Ila dada kabla ya hizi mbwembwe zake nilikuwa simjui ila sasa wengi tumemjua, sasa ni wakati wake wa kufanya kitu kutokana na jina alilolipata ili atengeneze fedha
Hahaha,aisee hii kali,
Ni kweli wenzetu nje wanatafuta kiki huku wanapesa,ila sie tunafanya tukio ili likivuma ndio utengeneze pesa.
Watu wengi walikuwa hawamjui kabisaa,ila sasa wanamjua,ila sema tu Bongo ni tofauti na unavyoijua.
Usiombe nchi hii watu wakakuchoka na habari zako,yaani utajuta kuzaliwa,maana kwanza wanakupotezea kabisaa,na pili wewe mwenyewe status yako kwako na kizazi chako ni mbaya,na wazazi wako unawatia doa mbele ya jamii.
Kuna familia leo hii wazazi wao wakionekana kwenye jamii wanaonekana na wao hovyo tu.
Na hizi picha ni still,ambazo hadi mjukuu wake atazikuta,ni mbaya sana.
Amuulize wema Sepetu leo hii yupo wapi,si alikuwa kwenye kila gazeti,watu wamechoka sasa hivi wanona hakuna jipya.
Wamuulize Sinta wa Nature alivyopotea hadi leo.
We fanya vizuri tu ndio utajua kwamba Nchi hii fursa zipo,BIG UP saana dada yangu LADY JAYDEE,hili jembe ndio nalikubali saana katika madada wa Nchi hii wenye kujua nini wanafanya.Heshma yake na familia na kwenye jamii ipo pale pale na inazidi kukua.
Na ukiwa mtu mzuri basi hata akitokea mtu kukuharibia basi anapotea yeye.