Faili la Makabidhiano ya Urais wa JMT na yaliyomo ndani kwa mtazamo wangu Mimi

Faili la Makabidhiano ya Urais wa JMT na yaliyomo ndani kwa mtazamo wangu Mimi

Kwanza hili ni jambo geni kabisa kutokea kama upinzani utashinda ...lakini cha kwanza kabisa...Rais mteule atakuwa rasmi chini ya ulinzi wa usalama wa taifa jeshi na organs nyingine za kiusalama
Halafu handover itafanyika kwa hatua kuanzia katiba na makabrasha yote muhimu ikulu mpaka wizara na vitengo vyake vyote
Makabidhiano muhimu yatakapokamilika ndio tendo la kuapishwa rasmi litafanyika...kwa kipindi chote kabla ya makabidhiano usalama wa taifa ndio watakuwa na majukumu makubwa ya kiusalama na nyendo zote za rais mteule

Kwasasa haitabiriki ninini kitatokea kwakuwa mpaka sasa chama dola hakijatoa tamko lolote kama kikishindwa kitakabidhi nchi kwa ridhaa na kwa amani
 
hukabidhiwa idadi ya wafungwa...

hukabidhiwa faili lenye idadi ya marafiki na maadui wa nchi.

hupewa mafaili mawili ya viapo kimoja Cha shetani kingine Cha Mungu kwamba achague ataongoza kwa msaada wa Nani maana hao wawili Ni superpower.
Duh..
 
Asante kwa kuboresha mawazo yangu
 
Raisi mpya atapewa lile begi jeusi ambalo raisi akiwa nje ya ikulu wale vijana wake wanakuwa nalo..
 
Habari za pilika Wana JF Wenzangu.
Niende madani.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza kwenye faili la Makabidhiano ya Urais Kuna nini ndani yake? Niliwaza hili wakati Rais Mkapa akikabidhi nchi kwa Rais Kikwete na Pia wakati Kikwete naye akimkabidhi Rais Magufuli. Hili jambo ni Muhimu kwani huu mwaka wa uchaguzi na sio ajabu akawepo Rais mpya.

Nimekuwa nikiwaza Ikulu inakabidhiwaje? Nchi inakabidhiwaje? Nimekosa mtu sahihi wa kunijuza na leo nikaja na mabunio au kubumba Kama sio assumptions zifuatazo.

1. Rais mpya hukabidhiwa Majengo yote ndani ya Ikulu kwa kutembezwa na kuoneshwa Kila jengo, chumba na matumizi yake ikiwa ni pamoja na faili la majengo hayo.

2. Rais mpya hukabidhiwa Rasilimali watu wote wa Ikulu na hivyo ni jukumu lake kubaki nao au laahh.

3. Rais mpya hukabidhiwa faili la maeneo yote ya nchi kuanzia idadi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata, na idadi ya vijiji na mitaa yote nchini. Majina sio lazima, ni idadi tu.

4. Rais mpya hukabidhiwa idadi yote ya Mashirika ya umma na mamlaka mbalimbali za serikali na majina yake.

5. Rais mpya hukabidhiwa faili la majeshi yote ya ulinzi na usalama na idadi ya Askari Kila jeshi. Sio majina ya Askari, ni idadi tu kwa Kila jeshi.

6. Rais mpya hukabidhiwa faili la Rasilimali zote nchini Kama wanyama pori, madini, misitu, viwanda vya umma Kama vipo, maziwa, bahari, ukubwa wa aridhi ya Tanzania mfano km za mraba........, Gesi, Mafuta au petroli iliyopo aridhini na Rasilimali nyinginezo. Baadae huambiwa awe tayari kufa akizilinda. Aridhi yetu ndiyo imebeba vyote hivyo na ndiyo kitu cha kuanza kulindwa na Rais ktk Rasilimali.

7. Rais mpya hukabidhiwa faili la makadirio ya idadi ya Watanzania waliopo nchini, nje ya nchi na idadi ya wageni waliopo nchini.

8. Rais mpya hukabidhiwa majina ya wizara zote na muundo wa Kila wizara.

9. Rais mpya hukabidhiwa faili la mapato ya nchi na mwelekeo wa uchumi ktk kipindi husika. Hapa mchanganuo wa sekta inayochangia zaidi hadi ya mwisho bila kuandika longongo nyingi.

10. Rais mpya hukabidhiwa faili la msimamo wa nchi ktk masuala mbalimbali ya kitaifa. Taifa liegemee au kutogemea upande wowote.

11. Rais mpya hukabidhiwa kitabu cha katiba ya nchi aitetee na kuilinda.

12. Rais mpya hukabidhiwa kitabu cha ilani ya chama chake Kama Rais anayeondoka na ajaye wanatoka chama kimoja kutakiwa kuilinda na kuitekeleza. Hata Kama anacho atapewa upya.

13. Rais mpya hukabidhiwa faili la madeni ya nje na ndani. Madeni yote ambazo nchi inadaiwa.

14. Mwishowe huambiwa Mshahara wake na Rais anayemaliza muda wake.

Nawe njoo na mabunio yako. Nikipata bunio jingine nalileta.

Karibuni.

Mods chondechonde nipo chini ya miguu yenu. Hili jukwaa la Great Thinkers.
Unamwanga katika hayo hata Kama no makisio
 
hukabidhiwa idadi ya wafungwa...

hukabidhiwa faili lenye idadi ya marafiki na maadui wa nchi.

hupewa mafaili mawili ya viapo kimoja Cha shetani kingine Cha Mungu kwamba achague ataongoza kwa msaada wa Nani maana hao wawili Ni superpower.
Hahahahah hizo superpower mbili hapo mwisho daaah
 
Hivi ni kweli ktk uongozi wa juu wa nchi lazima nguvu za giza ziwepo?
sio nguvu za Giza tu Bali hata nguvu za Mungu zipo.nimesema hapo juu Ni wewe tu kuchagua utaongoza kwa msaada wa Nani Kisha unasain.

Ila nimeandika maoni kulingana na uzi husika.

don't take it serious

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom