Fainali ya CAF: Yanga inahitaji washambuliaji katili kama Tumisang Orebonye, Aymen Mahious na Golikipa Djigui Diarra

Fainali ya CAF: Yanga inahitaji washambuliaji katili kama Tumisang Orebonye, Aymen Mahious na Golikipa Djigui Diarra

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Yanga imefikia levo za CAF, kwenye level hizo hakuna timu za ajabu ajabu, kwenye levo za CAF hakuna wachezaji wanaosita sita kupiga pasi na anapoamua kupiga pasi anapoteza, kwenye levo za CAF hakuna mchezaji anayekosa ndani ya boksi la kumi na nane, kwenye levo za CAF hakuna kiungo mshambuliaji anayeona ukuta wa adui na kurudisha nyuma, kwenye level za CAF, utawakuta magolikipa kama Djigue Diarra anayedaka mikwaju ya penalty utadhani yeye ni "screen protector" kwenye levo za CAF utawakuta washambuliaji katili kama Tumisang Orebonye na Aymen Mahious, kwao kosa moja wanakuadhibu.

Yanga inahitaji washambuliaji jangili "goal poacher" mshambuliaji anayepora mpira pale unaposita kumpiga chenga, mshambuliaji anayegusa mpira ndani ya kumi na nane na kuweka kambani, Yanga inahitaji "Goal king" mfano wa Fiston Mayele lakini awe mwenye uwezo wa kupiga goli tatu kila mechi kama Jean Baleke na kuamua mechi kama Kennedy Musonda. Yanga inahitaji kiungo mshambuliaji kama Luis Miquissone, sio Tuisila mwenye kufinya na kupoteza mpira. Yanga inahitaji ukuta imara usio katika hovyo na kusababisha madhara, na kumsubiri Golikipa Djigui Diarra atuokoe. Yanga inahitaji kusajili kaliba ya wachezaji wa Al Ahly, Wydad ama Raja Casablanca. Yanga inahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kucheza na Mamelodi Sundowns na kuwafunga. Yanga inatakiwa kuwa na wachezaji wenye skills kama Benard Morrison, Sure Boy na Djuma Shaban. Yanga inahitaji kuwa timu inayoweza kuifunga saba, klabu ya Al Ahly, AS Vita, Al Merrikh, Kaizer Chiefs na Wydad AC.

Yanga wamejitaidi ila hawapaswi kupewa hongera kwa sababu hawajachukua kombe. Yanga mlipaswa kuchukua kombe ili mvunje miiko, kila mchezaji alitakiwa kushinda mechi zake, sio kama Essien aliyesema ndugu zake wanamloga au Emmanuel Adebayor aliyesema Mama yake ndiye anamloga, ni dhahiri kuanzia dk65 hakuna mpira uliochezwa. Pengine Usm Alger walifanya uhuni na uchafuzi wa mpira ndio maana mataifa ya Magharibi ya mbali wanaicheka na kuishangaa Africa, lakini Yanga ilipata nafasi hazikuzaa goli, tunahitaji washambuliaji katili na jangili "goal poacher" na kiungo mwenye kuufuata ukuta wa adui na kuupenya kama Luiz Miquissone. Yanga mmejitahidi lakini mmeshindwa kufunga goli moja tu na kurudi na kombe Jangwani, Golikipa Djigui Diarra kafanya kazi yake sawa sawia ya kutoruhusu goli lakini viungo na washambuliaji sita mmeshindwa kufunga goli moja tu la ushindi. Yanga inahitaji mabadiliko.

Nikiishia hapa,
Mimi ni Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
 
Back
Top Bottom