Fainali Mapinduzi Cup 2019: Azam FC 2 - 1 Simba SC

MySoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
209
Reaction score
297
ZIMEBAKI saa kadhaa kabla ya Klabu ya Azam FC kuvaana na Simba katika fainali ya Kombe la Mapinduzi itakayofanyika Uwanja wa Gombani, Pemba leo saa 9.30 jioni.

Wakati Azam FC ikitinga fainali baada ya kuichapa KMKM mabao 3-0, Simba yenyewe imeshinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 3-1 dhidi ya Malindi kufuatia dakika 90 kumalizika kwa suluhu.

Mchezo huo unakumbushia fainali ya mwaka 2017, Azam FC ilipoifunga Simba bao 1-0, bao lililofungwa na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Himid Mao ‘Ninja’, kwa shuti la mbali lililomshinda aliyekuwa kipa wa Simba, Daniel Agyei.

Azam FC itaingia kwenye mchezo huo ikisaka taji la tano la michuano hiyo, na ubingwa wa tatu mfululizo, utakaoifanya kuandika rekodi mpya ya kuwa timu pekee kuwahi kufanya hivyo.

Kila ikiingia fainali, Azam FC mara zote imeweza kufanikiwa kutwaa taji hilo, ambapo kihistoria imelitwaa mwaka 2012, 2013, 2017, 2018.


Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa, ataingia kwenye mchezo huo akitaka kuendeleza moto wake wa kufunga mabao hadi sasa akiwa ndiye kinara wa kupachika mabao kwenye michuano hiyo, akiwa amefunga manne.

...........
Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura jana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wachezaji watatu wa Simba wamesafiri leo kuelekea Zanzibar kuongeza makali ya Mapinduzi CUP.

Haruna Niyonzima, Rashid Juma na Shiza Kichuya ndiyo waliosafiri kuelekea visiwani humo tayari kwa fainali hiyo.

Simba ilitinga fainali baada ya kuiondoa Malindi FC kwa mikwaju ya penati ikiwa ni baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya 0-0.


=====

Azam FC wananyakua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuifunga Simba SC Tanzania mabao 2-1 kwenye fainali iliyopigwa Uwanja wa Gombani huko Pemba.
 
1.Salim
2.Zana Kulibali
3.Asante Kwasi
4.P.Bukaba
5.Yusuf Mlipili
6.
7.Mo Ibrahim
8.H.Niyonzima
9.Rashid Juma
10.Adam Salamba
11.Shiza Kichuya
 
Mlipili Yusuf analevel aggregate hapa, one one dakika ya 63.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…