FALSAFA #1

FALSAFA #1

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
FALSAFA #1

: Anaandika
mwanafalsafa mmoja ya kwamba,
Katika hii dunia hakuna kitu kikubwa,kushinda mtu
Na ndani ya mwanaume hakuna kitu kikubwa
kinachoshinda FIKRA na UFAHAMU

NENO

Hapo mwanzo kulikua na Neno,naye Neno alikua kwa Mungu,
Na huyo neno alikua Mungu.
Pasipo yeye hakuna kilichofanyika,
Na kwa yeye vitu vyote vilipata kuwepo..
Nayeye Alipouvaa mwili tukapata kuuona utukufu wa Mungu.

HUYU NENO ni lugha ama kwa Tafsiri nyingine ni (WAZO)
Sasa twende pamoja.

Hapo mwanzo kulikua na WAZO,na hilo wazo lilikua ndani kwa Mungu,na hilo wazo ndio mungu mwenyewe,
Pasipo hilo wazo hakuna kilichofanyika,
Na kwa hilo wazo vitu vyote vilipata kufanyika.
Na hilo Wazo linapofanyika mwili watu wote huufurahia utukufu wa muumbaji....

:Nyumba unayoishi lilikua ni wazo lako kabla hujalivika mwili na watu wakaiona jinsi ilivyojengwa kwa ustadi na kukusifu.

:Gari ni wazo lililokua linatembea ndani ya fahamu za mtu...kisha akalivika mwili nasisi tukaliona gari nakuanza kuendesha na kufurahia utukufu wa muumbaji.

: Kila mtu ana Neno au wazo ambalo angetamani kulivika mwili,Ila nguvu inaweza kosekana ya kulitimiza wazo lake.
:Wazo lako ndio wewe,na wewe ndio wazo kamili la aliefanikisha ukavaa mwili.
Vitu vyote pasipo wazo hakuna kinachofanyika....
Heshimu sana ufahamu wako...
heshimu sana fikra zako
Hizo ndizo zinaumba...
Usiruhusu Ngono i destroy kiwanda cha uzalishaji ndani yako(Fikra)

Content created by : magical power
 
FALSAFA #2


: Kua muwazi na mwaminifu pale matatizo yanapokupata..

: Kua wa kawaida sana (Low profile) pale pesa inapokupata😎🥶

: Kua mnyenyekevu pale ambapo unapata madaraka na uongozi...!
Kwani kiburi hua kinatabia ya kukuchimbia shimo refu pasipo wewe,kutambua hivyo utashangaa ghafla umetumbukia.

: Na pia kua mtulivu pale ambapo hasira inapanda kutokana na makwazo....

Hii ndio ninayoita Falsafa#2
Usimamizi mzuri wa Fikra zako juu ya mazingira🤣

Katika FALSAFA #7
Ni heri niteseke ndani taratibu pekeangu,,,,huku nikiishughulisha Akili na Fikra katika kuumba suluhisho.
Kwa maana katika kuwaeleza watu shida na matatizo yangu..
Asilimia 70 Watafurahia na kucheka
Asilimia 25 watasema afadhali yamenikuta...
Asilimia 5 watajiangaisha kutatua
Sasa ni kwanini niusumbue utu wangu katika kujidhalilisha namna hii. Katika kundi kubwa la wasio maana.?

##4
Nilifikiria Nina shida na matatizo yangu kwamba ni makubwa kuliko ya wengine,lakini ilinibidi nicheke tu 🤣
Baada ya kumwona rafiki yangu ambaye alikua anahangaika kulipa madeni ambayo alikopa kwajili ya sherehe ya Harusi yake...
Na wakati huo tayari wameshatalikiana na Aliyekua mkewe.

#99
BINTI
Sikuizi wanaume nao wanawinda na kudate na kuoana na wanawake matajiri,utakufa single lady na style zako za kupika tu,Nenda katafute hela mama
Usisiburie mwanaume wa kuja kubeba na kutatua shida za huko kwenu
Utanisamehe ni utani🤣

#00

Mwaka huu hakuna wazo la biashara ambayo halikupita kwenye Akili yangu,,,
Duh pesa ngumu wakuu
Ndio maana sasa nafikiria mwakani ni bora nifungue kituo cha polisi tu tutajuana mbele kwa mbele

#####FALSAFA#6

Ninaamini Umbea na unafki unakufa pale unapofika kwenye sikio la mtu mwenye ufahamu na hekima....

Kwa maana umbea husambazwa na watu wenye chuki,
Na kuchukuliwa na kubebwa na wapumbavu....
Na kuaminiwa na wajinga

MWISHO

Content created by : magical power
 
Back
Top Bottom