Familia Bora hujenga Taifa bora
FAMILIA BORA, TAIFA BORA
Ningependa tuelimishane namna familia zinavyoweza kujenga taifa bora au kuaribu taifa. Kwanza kabisa ningependa kueleza maana ya familia na aina zake.
Familia ni muunganiko wa baba, mama na watoto au kikundi cha watu wanaoishi pamoja lakini kikiwajumuisha baba, mama, watoto na hata ndugu wengine au watu wengine.
Kwa ufupi kabisa ningependa ufahamu baadhi ya aina za familia ambazo ni;
Familia ya nyuklia au familia ya wazazi wawili-hii inajulikana kama familia ya kawaida katika jamii inayoundwa na mama, baba na watoto.
Familia ya mzazi mmoja ambayo kati ya baba au mama mmoja wao ndiye anayeishi na watoto na kulea familia.
Familia iliyo panuliwa, familia moja ya baba, mama na watoto wanaishi pia na ndugu wengine kama babu, bibi, mjomba, binamun.k.
Familia ya kuasili-hii ni familia ambayo wazazi wawili huchukua mtoto wa wazazi wengine na kumlea na kumpatia stahiki zote kama mtoto wao.
Baada ya kuelewa maana ya familia na aina zake, tukumbushane kwa uchache wajibu wa wazazi kwa watoto; wazazi wanawajibika kuwapatia watoto wao malezi bora yatakayo wawezesha kuwa watu wema katika jamii. Malezi yanahusu yale yote anayofanyiwa mtoto tangu akiwa tumboni mwa mama mpaka kufikia umri wa
kujitegemea.
Nikufahamishe kwamba familia ni muhimu sana katika ustawi wa taifa lolote lile duniani ndio maana serikali pamoja na bunge hawajaacha wazi bali walitunga sheria zinazoangazia masuala yote ya familia na ndoa vilevile zingatia kwamba hata wazazi wanapotaka kutarakiana mahakama uingilia kati kuangalia mustakabali wao na mustakabali na maslahi ya watoto ambao ni taifa la kesho. Kwa kuzingatia umuhimu wa ndoa, familia na watoto kwa taifa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na sheria ya mtoto ya mwaka 2009 zilitungwa.
NAMNA FAMILIA INAVYOJENGA TAIFA BORA NA IMARA
Unaweza ukawa unajiuliza namna familia inavyojenga taifa bora. Fuatilia Makala hii utafahamu namna familia inavyojenga taifa bora na lenye mafanikio katika Nyanja zote kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
Nianze kwa kujiuliza maswali tofauti tofauti; mimi na wewe tumetoka wapi? Je nafasi niliyonayo au nafasi uliyonayo bila malezi sahihi ningeipata au ungeipata? Je cheo ulichonacho ungekipata bila malezi bora? Je wadhifa ulionao ungeupata bila familia yako? Majibu ni mepesi tu kuwa mimi na wewe tumetoka katika familia zilizotulea na kutuandaa kuwa hivi tulivyo sasa, nanafasi uliyopo usingeweza kuifikia na kuipata bila malezi sahihi ya familia au cheo na wadhifa ulionao kazini usingeweza kuvipata bila ya malezi na maelekezo sahihi ya familia.
Tuendelee kujiuliza, Rais wa nchi katoka wapi? Jibu ni jepesi sana, katoka kwenye familia bora iliyomlea vizuri na hatimaye amekuwa rais. Tujiulize pia viongozi maarufu duniani kama Barack Obama wametoka wapi, wafanyabiashara na matajiri wakubwa duniani kama Elon Musk wametoka wapi, wanasayansi wakubwa duniani kama Albert Einstein wametoka wapi? Jibu bado ni jepesi tu wametoka kwenye familia zilizowajibika
kuwalea kwa maadili na kuwakuza katika misingi thabiti ya kijifunza. Kwahiyo familia bora ndiyo mzizi na shina la mti uzaao matunda. Hivyo, familia zina wajibika kuwalea watoto katika misingi bora kwaajili ya ustawi wao na ustawi wa taifa kiujumla.
Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ibara ya 8(1); inasema kwamba wananchi ndio msingi wamamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi. Hii inaonyesha kwamba watu ndio msingi wa madaraka yote kwenye taifa kwa maana hiyo tukiwa na familia bora tutakuwa na watu bora, tukiwa na watu bora tutakuwa na serikali bora na taifa bora.
Wahenga walisema “samaki mkunje angali mbichi”. Kwa muktadha wa andiko hili niseme kwamba ili tuwe na taifa bora tunapaswa kuwa na watu bora. Leo hii tunalia na tatizo la rushwa nchini tumetunga sheria za kupambana na kuzuia rushwa lakini tujiulize hawa wala rushwa wametoka wapi? jibu ni kwamba wametoka kwenye familia zetu. Hivyo, tuanze kupambana na rushwa kuanzia kwenye malezi majumbani na mashuleni
ili tuweze kuwa na taifa la watu wenye maadili na uzalendo kwani rushwa ni adui wa haki na maendeleo.
Pia tuna tatizo la ajira, dhana ya kujiajiri inagonga mwamba na mfumo wetu wa elimu bado ni uleule pia familia zetu zilitulea kwa kutuhimiza tusome ili tuajiriwe. Tofauti na kubadilisha mfumo wa elimu ili kukabiliana na changamoto hii, vilevile wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto kuhusu mabadiliko ya nyakati na kuwasaidia kuvumbua na kuendeleza vipaji vyao ili waje wajiajiri kupitia vipaji vyao.
NAMNA FAMILIA INAVYOWEZA KUHARIBU TAIFA
Namna familia inavvoweza kujenga taifa bora ndivyo hivyo inavyoweza kubomoa na kuharibu taifa na kusababisha kuwa na taifa lisilona dira. Unaweza ukawa unajiuliza namna gani familia inaweza kuaribu taifa. Jibu ni jepesi tu.
Tanzania na mataifa mengine hususani ya Afrika yanakumbana na matatizo ya rushwa, ufisadi, uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, uhalifu wizi, n.k. Zingatia kwamba matatizo haya yanatendwa na watu. Na watu hawa wanatenda makosa hayo kwasababu tu wamekosa maadili. Leo tuna mahakama ya mafisadi nchini lakini haiwezi kuwa suluhisho la mafisadi bali suluhisho kamili linaanzia katika malezi bora ngazi ya familia, makanisani na misikitini vile vile elimu ya maadili na uzalendo mashuleni.
Nitoe mfano halisi juu ya kikundi cha uhalifu cha watoto maarufu kama panya road; kikundi hiki kimefanya uhalifu mbaya sana mitaani. Polisi wamekuwa wakiwakamata na kuwapeleka mahakamani. Japo sio suluhisho la kudumu. Lakini tujiulize nini chanzo na suluhisho la panya road. Ukiangalia ni watoto wadogo hivyo chanzo ni wazazi na jamii kutowajibika ipasavyo katika malezi na suluhisho ni wazazi na jamii nzima kuwajibika
katika malezi bora.
Tunaweza kuwa na taifa bora lisilo na rushwa, ufisadi, wizi, utapeli, ujambazi, ubakaji, ukahaba, ujangili, mauaji, n.k kama tu wazazi watawajibika ipasavyo katika malezi bora ya watoto.
HITIMISHO
Naitimisha kwa kusema ‘TAIFA BORA NI ZAO LA FAMILIA BORA’. Hatuwezi kuwa na taifa bora bila kuwa na watu bora na watu bora hutoka katika familia bora. Wazazi na walezi mnapotamani kuona watoto wenu wamefanikiwa tambueni kuwa mafanikio ya watoto kwanza utengenezwa na wazazi kupitia malezi. Hivyo mnapaswa kuwalea watoto katika misingi imara ya maadili, dini pia ziendelee kufundisha na kusisitiza juu ya maadili na matendo mema; mashuleni walimu kufundisha na kusisitiza juu ya maadili na uzalendo. Serikali pia mbali na kutunga sheria inapaswa kuendelea kutoa elimu juu ya malezi bora, maadili na uzalendo kwa taifa

Upvote
1