Fainali kombe la Mapinduzi, Simba zaidi ya uijuavyo

Fainali kombe la Mapinduzi, Simba zaidi ya uijuavyo

sembo grafani11 umeona mtaalamu wetu huyu?

Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema ana taarifa kuhusiana na viwanja vibovu.

Koponovic tokea ametua nchini hajawahi kucheza mechi katika kiwanja kibovu.

Aliiongoza Simba kutwaa kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar ambao ni safiii. Halafu akaenda kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu kwenye Dimba la Nangwanda mjini Mtwara ambalo lina moja ya viwanja vizuri vya kuchezea.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Kopunovic amesema ana taarifa ya baadhi ya viwanja kuwa hoi kwa ubovu.

"Nimeambiwa kuhusiana na hilo, hii ni Afrika nalichukulia kama changamoto.

"Usisahau nimefanya kazi Rwanda kwa miaka mitatu, kuna changamoto nyingi nimekutana nazo na huenda zikawa zinafanana na hizi zilizopo.

"Hivyo ni suala la muda tu na kujua nini cha kufanya wakati tunakabiliana nazo," alisema Mserbia huyo.

Source: Saleh Jembe
 
Last edited by a moderator:
Freeland kiwanja kibovu kimebakia kimoja tu, nacho ni jamhuri stadium cha moro, labda na mkwakwani.. ila naamini hata huko Goran Kopunovic ataendeleza dozi zake.
 
Last edited by a moderator:
Huyu naye siku zake zinahesabika.. jumamosi polisi wanamtupa lupango milele.
Hao wakifungwa na Polisi tumewapoteza, maana hawakawii kujitoa kwenye Ligi Kuu kwa kisingizio cha kukamiwa na kila timu.
 
Freeland kiwanja kibovu kimebakia kimoja tu, nacho ni jamhuri stadium cha moro, labda na mkwakwani.. ila naamini hata huko Goran Kopunovic ataendeleza dozi zake.
Mkuu hivi Yanga wakisema wanajiandaa kucheza kwenye kiwanja kibovu ili wapate matokeo mazuri, kwani zile sare mfululizo zote wamechezea Jamhuri Stadium?
 
Freeland kiwanja kibovu kimebakia kimoja tu, nacho ni jamhuri stadium cha moro, labda na mkwakwani.. ila naamini hata huko Goran Kopunovic ataendeleza dozi zake.

Kuna kaitaba kule hua kunajaa maji
Hata Jamhuri nadhani bado ni shida
Mkwakwani ni shida
Sokoine status vipi?

cc grafani11

Yanga are never serious mkuu......hawajui kuwa wana timu ya mababu....wao ni wajanja wa visingizio

Next time watagomea mechi ya polisi kwa sababu ni timu ya jeshi

Ila tukikutana nao ...watamtimua huyu babu wao
 
Mkuu Kaitaba hivi sasa inakarabatiwa, kwa hiyo mechi zote zinachezewa Kirumba Stadium.
Sokoine Stadium kabla ligi haijaanza waliukarabati, nadhani sasa utakuwa fresh.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu tupo sana, sema tu nyuzi zenu zimekuwa za muda mrefu sana. Pamoja sana Wakuu.
 
Mkuu Kaitaba hivi sasa inakarabatiwa, kwa hiyo mechi zote zinachezewa Kirumba Stadium.
Sokoine Stadium kabla ligi haijaanza waliukarabati, nadhani sasa utakuwa fresh.
Wakifungwa watakuja na kusingizio kingine
 
Wakuu tupo sana, sea tu nyuzi zenu zimekuwa za muda mrefu sana. Pamoja sana Wakuu.

Pamoja sana Legendary Makoye Matale......

Bahati mbaya Jumamosi itakuwa ni sabato mkuu

Nahisi hatutakuwa pamoja hapa mtakapotolewa kamasi na polisi
 
Last edited by a moderator:
Hata jana ulikuwa ibadani mkuu?

Ndiyo. Sasa hivi tunaendelea na Mahubiri ya hadhara kwa watu wote kila jioni. Nachukua fursa kukualika ukaribie katika kanisa lolote la Waadventista Wasabato lililo karibu nawe kila jioni majira ya saa 10.

Karibu sana na Mungu akubariki.
 
Ibada inamalizika saa ngapi?
 
Back
Top Bottom