Fainali ya Ligi kuu ya mbio za mabasi Tanzania (Sauli vs New Force/ Golden Deer) na lori la mafuta, serikali imejifunza nini?

Ghafla nimeona taarifa now.kumbe katika Hilo sauli la Leo ndo analofanyia kazi rafiki yangu wa tangu shule..imagine mtu anapiga kazi na afya njema Kisha kesho inatangazwa kafa..ajali hizi

Hiyo ajali watu kibao wamekufa ila wanaficha
Kwanini tunafichwa? Si Latra wana Manifest? Itumike kutambua majeruhi na marehemu
 
Ninawezatu kusema hata abiria pia wanamatatizo maana hawapazi sauti.
Muda wote abiria wapo kwa gari hawatoi taarifa je polisi wanaotozatu faini na kuruhusu gari iondoke ndio wabebe lawama zote?
Ninawaombea majeruhi wapate nafuu haraka na marehem walale mahala pema na yatima wapate faraja
 
Kwanza niwape pole wale waliofiwa na ndgu na jamaa zao ktk ajali hyo,hao madereva wanabeti mtu akiwa wa kwanza uwa wanapewa hela pia kuna baadhi ya abiria wanapenda kuwai ndio wadau wakubwa wa mabasi hayo.sifa ndizo zinawagharimu watu maisha ukienda mfano zambia ni nadra kuona ajali hovyo hovyo ila ukiwa njiani unaona gari nyingi za kitanzania ndizo zinazopata ajali.
 
Duuu Pesa Adui wa Haki ,
 
Hilo bus la Sauli nililipanda mara ya mwisho ilikuwa ni 2020 December naelekea Mbeya kwenye msiba wa mzee wake na rafiki yangu, ilikuwa ile Benz DPC dereva dogo mmoja anaitwa Nabii Tito. Niseme tu ule mwendo na hizo overtaking jamaa alikuwa anafanya ilikuwa ni hatari sana niliapa sitakaa nipande tena hilo bus, na sikupanda ten mpka leo hii. Bora mzee Ngalo wa ABC ameingiza bus hiyo njia aokoe jahazi huko, hao New Force nao hata bure sipandi, kila leo ajali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…