Fainali CECAFA U20: Tanzania bara VS Kenya

SPINE

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2017
Posts
1,068
Reaction score
1,150
Timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20 itacheza mchezo wa fainali dhidi ya vijana wenzao kutoka Kenya katika mashindano ya Cecafa U20 yanayofanyika nchini Uganda. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo kuanzia majira ya saa 9:30 alasiri ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Itakuwa ni patashika kati ya wababe wawili Tanzania Bara dhidi ya Kenya ambao kwenye hatua ya makundi walitoshana nguvu kwa kutoka sare ya 2-2.

FUFA online TV na Azam XTRA wanategemea kuonyesha mchezo huo live.
 
Ndio nchi gani hii? Nime Google siioni


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Ndivyo inavyotambuliwa kwenye hayo mashindano mkuu maana Zanzibar nayo ilishiriki....Nadhani CECAFA hawaitambui Tanganyika ila wanatambua Zanzibar na Tanzania....lol 🤔 🙄😳
 
SPINE karibu kuokoa jahazi. Njoo mzalendo,hiyo channel ya Azam extra hawana habari na game
 
SPINE karibu kuokoa jahazi. Njoo mzalendo,hiyo channel ya Azam extra hawana habari na game
Mpira umeshaanza......check kupitia FUFA online Tv.....link hapo chini
 
Tusubiri kipindi cha pili kitaamuaje
 
Naona hiyo online tv tunayo iangalia kupitia Azam Xtra, muda mwingi inautumia kusearch tu! Hata ile ladha ya kuangalia mechi inakosekana kabisa.
Kwa hili waganda wamechemka aisee!

Fainali haina hata mvuto! Uwanja uko maporini! Hovyo kabisa. Ila mwisho wa yote, nawatakia vijana ushindi.
 
Waganda wamechemsha sana kuandaa haya mashindano......ila nasi television yetu ya taifa inaonyesha nini?? Timu ya taifa inacheza nchi jirani lakini haiwezi kuonyesha mpira live, vijana wakishinda mnawaita bungeni na ikulu....hovyo kabisa.
 
Tumeshindaaaaa,1-0. Hongera vijana..
 
Hongera Ngorongoro heroes
 
TFF ni wakati sasa muwe na online TV yenu tuwe tunaona mechi za timu ya taifa online maana TBC wapo kichama zaidi, hawajali mechi za timu ya taifa kabisa.
 
Vijana wako vizuri, ila shida ni muendelezo wao, tff haina program nzuri ya kuwaendeleza hawa vijana.
 
Hongereni sana vijana kwa kupambana na pia kwa kutulipia kisasi cha Afcon kwa majirani zetu manyang'au wa Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…