radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,440
- 32,260
Straika wa Colombia Radamel Falcao amekiri kwamba alifanya mazungumzo na kiungo wa Peru, Renato Tapia kwamba matokeo ya sare baina ya mataifa hayo
mawili yatawavusha wote kwenda kucheza Kombe la Dunia nchini Urusi.
Falcao alikosolewa baada ya kuonekana akiwaarifu wachezaji wa Peru kwamba hawana haja ya kujaribu kufunga goli la ushindi kwasababu 1-1 itawapa nafasi Colombia kwenda Urusi moja kwa moja na Peru kwenda kucheza mechi ya mtoano.
Hakuna magoli mengine yaliyofungwa, na hatimae Peru watacheza mechi ya mtoano dhidi ya New Zealand katika mechi mbili za nyumbani na Ugenini.
Baada ya mechi Falcao alisema," Tulikuwa tunajua nini kinaendelea katika mechi nyingine, tulikuwa tunacheza kwa kujua matokeo mengine na kwa muda ule nilijaribu kusambaza habari hizo kwa wachezaji wa Peru."
Tapia pia amekiri kwenye mahojiano na waandishi wa habari alifanya mazungumzo na Falco kuhusu matokeo ya mechi nyingine lakini amekanusha kwamba hakuna makubaliano ya kupanga matokeo ya mechi yao.
"Katika dakika tano za mwisho, wachezaji wa Colombia walitufuata . Walikuwa wanajua matokeo ya mechi zingine zilizokuwa zinaendelea" Tapia aliiambia Panamericana TV.
"Kwahiyo tuliamua kucheza mechi kama tulivyokuwa tunataka ..niliongea na Radamel akaniambia kwamba wote tumeshafuzu ( Kama mechi ikibaki kama ilivyo ) lakini huu ni mpira tunacheza ili kushinda."