Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kwa wale waliosoma Civics watakumbuka aina mojawapo ya familia ya "extended family" ambayo kwa kiswahili kisicho rasmi ni aina ya familia pana inayokusanya watu wengi zaidi ya wazazi na watoto wao. Hii ni familia inayohusisha watu wengine wengi wasio watoto wa mwenye familia.
Vijana wengi wanaopata ajira au biashara ndogo wanaotoka kwenye extended families ambazo kwa Tanzania ndio aina kubwa ya familia na nyingi zake ni maskini huishia kuhudumia mahitaji ya wanafamilia hizo na kufanya maisha yao yote ya hapa duniani kuwa ya mkononi kwa mdomoni "hand to mouth" bila maendeleo yoyote ya maana.
Nchi nyingi zilizoendelea aina ya familia ni "nucleus family", mtu anahudumia watoto wake wa kuwazaa tu, hakuna habari za mtoto wa mjomba, mpwa, shangazi, mtoto wa baba mkubwa, mdogo n.k. Hata hao watoto wa kuwazaa wenyewe wanapofikisha miaka 21 huwa wanasukumwa kwenda kujitegemea na kutafuta maisha yao binafsi kwa kufanya kazi mbalimbali. Hali hii inapunguza sana utegemezi kwa watu binafsi na kuwafanya hata kipato kidogo wanachopata kuweza kukiwekeza kwenye vitegema uchumi mbalimbali hususani kupitia masoko ya hisa.
Nchini kwetu kijana mdogo tu aliyeingia kwenye ajira ngazi ya chini kabisa kwa mara ya kwanza au umachinga anahudumia familia ya hadi watu 15! Kuna kuendelea kweli katika hali hiyo au ni kuendeleza mduara wa umaskini usioisha?! Lazima tubadilke kama tunataka kuumaliza umaskini.