Faini za Maegesho – Serikali Inakusanya Mapato kweli au Mfumo Unavuja?

Anana_

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2024
Posts
210
Reaction score
633
Jana nilipaki gari, nikavuka barabara kwenda kuchukua dawa pharmacy. Niliporudi, nilikutana na watu waliojitambulisha kuwa wanahusika na kukamata magari yaliyopaki vibaya.

Wakaingia ndani ya gari na kuniomba 150k hapo hapo au wanipeleke ofisini ambapo faini ilikuwa TZS 340,000. Nilikataa kulipa hapo hapo na nikakubali kwenda ofisini.

Nilipofika ofisini Temeke, ndipo nilipoona jambo lililonishangaza zaidi:

  • Watu walikuwa wakilipa TZS 120,000–150,000 cash na kuondoka.
  • Baadhi walikuwa wakilipa kwa sim bila kupewa control number.
  • Wakati huo huo, tuliambiwa control numbers hazitoki kwa sababu hakuna mtandao.
  • Hakukuwa na mfumo unaoonekana wa kuthibitisha kiasi halisi kilicholipwa na kueleza fedha hizo zinaingiaje kwenye mfumo wa serikali.

Swali langu ni hili: Kama faini rasmi ni TZS 340,000, kwa nini baadhi ya watu wanalipa TZS 120,000–150,000 mezani bila control number na wanaondoka?

Kama huu ni mfumo wa serikali wa kukusanya mapato, mfumo wa malipo na accountability uko wapi?

Serikali inaweza kuwa imeanzisha mradi mzuri wa kudhibiti maegesho, lakini kama mfumo wa ukusanyaji wa faini hauna control na uwazi, kuna hatari kubwa ya mapato ya serikali kupotea.

Naomba mamlaka husika zifuatilie mfumo huu wa malipo na utoaji wa faini za kupaki Temeke.
 
Wamejipatia mrija wa kufyonza, wanafyonza tu ata siwalaumu usipopiga wewe mwenzio atapiga.
 
Sheria ndogo ndogo za halimashauri husika, zimetaja kiwango gani kama faini ya hilo kosa?
Muda mwingine kama una muda wa kutosha, unapelekana nao mahakamani. Unawaachia garil lako, halafu unawageuzia kesi pia.
 
Safi sana
 
Rushwa kila mahali......na vile hakuna wa kukemea, ndo maana upigaji umetamalaki mno
 
Ilinitokea na Mimi jmosi moja. Jamaa wako sharp sana. Nilisimama ndani ya dk tu wameshazama ndani. Nikaenda nao mpaka keko kwenye yard yao.
Wanataka 250,000 cash ndio nitoke.
Nililock gari vizuri nikajifanya Niko bize kuwatafutia hiyo pesa. Kifupi sikuwa nayo.
Nilienda Moja kwa Moja kwa mlinzi getini nikamsomesha baadae nije kuitoa Ile gari akakubali.
Jioni nikarudi nikaitoa bila kwere nikamshikisha mlinzi 20k yake.
 
Back
Top Bottom