Fainali ya Ligi kuu ya mbio za mabasi Tanzania (Sauli vs New Force/ Golden Deer) na lori la mafuta, serikali imejifunza nini?

Fainali ya Ligi kuu ya mbio za mabasi Tanzania (Sauli vs New Force/ Golden Deer) na lori la mafuta, serikali imejifunza nini?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Kùjifunza ni kitu kisicho na mwisho wala mipaka. Serikali yetu na watendaji wake hawajàona haja ya muda mrefu kujifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya fainali ya Ligi Kùu ya mbio za mabasi Tanzania kati ya New Force/ Golden Deer vs Sauli.

Maafa tumeanza kuyaona, leo mabasi yamegongana na Lori la mafuta, watu wamekufa, wengine kujeruhiwa. Lakini kesho makosa haya haya yatajirudia na watendaji wa serikali wenye wajibu wa kuwadhibiti wasafirishaji hawa wataendelea kushabikia fainali hiyo.

Polisi wa usalama barabarani na LATRA wanahusika kwa kiasi kikubwa kutokana na udhalimu huu unaoathiri maisha ya abiria wasio na hatia.
---
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw.Abubakar Kunenge, amezungumza na #ITVDigital ambapo amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya New Force, basi la Kampuni ya Sauli pamoja na Lori la mafuta, katika eneo la Ruvu, mkoani humo.

Kunenge amesema abiria walifanikiwa kutoka kwenye mabasi hayo isipokuwa abiria wawili ambao walikuwa wamebanwa kwenye moja ya mabasi hayo na wakati Jeshi la Zimamoto na Jeshi la Polisi wakiendelea na juhudi za kuwaokoa ndipo moto ukalipuka na kusababisha abiria hao kufariki dunia.

Soma:
- Kugongana kwa mabasi Sauli na New Force lilikuwa jambo la Muda tu
 
Kùjifunza ni kitu kisicho na mwisho wala mipaka. Serikali yetu na watendaji wake hawajàona haja ya muda mrefu kujifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya fainali ya Ligi Kùu ya mbio za mabasi Tanzania kati ya New Force/ Golden Deer vs Sauli...
Watu weusi bado tuko nyikani. hayo unayoyaeleza yako nje ya akili ya mtu mweusi.
 
Hao polisi uliowataja nao ni "wanazi" wa hayo mabasi,ndiyo maana huoni action yeyote ikichukuliwa.

Alafu Kuna wanazi wa katarama na nasi Gani Lile sijui. Kuna watu wanapenda hizi ligi sijui kwa nini.
 
20240328_203729.jpg
20240328_203746.jpg
20240328_203752.jpg
20240328_203734.jpg
 
Muda mchache kabla ya moto

Tank Ilikua imeharibika road ( Ruvu )

BM Coach alikua mbele akachomoa

Sauli Luxury Bus naye akaiga kachomoa pakawa padogo

New Force naye kachomoa too late akajaa nyuma ya Sauli.

Sauli kaparamia tank ubavuni wese likamwagika ndio moto ukashika
 
Kùjifunza ni kitu kisicho na mwisho wala mipaka. Serikali yetu na watendaji wake hawajàona haja ya muda mrefu kujifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya fainali ya Ligi Kùu ya mbio za mabasi Tanzania kati ya New Force/ Golden Deer vs Sauli...
Acha blaaa blaaaa Serikali ipige njia Nne Kibaha hadi Tunduma hizo ajali kichaa zitaisha zenyewe.
 
Back
Top Bottom