Faida za tunda la ukwaju


Hasante, na juisi ya ubuyu ina eaida gani?
 
Nimempa mwanangu ukwaju kwenye uji na kwenye juice . ucku kalal kuliko kawaida yaani no kujitingisha wala kuangaika mpaka nikaogopa, ila mzima wa afya njema tuu
 
Inasaidia mzigi kutoka kiulaini muda wa kukata gogo aisei...
 
Acha uongo! Nimekula sana ukwaju na ubuyu hakuna faida niliyopata zaidi ya meno kufa ganzi...
 
Safi Sana Ukwaju Tuutumie Vema
Ukinywa Wa Kutosha Glass Tatu Ukae Jirani Na Maliwato
 
Juice ya ukwaju ni katika vinywaji asilia ambavyo ni muhimu sana hasa kwa watu wanaoishi mazingira ya joto. Sifa moja kubwa ya ukwaju ni kulainisha choo. Kumbuka mtu anapokuwa hapati choo vizuri anapata matatizo mengi sana ikiwemo kuumwa na kiuno, kungurumwa na tumbo. Kukosa hamu ya kula na baya zaidi husabisha upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume na kukosa hamu ya tendo la ndoa na kuchelewa au kushindwa kufika kileleni kwa mwanamke. Kwa hio unapotumia juice ya ukwaju mara kwa mara tatizo hili hupungua. Vile vile ukwaju unapoza mwili... Hivyo kuwa kinywaji murua nyakati za joto kali.Ukwaju ni kinywaji kizuri kwa watu wenye pressure ya kupanda (hypertension). Vile vile ukwaju ni chanzo kizuri cha vitamin C hivyo kuboresha kinga ya mwili dhidi ya maradhi. Hayo ni machache niliyofanikiwa kukuleteeni kuhusiana na ukwaju ambao mbali ya kutengenezwa juice pia hutumiwa kama kiungo cha mchuzi kutokana na umuhimu wake kwa mwanadamu. Wadau mnaoweza kuongezea kuchangia mnakaribishwa
Karibuni sana!
 
Inategemea makusudio yako.... Lkn juice ya kawaida iliyowekwa sukari haina madhara.... lakini ikiwa baridi inaweza kukuletea matatizo ya tumbo.
 
Hapo kwenye kiungo cha Mboga ni balaa na unanikumbusha Enzi za Miaka hiyo huko kijijini kwetu. Hii kitu ikiungwa kwenye samaki aina zote ambazo ni bado wabichi siyo wa kula Usha Nakwambia mchuzi wa hapo unaweza ukanywa sufurua zima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…