Faida za UMASKINI

Faida za UMASKINI

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Leo ngoja nikupe faida za UMASKINI,.
Unaambiwa katika dunia kila kitu kina hasara na faida. Hivyo kabla kufikilia kufanya unashauliwa kuanza kuangalia pande zote mbili yaani (ADVANTAGE na DESADVANTAGE ) kimombo changu changu kinaweza kisiwe sawa ni kutokana na kiwango chagu cha elimu.
Pia kama wewe ni mpambanaji na unapambana juu ya umaskini na hali ya maisha uliyonayo kwasasa basi nikutie moyo pambana sana, kwamaana FAIDA za umaskini si lolote si chochote ukilinganisha na hasara zake.

Sina sababu za kumuelezea sana maskini kwa maana maskini wenyewe mnajijua na matajiri pia mnajijua.

Faida kubwa za UMASKINI
1. MASKINI HANA SIKU YA HUKUMU
maskini ukifa umekufa, maskini haukumiwi maskini ni laana ambayo Mungu alishakupa duniani na mahangaiko yako. Kama unahisi kuwa utahukumiwa ukifa wewe sio maskini labda wale matajiri.
Maskini haambiwi atoea sadaka wala haambiwi aende kuiji makka wala haulazimishwi kwenda ibadani wewe ibada yako ni kuhangaika. Nenda kahangaike na kulipia watoto ada, nenda kahangaike na pango za nyumba nenda kahangaike na kula maswala ya kwenda kuimba ibadani waachie walio jipata, na Mungu atakuwa pamoja na wewe.


2. MASKINI HAFIRISIKI
Maskini hawazii sijui kufirisika, sijui kushuka kiuchumi,.
Maskini akipata poa akikosa poa pia.

3. MOYO WA MASKINI NI WENYE UTULIVU
Ndio maskini hupata tabu ya mwili, ila kapewa amani ya akili na mwenye moyo mtulivu na amani.
Maskini haitaji ulinzi wa mabaunsa mlangoni kwake, wala haitaji kupima chakula kabla ya kukila. Maskini huokota tunda na kulila bila kuwaza, tena bila kuzulika.

4. MARA NYINGI ANAKUWA HURU
mara nyingi anakuwa jamiiforum, mara nyingi anakuwa kijiweni kwenye vijiwe vya kawaha nk, mara nyingi hupenda kuzunguka zunguka na kuranda mitaani huku na kule na ndio wengi wao tunawaona facebook instagram na X.

5. KUNYWA POMBE ZA KIENYEJI
Kati ya vitu maskini huwa anafaidika navyo ni pombe za kienyeji, pombe ambazo zimejaa mambo mengi mazuri na yenye furaha.

6. UMASKINI HUFA JASIRI
Maskini haachi majumba makubwa , magari wala viwanja.
Huchumia tumbo lake mpaka mwisho wa pumzi yake.
Huyu ndio mwamba, anakuja kwenye dunia na kuondoka bila kuacha ushahidi. Mr silent

Amini amini nawaeleza hukumu ya MASKINI imeshapita tokea duniani.


1.huna hofu ya kuvamiwa na wezi mana hakuna mali ya thamani kwako ya wao kuiba.

2.Huna haja ya kwenda gym kufanya mazoezi maisha yako ni mazoezi tosha

3.Huna haja ya kukataa ndoa mana mke wako ni wife material hayupo kwako kimaslahi.

4.Huwezi kupata unene(magonjwa ya unene) kwa sababu ya kula ovyo ushauri wa dr janabi wa kula kidogo wewe unaufuata automatically.
 
Alafu umaskini raha yake huwezi sikia unaumwa magonjwa ya ajabu ajabu eti sijui cancer mara add sijui alzaimers au kisukari na presha.

Mwisho kabisa maskini tunakula mbususu kavu kavu. Hakunaga maskini anagegeda na condom hizo ni za wasomi na matajiri
 
Back
Top Bottom