Faini za Barabarani kwa Bodaboda sasa ni Tsh. 10,000

Faini za Barabarani kwa Bodaboda sasa ni Tsh. 10,000

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Kati ya mambo ya maana katika budget hii ni kupunguzwa kwa faini za barabarani.

Hii Tsh. 10,000 ndio tulikuwa tunawahonga askari wa barabarani, sasa naandaa Tsh. 2,000 wakigoma kupokea nawaambia tena kwa kiburi kikubwa kinachoambata na madoido nipatieni hicho kirisiti nitalipa mbele ya safari.

Haaaaa haaaaa mwendazake anaondoka na mambo mengi si mchezo.
 
Faini 10,000/ kwa bajaji na Boda Boda sio gari, nategemea kuona Boda Boda na bajaji wanafuata sheria.

Faini ya 30,000 ilikuwepo lakini haikuzingatiwa sana kwa vyombo hivyo.
 
Ni kwa pikipiki na bajaji.

Dha nawasikitikia sana hawa vijana , nahisi kutakuwa na ongezeko kubwa sana la ajali
 
Yaani ntawagonga kila siku!!kama walikuwa wananivimbia na faini ya 30,000 sasa hivi si ndiyo watataka kunipiga mateke kabisa?kesho naanza rasmi kuwagonga!! Wakijichanganya tu nawapanda,kumbe wanabebwa ndiyo maana wanakuwa na kiburi,wajinga sana hawa!!
 
Polisi lazima wakuundie zengwe. Utasikia una makosa 6 😂😂😂😂😁 ndio utatia akili. One door is closed, other r open.
 
Boda boda lini wanaandikiwa faini? Mimi naona wana utawala wao binafsi askari hawahangaiki nao kabis
Kuna askari mmoja pale Kibada alijitia kumsimamisha bodaboda, aliambulia mate ya uso. Ahahahaha hii nchi kwakweli ngumu sana, ilimbidi askari aende kichakani kunawa!

Bodaboda alifyatua speed hata ndege za SU 57 za Urus au F35 raptor isinge mpata ahahah
 
umenivunja mbavu mkuu
pole kwa askari
 
Bodaboda hadi akamatwe apigwe faini, amesimama tu anasubiria?! Wale jamaa wanakuaga kama panzi...
Labda Traffic officer atakuwa anatembea na chain. Akimkamata bodaboda anafunga bike kwenye mango tree, halafu anaanza kuandika kwenye efd machine. Tofauti na hapo kweli, ataambulia vumbiiiii
 
View attachment 1814605

Kati ya mambo ya maana katika budget hii ni kupunguzwa kwa faini za barabarani.

Hii 10,000 ndio tulikuwa tunawahonga askari wa barabarani,sasa naada 2,000 wakigoma kupokea nawaambia tena kwa kiburi kikubwa kinachoambata na madoido nipatieni hicho kirisiti nitalipa mbele ya safari.

Haaaaa haaaaa mwendazake anaondoka na mambo mengi si mchezo.
Hivi ni kwa boda boda tu...khaa mbona rahaa
 
View attachment 1814605

Kati ya mambo ya maana katika budget hii ni kupunguzwa kwa faini za barabarani.

Hii 10,000 ndio tulikuwa tunawahonga askari wa barabarani,sasa naada 2,000 wakigoma kupokea nawaambia tena kwa kiburi kikubwa kinachoambata na madoido nipatieni hicho kirisiti nitalipa mbele ya safari.

Haaaaa haaaaa mwendazake anaondoka na mambo mengi si mchezo.
Hiyo ni kwa Bodaboda na Bhajaji siyo magari mkuu.
 
Back
Top Bottom