Faida za Vitamini D

Faida za Vitamini D

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Binadamu huhitaji Vitamini D ili kuimarisha kinga ya mwili na afya ya mifupa, kupambana na aina mbalimbali za saratani pamoja na kuboresha usafirishwaji wa taarifa za mfumo wa fahamu na mijongeo ya misuli.

Upungufu wake husababisha kutokea kwa tatizo la kudhoofika na kupinda kwa mifupa (Matege) kwa watoto na kupungua ujazo wa mifupa kwa watu wazima. Pia, husababisha maumivu ya misuli, kudhoofika kwa kinga ya mwili na kwa baadhi ya watu huongeza nafasi ya kupatwa na mzio (allergy).

5C9F8C5C-C7B9-4898-A7FD-ED190E009164.jpeg


Kiasili, mwili wa binadamu hutengeneza vitamini hii kwa kutumia mwanga wa jua. Pia, inaweza kupatikana kutoka kwenye vyakula vichache kama maini ya wanyama, kiini cha yai, maziwa, mafuta ya samaki pamoja na baadhi ya aina za uyoga.

Chanzo: NIH
 
Back
Top Bottom