Faili la Makabidhiano ya Urais wa JMT na yaliyomo ndani kwa mtazamo wangu Mimi

Faili la Makabidhiano ya Urais wa JMT na yaliyomo ndani kwa mtazamo wangu Mimi

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari za pilika Wana JF Wenzangu.
Niende madani.


Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza kwenye faili la Makabidhiano ya Urais Kuna nini ndani yake? Niliwaza hili wakati Rais Mkapa akikabidhi nchi kwa Rais Kikwete na Pia wakati Kikwete naye akimkabidhi Rais Magufuli. Hili jambo ni Muhimu kwani huu mwaka wa uchaguzi na sio ajabu akawepo Rais mpya.

Nimekuwa nikiwaza Ikulu inakabidhiwaje? Nchi inakabidhiwaje? Nimekosa mtu sahihi wa kunijuza na leo nikaja na mabunio au kubumba Kama sio assumptions zifuatazo.

1. Rais mpya hukabidhiwa Majengo yote ndani ya Ikulu kwa kutembezwa na kuoneshwa Kila jengo, chumba na matumizi yake ikiwa ni pamoja na faili la majengo hayo.

2. Rais mpya hukabidhiwa Rasilimali watu wote wa Ikulu na hivyo ni jukumu lake kubaki nao au laahh.

3. Rais mpya hukabidhiwa faili la maeneo yote ya nchi kuanzia idadi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata, na idadi ya vijiji na mitaa yote nchini. Majina sio lazima, ni idadi tu.

4. Rais mpya hukabidhiwa idadi yote ya Mashirika ya umma na mamlaka mbalimbali za serikali na majina yake.

5. Rais mpya hukabidhiwa faili la majeshi yote ya ulinzi na usalama na idadi ya Askari Kila jeshi. Sio majina ya Askari, ni idadi tu kwa Kila jeshi.

6. Rais mpya hukabidhiwa faili la Rasilimali zote nchini Kama wanyama pori, madini, misitu, viwanda vya umma Kama vipo, maziwa, bahari, ukubwa wa aridhi ya Tanzania mfano km za mraba........, Gesi, Mafuta au petroli iliyopo aridhini na Rasilimali nyinginezo. Baadae huambiwa awe tayari kufa akizilinda. Aridhi yetu ndiyo imebeba vyote hivyo na ndiyo kitu cha kuanza kulindwa na Rais ktk Rasilimali.

7. Rais mpya hukabidhiwa faili la makadirio ya idadi ya Watanzania waliopo nchini, nje ya nchi na idadi ya wageni waliopo nchini.

8. Rais mpya hukabidhiwa majina ya wizara zote na muundo wa Kila wizara.

9. Rais mpya hukabidhiwa faili la mapato ya nchi na mwelekeo wa uchumi ktk kipindi husika. Hapa mchanganuo wa sekta inayochangia zaidi hadi ya mwisho bila kuandika longongo nyingi.

10. Rais mpya hukabidhiwa faili la msimamo wa nchi ktk masuala mbalimbali ya kitaifa. Taifa liegemee au kutogemea upande wowote.

11. Rais mpya hukabidhiwa kitabu cha katiba ya nchi aitetee na kuilinda.

12. Rais mpya hukabidhiwa kitabu cha ilani ya chama chake Kama Rais anayeondoka na ajaye wanatoka chama kimoja kutakiwa kuilinda na kuitekeleza. Hata Kama anacho atapewa upya.

13. Rais mpya hukabidhiwa faili la madeni ya nje na ndani. Madeni yote ambazo nchi inadaiwa.

14. Mwishowe huambiwa Mshahara wake na Rais anayemaliza muda wake.

Nawe njoo na mabunio yako. Nikipata bunio jingine nalileta.

Karibuni.

Mods chondechonde nipo chini ya miguu yenu. Hili jukwaa la Great Thinkers.
 
hukabidhiwa idadi ya wafungwa...

hukabidhiwa faili lenye idadi ya marafiki na maadui wa nchi.

hupewa mafaili mawili ya viapo kimoja Cha shetani kingine Cha Mungu kwamba achague ataongoza kwa msaada wa Nani maana hao wawili Ni superpower.
 
Atakae kabidhiwa ni Benard Membe kama jpm akishindwa!CCM hawawezi kumpa mpinzani wa kweli TUNDU LISU!!!NAUONA MNYUKANO MKALI SANA !!!
 
Atakae kabidhiwa ni Benard Membe kama jpm akishindwa!CCM hawawezi kumpa mpinzani wa kweli TUNDU LISU!!!NAUONA MNYUKANO MKALI SANA !!!
Je Kuna kitu Muhimu cha kumkabidhi huku nimekisahau
 
Lissu Atakabidhiwa File LA Mrembe Wakati Magu Ataapishwa Amalizie ngwe yake
 
hukabidhiwa idadi ya wafungwa...

hukabidhiwa faili lenye idadi ya marafiki na maadui wa nchi.

hupewa mafaili mawili ya viapo kimoja Cha shetani kingine Cha Mungu kwamba achague ataongoza kwa msaada wa Nani maana hao wawili Ni superpower.
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji87][emoji87][emoji87][emoji15][emoji15][emoji15][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Katika vyote KATIBA ya nchi ndio muhimu kuliko vyote
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji87][emoji87][emoji87][emoji15][emoji15][emoji15][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
mkifika wawili mnashangaa hii post yangu naifuta..

[emoji853][emoji853]
 
Back
Top Bottom