguka ni mwema..
2: Majina yaliyokuwapo kwenye fimbo ya Mussa (moses) na Alyoyatumia Yesu kuponya na kufufulia wafu
Haya ni majina katika list ya pili ambayo muumba aliyaumbia malaika wenye kusifu utukufu wake na utakatifu, ndio haya Adam (rehema na amani ziwe juu yake) aliyasema na Allah akamsamehe kosa lake,
Pia ndio haya Nabii Issa mwana wa Mariam/Yesu mwana wa Maria (rehema na amani ziwe juu yake) aliyatumia kufufulia wafu na kuponya wana wa Izrael, alikuwa akiwaponya watu kwa ruksa ya Allah na kufufua kama ukiwa msafi ukayasema, milima itatetemeka kwa utukufu wake:
Majina na Kauli zenyewe ni *************
Dua yake:
Wewe ni muumba,tofauti n wewe hakuna Mwenyezi mungu,mtakatifu kabisa kwa wale wanaokukumbuka na kukutii,pekee katika kila kinachoonekana na kisichoonekana unabudiwa, mwenye utakaso mkubwa kabisa wenye kukosa mipaka,pekee ndiye unayeombwa,unaeongoza kwenye njia nyoofu na mwenye kuwapa wenye kutoa Hakuna mungu isipokua wewe, mjuzi zaidi wa wale wanaojua,hakimu wa wenye kuhukumu,mwenye msaada mkubwa kwa wale ambao msaada unawafaa,hakuna mungu isipokua wewe, umejificha kwa ulivyoviumba, umejiwekea sifa zote njema wewe mwenyewe, wewe pekee ndio mwenye kumiliki majina mazuri,umevifanya vitu kuwa kwa elimu na nguvu, unapoombwa unajibu, umehifadhi mwanzo na mwisho wa kila kiumbe, wewe ni mfalme,mwenye nguvu,Mmoja na wapekee,mmiliki wa vyote hakuna mungu unayemtegemea upo peke yako,umejawa na neno na kauli tu na ukitaka jambo kuwa linakuwa. Wewe ni Mungu Mjuzi na mkuu, moyo wa kila kiumbe upo mikononi mwako, na unauwezo wa kuvigeuza utakayo kwa kusema tu, kauli ni zile unazozungumza tu,utambuzi ni wako pekee. Hukumu, ni hukumu yako pekee, hakuna wa kupinga amri yako, hakuna wa kujua ambacho hujaruhusu ajue, Wewe ni wa Mwanzo na wa Mwisho,
FAIDA ZAKE:
Fahamu ewe ndugu yangu haya majina yalikuwa kwenye fimbo ya Mussa (rehema na amani ziwe juu yake) ni majina 31 kumi kila upande na la kati yao ndio mtu anaweza kufanya muujiza wowote na ndio jina kuu la siri la Mwenyezi mungu basi washindane na wanaoshindana hakika atakae lijua atafunuliwa mengi wanayoyajua watu na wasioyajua, na yote kwa ujumla basi huweza kufanya maajabu yenye kufungua loki zote za duniani,kuvunja uchawi na nguvu za giza,kufunga ndimi,kutawanyisha mapepo,kushinda maadui,na kuvuta malaika yoyote wa ardhini na makudam wowote wa mbinguni na ardhini,unaweza ukayatumia kwa kukuzia mazao,kukata chochote,kutenganisha,kupendwa,kuvuta waliombali,na kukidhi mahitaji yote, kwa nguvu ya Allah unatakiwa uyatumie kwa mambo ya haki tu,
Miongoni mwa maajabu yake ukiyaandika kwenye kioo kwa usiyekuwa na imani wala usiyesali na ukayalaza nje usiku saba kwa kufuata taratibu, basi kioo hicho unaweza ukakitumia kuita yoyote au chochote kikaja na ukaagiza unavyotaka au unaweza ukamuita yoyote na kumuuliza mambo yake na akakwambia hakuna utakachoita kikagoma kuja, pia unaweza kutumia kwa kutafuta ulichoibiwa na kikarudi na hazina zilizojificha,
Unapoyataja majina hayo basi malaika watakutokea kila mmoja wao mbawa zake zitakuwa mbili na moja inagusa mashariki mwa dunia na nyingine inagusa magharibi mwa dunia na wanaweza kufanya chochote unachotaka,
Nitaendelea baada ya muda,
Hapa nitareveal all the secrets of people who think they are extraodinary, wanajificha na kujidhirisha kwenye mwamvuli wa majina ya mungu, kauli na majina mbali mbali na kufanikiwa
Hayo ni machache tu bado list inakuja na faida zake
Rakims
Habari mkuu, kwanza kabisa nikutakie kufaidika katika kuyapata majina hayo lakini pia ni majina ambayo mimi ninaanza kukupa funguo kwamba kuna majina yapo hivi na yanatumika hivi sasa inabaki kazi kwako kuweza kuyapata na kuyatumia, hapa kwenye forum kuna watu tofauti tofauti believers na non believers sasa unapoweka vitu hivi hadharani inaweza kuwa na maana mbovu kwa majadiliano au kwa mawazo ya watu, ni sawa na wewe uwe msikitini kwa wanaume halafu aingie jike kavaa kimini, maana ipo wapi?...Mkuu Rakims, unaposema hayo majina sio ruhusa kuyaweka hadharani na hapa sio hadharani ni familia moja ya JF, huoni faida iliyotarajiwa kutokana na somo hili inakuwa haifikiwa?
Na je ruhusa ya kuyataja majina haya inatoka wapi?
Mimi kama mimi nikitaka kuyafamu ninamuomba nani ruksa??
Nitakushukuru kwa majibu mema...
Sent using Jamii Forums mobile app
Vizuri mkuu, ndio maana ni elimu ambayo huipata wachache sana miongoni mwetu,Jamaa ni mzinguaji.Analeta mada alafu anaficha baadhi ya mambo.
Hana lengo la kuelimisha zaidi ya kutaka maslahi flani flani hivi kupitia hayo majina.
Huenda ukimpatia mshiko au ukiendana na matakwa yake atakutajia.
Kaishia kuelezea dua za waliyoyatumia majina ya MUNGU MWENYEZI na zilivyopokelewa kwa heshima ya hayo majina alafu mwisho wa siku hataki kuyataja hayo majina.
Sioni jipya kwa mtoa mada na wala sijapata elimu yoyote hapo.
Sent using Jamii Forums mobile app