False History(Historia Bandia)

False History(Historia Bandia)

D O A

Member
Joined
May 26, 2020
Posts
5
Reaction score
2
leo akati napita pita mtandaoni nikaona hii kitu.

Inasemekana kwamba kuna watu waliongeza miaka ili wawepo kwenye histori ya dunia. Mfano
Julian calendar na Georgian calendar
[Julia caesur alitunga calendar ili ajiweke kwenye historia]

Afu anasema Ano Domino[A.D] ni harakati za watu kama kina Pope Silvester II na roman empire ili wawepo kwenye raman ya dunia.
(Anaeleza Helbert Iige)

Bwana Iige anaelezea watu wengi zaidi, mimi nimegusia wahusika wachache tu.

najiuliza hivi ii kitu ni kweli,kwa anaeelewa zaidi anaweza kufafanua
 
Sijakuelewa.
Mfano ceasur aritunga kalenda yake ili aweke sikukuu zake..
Afu pia inasemekana AD ni mipango ya watu.wanasema iliongezwa miaka 1000.ili Carbondating ionekane kwel
 
Kalenda zilianzishwa na mamlaka za wakati huo ambao Ni watawala wa Rumi ya kale kama Julias Ceaser na mapapa wa katoliki kulingana na kuhama kwa nguvu kati ya wafalme na kanisa.Miezi ilikuwa inaongezeka kulingana na matakwa ya mamlaka na majina ya miezi yaliamriwa na mamlaka mfano mwezi wa Saba unaitwa July kwa sababu ya Julias Ceaser na August ni Augustus.Hapo kabla mwaka ulikuwa na miezi Saba tu.Julian calendar sababu ya Julias Ceaser na Gregorian Calendar ni Pope Gregory.
 
Kila wakipigana vita mataifa ya Ulaya
Mshindi anaandika historia ya kumkweza na kuwaponda wenzie..

Historia yote ya Ulaya imejaa uwongo..

Ndo maana ottoman empire ilivyo shindwa
Historia Yao ya walivyotawala Ulaya na dunia imefichwa fichwa na kupotezwa..

Hata ujerumani history Yao inapotezwa..

Waingereza wamejikweza.mno wakati kalikuwa Ka Taifa kadogo wakati wanaume wanapigana kutawala dunia..

Watu hawajui hata Uingereza ishatawaliwa na ufaransa na mataifa mengine
 
Mfano ceasur aritunga kalenda yake ili aweke sikukuu zake..
Afu pia inasemekana AD ni mipango ya watu.wanasema iliongezwa miaka 1000.ili Carbondating ionekane kwel
KWANINI HARIHAMUHA KUTUNGA KARENDA, WAKATI KIRA SIKU, NA KIRA WAKATI TUNAPATA MISIMU MINNE YA MWAKA, vuri, masika kihangazi na kipupwe?
Hayo matumizi batiri ya H NA R ni kwasababu maharumu, reho nimekura chakura Cha Kikurya, kichuri, ugari wa mtama na tunyama twa kuchoma.
 
Kabla ya kutunga kalenda yake ni kalenda ipi ilikuwa inatumika?
Mfano ceasur aritunga kalenda yake ili aweke sikukuu zake..
Afu pia inasemekana AD ni mipango ya watu.wanasema iliongezwa miaka 1000.ili Carbondating ionekane kwel
 
Kalenda ya kwanza kutumika na sehemu kubwa ya dunia ilikuwa ipi?
Ilikuwa na mapungufu gani?
Ukiweza kuyajibu haya maswali mengine uliyouliza ni rahisi sana.
leo akati napita pita mtandaoni nikaona hii kitu.

Inasemekana kwamba kuna watu waliongeza miaka ili wawepo kwenye histori ya dunia. Mfano
Julian calendar na Georgian calendar
[Julia caesur alitunga calendar ili ajiweke kwenye historia]

Afu anasema Ano Domino[A.D] ni harakati za watu kama kina Pope Silvester II na roman empire ili wawepo kwenye raman ya dunia.
(Anaeleza Helbert Iige)

Bwana Iige anaelezea watu wengi zaidi, mimi nimegusia wahusika wachache tu.

najiuliza hivi ii kitu ni kweli,kwa anaeelewa zaidi anaweza kufafanua
 
Kalenda zilianzishwa na mamlaka za wakati huo ambao Ni watawala wa Rumi ya kale kama Julias Ceaser na mapapa wa katoliki kulingana na kuhama kwa nguvu kati ya wafalme na kanisa.Miezi ilikuwa inaongezeka kulingana na matakwa ya mamlaka na majina ya miezi yaliamriwa na mamlaka mfano mwezi wa Saba unaitwa July kwa sababu ya Julias Ceaser na August ni Augustus.Hapo kabla mwaka ulikuwa na miezi Saba tu.Julian calendar sababu ya Julias Ceaser na Gregorian Calendar ni Pope Gregory.
Hapana hakuna miezi iliyoongezwa kufuatana an matakwa ya serikalli. Naeleza sasa hivi.
 
leo akati napita pita mtandaoni nikaona hii kitu.

Inasemekana kwamba kuna watu waliongeza miaka ili wawepo kwenye histori ya dunia. Mfano
Julian calendar na Georgian calendar
[Julia caesur alitunga calendar ili ajiweke kwenye historia]

Afu anasema Ano Domino[A.D] ni harakati za watu kama kina Pope Silvester II na roman empire ili wawepo kwenye raman ya dunia.
(Anaeleza Helbert Iige)

Bwana Iige anaelezea watu wengi zaidi, mimi nimegusia wahusika wachache tu.

najiuliza hivi ii kitu ni kweli,kwa anaeelewa zaidi anaweza kufafanua
Usiogope, hakuna historia bandia. Lakini kulikuwa changamoto ya kutunga kalenda iliyo sahihi. Hasa kalenda inayolingana na majira.
Kalenda rahisi ni kalenda ya Mwezi jinsi wanavyotumia Waislamu kwa sikukuu zao. Unatazama mwezi mpya tu, tayari unajua kipindi kipya kimeanza.

Lakini kalenda ya mwezi halilingani na majira. Majira yetu hufuata Jua katika mwaka wa siku 365 hadi 366. Vipindi 12 vya Mwezi mpya ni siku 354 pekee. Hivyo Ramadhani mara iko masika, mara iko vuli. Katika nchi ambazo ni mbali na ikweta tofauti ni kubwa zaidi na muhimu kwa kulima. Maana pale wanaangalia sana sikusare (siku 2 za usawa wa mchana na usiku, 21 Machi na 21 Septemba; maana Ulaya ya Kati siku ndefu kwenye Juni ni mwanga kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa 4 usiku, lakini Desemba ni giza kuanzia saa 11 alasiri hadi saa 2 asubuhi). Mazao na mimea hufuata mwanga, si mwezi.

Kwa sababu hiyo watu walianza kutunga kalenda ya Jua. Kuna mwaka unaodumu hadi jua limefika sehemu hiyohiyo angani tena, ambao ni siku 365.2425 , yaani karibu 365 na robo.

Unaona kwamba siku na mwaka havilangani kikamilifu. Hapa unahitaji kusawazisha tofauti hii kwa namna fulani, lakini ilichukua karne kadhaa hadi watu wameelewa yote.

Julius Ceasar alikuwa mtawala wa Roma aliyekuwa na kalenda ya mwezi na hii ilileta matatizo ya utawala maana unataka kodi wa wakulima wakati wa mavuno lakini mavuno hayafuati kalenda ya mwezi. Aliona kalenda ya Jua itakuwa nafuu. Alitumia wataalamu wa Misri (mmoja Sosthenes) waliomkadiria hesabu. Mwaka wa kalenda yake ilikuwa na siku 365 na robo. Yaani kila mwaka ilikuwa na siku 365 na mwaka wa nne ilikuwa na siku ya nyongeza (=29 Februari) ili kuingiza hizo robo siku mara nne.
Lakini Kalenda ya Juliasi ilikuwa na kasoro ambayo haikujulikana mwanzoni. Muda kamili wa mwaka wa jua si siku 365 ¼, ni chini yake kidogo. Tofauti ilikuwa dakika 11 na sekunde 14. Hadi karne ya 14 BK tofauti hiyo ilikuwa imefikia tayari jumla ya siku 7. Hayo yalionekana hasa wakati wa Pasaka ambayo haikufuata tena utaratibu wa kuwa kipindi baada ya sikusare ya machipuo.

Hapa Papa Gregori katika karne ya 16 aliita kamati ya kurekebisha kalenda. Utaratibu wake tunafuata hadi leo:
* kila mwaka wa nne utakuwa na siku 366 badala ya 365 kwa kuongeza tarehe 29 Februari. Mifano: 2020, 2024, 2028
* kila mwaka ambao namba yake inagawiwa kwa 100 utakuwa na siku 365. Mifano: 2100, 2200, 2300 (ingawa inagawiwa kwa nne)
* kila mwaka ambao namba yake inagawiwa kwa 400 utakuwa tena na siku 366, si 365. Mifano: 1600, 2000, 2400, 2800, 3200 (ingawa inagawiwa kwa 100)

Wakati wa kuanzisha kalenda iliyosahihishwa, walipaswa kuruka mbele tarehe 10. Kwa hiyo hesabu ya kalenda iliruka wakati ule kutoka Alhamisi 4 Oktoba 1582 kwenda Ijumaa 15 Oktoba 1582. Nchi kadhaa ziliendelea kutumia kalenda ya zamani, mfano Urusi hadi 1918.

Jisomee hapa:
Kalenda ya Gregori - Wikipedia, kamusi elezo huru
Kalenda ya Juliasi - Wikipedia, kamusi elezo huru
Kalenda ya mwezi - Wikipedia, kamusi elezo huru
Kalenda ya jua - Wikipedia, kamusi elezo huru
Kalenda - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
KWANINI HARIHAMUHA KUTUNGA KARENDA, WAKATI KIRA SIKU, NA KIRA WAKATI TUNAPATA MISIMU MINNE YA MWAKA, vuri, masika kihangazi na kipupwe?
Hayo matumizi batiri ya H NA R ni kwasababu maharumu, reho nimekura chakura Cha Kikurya, kichuri, ugari wa mtama na tunyama twa kuchoma.

Wee Fara jifunze kuandika vizuri. HARIHAMUHA ndo nini?? Kihangazi ndo nini??

Pumbavu
 
Kalenda zilianzishwa na mamlaka za wakati huo ambao Ni watawala wa Rumi ya kale kama Julias Ceaser na mapapa wa katoliki kulingana na kuhama kwa nguvu kati ya wafalme na kanisa.Miezi ilikuwa inaongezeka kulingana na matakwa ya mamlaka na majina ya miezi yaliamriwa na mamlaka mfano mwezi wa Saba unaitwa July kwa sababu ya Julias Ceaser na August ni Augustus.Hapo kabla mwaka ulikuwa na miezi Saba tu.Julian calendar sababu ya Julias Ceaser na Gregorian Calendar ni Pope Gregory.
Hapo kwenye mwaka kuwa na miezi saba hata mimi naona kuna mashiko.
unakuta wanasema katika biblia mtu aliishi miaka 963 serious? kumbe mwaka ilikua ni siku 30 enzi hizo unakuta!
 
Hata ile ya Methusela miaka 900+ inawezekana ikawa humohumo na biblia inasema miaka elfu moja duniani Ni sawa na siku moja mbinguni
 
Back
Top Bottom