Falcao akiri kufanya mazungumzo na kiungo wa Peru, Renato kwamba matokeo ya sare yanawafaa.

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Straika wa Colombia Radamel Falcao amekiri kwamba alifanya mazungumzo na kiungo wa Peru, Renato Tapia kwamba matokeo ya sare baina ya mataifa hayo mawili yatawavusha wote kwenda kucheza Kombe la Dunia nchini Urusi.

Falcao alikosolewa baada ya kuonekana akiwaarifu wachezaji wa Peru kwamba hawana haja ya kujaribu kufunga goli la ushindi kwasababu 1-1 itawapa nafasi Colombia kwenda Urusi moja kwa moja na Peru kwenda kucheza mechi ya mtoano.

Hakuna magoli mengine yaliyofungwa, na hatimae Peru watacheza mechi ya mtoano dhidi ya New Zealand katika mechi mbili za nyumbani na Ugenini.

Baada ya mechi Falcao alisema," Tulikuwa tunajua nini kinaendelea katika mechi nyingine, tulikuwa tunacheza kwa kujua matokeo mengine na kwa muda ule nilijaribu kusambaza habari hizo kwa wachezaji wa Peru."

Tapia pia amekiri kwenye mahojiano na waandishi wa habari alifanya mazungumzo na Falco kuhusu matokeo ya mechi nyingine lakini amekanusha kwamba hakuna makubaliano ya kupanga matokeo ya mechi yao.

"Katika dakika tano za mwisho, wachezaji wa Colombia walitufuata . Walikuwa wanajua matokeo ya mechi zingine zilizokuwa zinaendelea" Tapia aliiambia Panamericana TV.

"Kwahiyo tuliamua kucheza mechi kama tulivyokuwa tunataka ..niliongea na Radamel akaniambia kwamba wote tumeshafuzu ( Kama mechi ikibaki kama ilivyo ) lakini huu ni mpira tunacheza ili kushinda."
 
falcao alihaha kuhamasisha ngoma ibaki droo, ila mbona amekiri mapema hivi
 
Kumbe chile anaweza pewa nafasi ya kufuzu maana fifa hawapendi upuuzi kama huu.

nawaza lakini.
 
Kumbe chile anaweza pewa nafasi ya kufuzu maana fifa hawapendi upuuzi kama huu.

nawaza lakini.

Taifa la colombia litamchukia sana endapo watatolewa kaongea jambo la ajabu sana kwa mtazamo wangu lakin mana wengine ukweli hawaupend
 
Duh!! Yaani sijui ni kukosa hekima na akili kichwani ngoja tuone kama wote wawili watabaki salama.
 
Ukweli utakuweka huru.Lakini hiyo haina tofauti nakupanga matokeo.
 
Nashukuru mkuu kumbe ushaliona japo misiwe muongo sikuangalia mechii hii ila baada ya matokeo kutokea sare kwa hawa na chile akitupwa nje nikaanza kufatilia hizi mechi nipate cha kusimulia ata wana kijiweni pindi tukipata kahawa .... Radamel Falcao Garcia: alitumia mdomo kupunguza kasi ya Peru na pressure ya mchezo golini kwa Colombia. Baada ya Peru kupata goli la kusawazisha dk 70 kupitia kwa Jose Paolo Guerrero, mkwaju wa free kick ambao ulikwenda moja kwa moja kwenye nyavu za David Ospina. Na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Kucheza nyumbani(home ground), nguvu ya mashabiki, pamoja na kusawazisha goli katika muda ambao ulikuwa unakimbia kweli kuelekea kumalizika kwa mchezo zikiwa zimebaki dakika 20 tu za mchezo huo kati ya Peru dhidi ya Colombia.

Baada ya goli la Jose Paolo Guerrero, Colombia walikuwa watumwa wa kila kitu, kabla ya mdomo wa Radamel Falcao Garcia kupunguza kasi ile ya Peru. Peru muda wote wa dk 20 baada ya kusawazisha goli wao walikuwa wameweka kambi golini kwa Colombia muda wote..... Muda wote huo Colombia walikuwa wanatumia ujanja wa kujiangusha ili kupoteza muda pamoja na kupunguza kasi na pressure ya Peru golini kwao.....

Kwa namna Colombia walivyokuwa wanajiangusha na kupata huduma ya kwanza ndipo captain wa Colombia Radamel Falcao Garcia alipopata habari kuwa Chile keshapokea goli tatu kwenye nyavu zake toka kwa Brazil, hivyo basi kama matokeo ya mchezo wao yataisha 1-1 kama yalivyokuwa basi Colombia atakuwa kafuzu na Peru atakwenda playoff dhidi ya New Zealand.

Mdomo wa falcao ukaanza kuwapa taarifa wachezaji wa timu zote mbili hususani wa Peru ambao akili yao ilikuwa inawaza ushindi zaidi katika mchezo huo...... Mdomo wa falcao ukafanikiwa kwa asilimia zote kutuliza mchezo. Dk 90 zikatimia na Mwamuzi wa mchezo akaongeza dk 3. Kuanzia hapo Peru walikuwa na mpira golini kwao wakipiga back pass 44 wenyewe kwa wenyewe Bila ya kufuatwa na mchezaji yeyote wa Colombia mpaka dk 3 zikamalizika mpira ukiwa kwenye eneo la Peru wakijipigia pasi wenyewe tu.... Baada ya kipenga cha mwisho mambo yakaenda kama yalivyopangwa.

Colombia wakiwa wanashangilia upande wao, Peru nao walikuwa wanashangilia upande wao..... Tunaanzia hapa kwenye mdomo wa Radamel Falcao Garcia kwanza ambapo Mimi, wewe na FIFA tunaweza sasa kuanza kuangalia kama ule mdomo wa Radamel Falcao Garcia hauhusiki na match fixing.
Ngoja tuwasubirie wenye sheria zao tuonee
 
Sidhani kama Colombia wataadhibiwa isipokua Falcao peke ake ndio atapewa rungu
 
Mimi hapo nashindwa kuelewa,inamaana Peru waliachana na kushambulia kwa nguvu japo walikuwa na uwezo Wa kupata goli ili wakacheze play off kwa kumsikiliza falcao? Ila kwa Hali ilivyo hyo ni scandal tayari,tusubiri maamuzi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…