Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Chama cha Mapinduzi (CCM), miongoni mwa vyama vikongwe zaidi barani Afrika, kinaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Tayari kimethibitisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan atapeperusha bendera kuwania nafasi ya urais, huku kikitangaza orodha ya wagombea wa Ubunge, Udiwani na Baraza la Wawakilishi.
Miongoni mwa wagombea hao, wapo wanaotoka kwenye familia za viongozi wakuu wa CCM, akiwemo rais wa sasa na marais wastaafu.
1. Rais mstaafu Kikwete
Katika Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi, CCM itawakilishwa na Salma Kikwete, ambaye yupo katika nafasi ya Ubunge tangu mwaka 2017. Ikumbukwe Salma ndiye aliyekuwa Mgombea pekee aliyechukua fomu katika Jimbo la Mchinga.
Katika familia ya Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kuna mwanasiasa mwingine, ambaye atagombea katika Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, naye alikuwa mgombea pekee kuchukua fomu.
2. Rais Samia
Mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan, Wanu Hafidh Ameir alipitishwa na CCM kama mtia nia wa Ubunge jimbo la Makunduchi, Zanzibar, na hatua iliyofuata ni kuchuana na wenzake katika kura za maoni.
Baada ya kura za maoni, Wanu alipata ushindi kwa kura 1356, akiwabwaga wapinzani wake, huku mpinzani wake wa pili akiambulia kura 3 pekee. Hatimaye CCM imepitisha jina lake kugombea ubunge jimbo hilo.
3. Hayati Rais Mwinyi
Familia ya Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi na mtoto wake ambaye ni Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi, imejikita katika siasa za Tanzania kuanzia nafasi ya urais hadi katika Bunge la Tanzania.
Hussein Mwinyi atagombea urais Zanzibar. Huku Asma Ali Hassan Mwinyi aliibuka mshindi katika kura za maoni za CCM kwa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Welezo Zanzibar. Chama chake kimempitisha kugombea Ubunge jimbo hilo.
4. Hayati Rais Magufuli
Chama Cha Mapinduzi(CCM) kilimteua Mtoto wa Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli, Jessica Magufuli na wagombea wengine 30 kugombea Ubunge Viti Maalum kupitia kundi la UVCCM.
Jesca alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 361, akitanguliwa na Ng'wasi Kamani aliyepata kura 409, nafasi ya tatu ikichukuliwa na Halima Bulembo aliyepata kura 320.
CCM imemteua Jesca kuwa Mgombea Ubunge viti maalum Vijana (UVCCM).
5. Dkt. Emmanuel Nchimbi
Aliyekua Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, John John Nchimbi aliongoza kura za maoni Jimbo la Nyasa baada ya kupata kura 9,157 kati ya kura 10,695 zilizopigwa. Jana CCM imemteua kupeperusha bendera katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo hilo.
Huyu ni ndugu na Emmanuel John Nchimbi. Mpaka mwishoni mwa wiki alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, kabla ya Jumamosi kutangazwa Asha-Rose Migiro kushika nafasi hiyo. Emmanuel Nchimbi ndiye mgombea mwenza katika nafasi ya Makamu wa Rais katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025 kupitia chama hicho.
Lakini kwenye mchakato wa mwaka huu wa CCM, pia wapo familia za vigogo walioachwa. Januari Makamba, mtoto wa Katibu wa zamani wa CCM, na mwanachama mwandamizi wa siku nyingi wa CCM, Mzee Yusuph Makamba jina lake halikurudi kabisa hata kupigiwa kura.
Kada wa CCM Kambarage Wasira kutoka familia ya Makamu mwenyekiti wa CCM, Stephen Wassira, aliomba kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge Bunda Mjini naye alikatwa.
Chanzo BBC Swahili