Faiza Ally amwaga povu kisa Zari kupata deal Tanzania

Faiza Ally amwaga povu kisa Zari kupata deal Tanzania

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
BCDCC513-4EBD-4137-AEA3-5AD47B7EF1E0.jpeg

Msanii wa BongoMovie, Faiza Ally huenda akawa ni moja ya mastaa ambao wamekasirishwa na kitendo cha mwanamama Zari kupata dili la kutangaza nepi za watoto za Soft Care.

Faiza Ally amesema kuwa ameshangazwa na kampuni hiyo kumtumia Zari kutoka Uganda kwenye matangazo yao ile hali kuna Watanzania wengi na wenye majina ambao wangetumika kutangaza bidhaa zao.

I know this is gonna look bad for somepeople but let me be honest , how stupid Tanzanian can be , mastaa wote watanzania , watu wote watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya zari ?

Ina maana uhitaji bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje ?? Kwa nini tunawapa kipa umbele wageni tunajizarau sisi ???

Mlishawahi kuona Uganda na kenya wamempa nani dili wakamuacha wa kwao ?? Eti sasa hivi mganda na mkenya wanapongezan na sisi wote tunaonekana hatukufaaa,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, Faiza amemshangaa mwanamitindo Noel ambaye yeye ndiye aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanya connections hadi Zari kupata dili hilo.

Noel you know all the Tanzania star na uko karibu hukuona anae faa ? I don’t hate zari but I hate kuona vitu wanavyo stahili kupata watanzania kapata mganda this is no good !

Hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipa umbele zaidi ya mwenyeji , kiasi mpaka ukiwa unasuburi tax mpaka mwenye nchi apate na wewe ndio unafata,“ameeleza Faiza Ally.

Mtazamo wa Faiza umepigwa na baadhi ya Watanzania waliotoa maoni yao kwenye posti yake wakidai kuwa wanawake wengi wa Tanzania wanautumia umaarufu wao vibaya.

  • mimahrayvannyWabongo mpo serious na Instagram mganda yupo serious na kazi acha tu apewe
  • oddy_is_a_baeMarekani yenyew iliongozwa na mkenya sembuse Tz mwachen zari wa watu anastahili
  • rukkysaidWanaangalia vitu vingi dear,kwa mfano wewe ile post ya mchupi umechoka vile kweli wanaweza kukupa dili km hyo kirahis.
  • iam_g_mtonyohakuna mtu anayeweza kushawishi kuwa balozi @faizaally_ kwanza hatujui kujiwekea brand alafu tupo cheap sana unafikiri angeenda mbongo hicho kitu kisingejulikana yaana hakuna wa kutustua bongo, wenye makampuni wanatarget za mbali sio za hapo ulizofikiria wewe..! Zari ni brand tosha kama ulikuwa hujui, na anajimudu. SASA wewe kwa mfano ndo kampuni ni yako ungemuita nani aje kuwa barozi!
  • mwana_heriFaiza jamaniii kha eti “hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipaumbele zaidi ya wenyeji” iiii hamjuwi mambo ya nchi zilizoendelea HEAD OF THE BANK OF ENGLAND IS A CANADIAN CITIZEN (one of the top jobs available) because he was the best man for the job! First foreigner to run that institution in over 300 years but they had to make changes walisikia how successful alivyokuwa akiwa head of the Canadian bank. Sisi wa chini huku ndio usiseme! Mpaka unajiuliza kwa nini hawakumpa hii kazi mwenzao? Ma employer hapa wanaajiri sana watu wa eastern European sana wakiulizwa kwa nini hamuajiri watu wenu jibu ni moja “they are lazy and have no work ethic” mara leo mgonjwa, mara kesho kafiwa, mara anataka holiday! Muajiri ataweza? Lazima achukuwe mfanyakazi bora! Wewe unaonekana kama ni mpambanaji endelea tu kujitahidi please acha roho ya kwa nini mwenyeezi mungu hapendi, mshukuru tu kwa anachokupa akuongezee na juwa cha mwingine hakiwezi kuwa chako.
Jana Machi 28, 2018 Zari alisaini dili hilo nono la kutangaza bidhaa za Softcare Diapers ingawaje bado haijajulikana mkataba huo umemuingizia kiasi gani cha fedha.

Source: Bongo 5

Soma: VIDEO: ZARI aingia bongo kimya kimya kusaini Deal na Keds
 
Bwana wee hiyo hata mimi namuunga mkono Faiza, tatizo sisi wabongo tuna roho mbaya hatupendani mawivu yametujaa

Hapo unaweza kuona Noel ndo kahusika kumbe kuna msururu wa watu nyuma yeye anatumika tu, huwezi jua kuna wabaya wa mondi, wa hamisa, wa wema yaani watanzania tunachoweza ni majungu na kukomoana

Eti mnasema mastar watanzania hawajiheshimu huyo mganda anajiheshimu kwenye nini wakati na yeye ni wale wale tu.

Ama kweli nimeamini nabii hathaminiwi kwao huko kwao Uganda hana dili yoyote ya maana ila huku kwetu tunamuona malaika na hata aliyemfanya akajulikana kwa wengi sasa wanamtukana eti hana akili mwanamke ndo mwenye akili, angekuwa hana akili angemzalisha watoto wawili
 
Juzi diamond uzinduzi wa album yake umedhaminiwa na safari com ya kenya bado wakampa eneo lenye ukubwa wa nusu heka kenya.
Basi ingekuwa hivyo wasanii wakenya nao wangeandamana kwanini mgeni amependelewa wakati kenya kuna wasanii kibao
 
Wasanii wa bongo wengi hawana uelewa wa mambo ya biashara mkuu.
Hawa ni wa kuhurumia tu.
 
Bwana wee hiyo hata mimi namuunga mkono Faiza, tatizo sisi wabongo tuna roho mbaya hatupendani mawivu yametujaa

Hapo unaweza kuona Noel ndo kahusika kumbe kuna msururu wa watu nyuma yeye anatumika tu, huwezi jua kuna wabaya wa mondi, wa hamisa, wa wema yaani watanzania tunachoweza ni majungu na kukomoana

Eti mnasema mastar watanzania hawajiheshimu huyo mganda anajiheshimu kwenye nini wakati na yeye ni wale wale tu.

Ama kweli nimeamini nabii hathaminiwi kwao huko kwao Uganda hana dili yoyote ya maana ila huku kwetu tunamuona malaika na hata aliyemfanya akajulikana kwa wengi sasa wanamtukana eti hana akili mwanamke ndo mwenye akili, angekuwa hana akili angemzalisha watoto wawili

Sio roho mbaya. Soko ndio linalo amua. Wangemtumia Zari kama asingekuwa effective? Kwa upendo gani?
 
Dada amefanikiwa kuyabrand maisha yake
Amefanikiwa kujiweka high profile...

Binafsi naweza kumfananisha na baadhi ya wadada kama Jokate,nancy,Caroline,klyn na baadhi yao
Wameweza kujipa hadhi fulani hivi.
Wenzake wanamuonea wivu kwa hilo.
 
Back
Top Bottom