Faiza Ally: Sipo tayari kurudiana na ‘Sugu’ ila akihitaji mtoto mwingine nipo tayari ‘kumpatia’

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Muigizaji na mrembo Bongo, Faiza Ally amesema hayupo tayari kurudiana kimapenzi na baba watoto wake ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, ila yupo tayari kuzaa nae mtoto wa pili.

Akiongea kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm Jana, bidada huyo Mama wa mtoto mmoja aitwae Sasha amedai hamkumbuki Sugu kwa kuwa hakuwa ‘Romantic’ na alizo nazo kwake ni hisia tu za kupata mtoto wa pili na yeye.

“Sitaki kuzaa na kila Mwanaume, nieleweke wazi sitaki kurudiana na Sugu ila akinifata akidai anataka tuzae mtoto wa pili nipo tayari” Alisema.

Katika ‘line’ nyingine Mama Sasha alisema anajutia kitendo chake cha kutokutumia kinga alipojamiiana na Baba mtoto wake huyo kitendo ambacho kilisababisha kupata Ujauzito.
 
Mtu huna hisia naye halafu huyo huyo uko tayari kuzaa naye?! Hii lugha gongana, mwambieni anyooshe maelezo tu
 
sasa ni kwamba anampenda ama ni nini
 
ina maana akiwa na Sugu ili apate hisia atamuwaza ampendaye ila anachotaka ni mbegu za Sugu tu
 
Mi huyu dada nmemuelewa na ukiangalia vizuri anamantic kwa alichokiongea,kasema hataki watoto wake wawe na mababa tofauti tofauti something which is good kwa malezi ya watoto pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…