Familia Tajiri ya kihindi yenye ukwasi wa Trilioni 100+ yahukumiwa Jela kwa kuwanyanyasa wafanyakazi wa ndani na kuwalipa malipo kiduchu

bikira latifah

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2016
Posts
667
Reaction score
1,850
Jana na Leo kuna Habari ilisambaa kwenye Mitandao now imewekwa BBC kuhusu Tajiri namba moja UK mwenye asili ya INDIA Ajay Hinduja kufungwa miaka Minne jela yeye mkewe na watoto wake kwa kosa la kutumikisha Wahindi wenzao kutoka India kwa kazi za Ndani kwa mshahara mdogo sana

Screenshot 2024-06-22 170625.png

Wamefungwa huko Geneva Uswiss walipokuwa wanaishi, Unaambiwa waliwachukua mabinti kutoka India wakawasafirisha hadi Uswiss kisha wakawa wanawatumikisha kazi kwa saa 18 kwa siku huku wakiwa wamepokonywa pasi za kusafiria na hakuna ruhusa ya kutoka nje huku walilipwa pesa ndogo

Hiki kisa kimenikumbusha enzi hizo najitafuta niliwahi kuajiriwa sehem tena kampuni kubwa tu na kazi ilikuwa ni kumsaidia chief C, Mpishi mkuu wa Boss mkubwa tu Tajiri la kihindi hapa Bongo kwa mkataba wa sh 180,000 kwa mwezi ilikuwa mwaka 2015 hiyo, Chief yeye Ali kuwa analipwa 250,000 kazi ya kumpikia Bilionea hiyo jamani Wahindi shkamooni

unapokuwa Tajiri mkubwa hakikisha wasaidizi wako wa Ndani na wanaokupikia uwape pesa nzuri la sivyo wa naweza hata kushawishika kukuwekea sumu wakapotea, Bilionea una mzigo wa Trilioni alafu anaekupikia unamlipa mshahara mbuzi hamuogopi kufa?
 
Familia ya Hinduja ni raia wa uingereza wenye asili ya kihindi inayothaminiwa kuwa na utajiri wa takribani dola bilioni 47 (shilingi trilioni 123)

Screenshot 2024-06-22 170625.png

L to R: Prakash. P. Hinduja, Chairman, Hinduja Group (Europe); Srichand. P. Hinduja, Chairman, Hinduja Group; Gopichand.P. Hinduja, Co-Chairman, Hinduja Group; Ashok. P. Hinduja, Chairman, Hinduja Group (India)

Watu wanne wa familia ya bilionea Hinduja wamepatikana na hatia ya kuwanyonya wafanyikazi wa nyumbani katika jumba la kifahari huko Geneva nchini Uswisi.

Inadaiwa kuwa wafamilia Prakash Hinduja na Kamal Hinduja, pamoja na mtoto wao wa kiume Ajay na mkewe Namrata walikuwa wanawaleta wafanyakazi za ndani kutoka India na kuwaleta wawafanyie kazi za nyumbani.

Katika moja ya jumba lao la kifahari wanalomiliki nchini uswisi, imebainika wafanyakazi walikuwa wanapitia manyanyaso haya:

  • Kuwanyanganya pasi za kusafiria
  • kuwaminya uhuru wa kutoka nje ya nyumba
  • kuwatumikisha masaa 16 hadi 18 kwa siku
  • Kuwalipa malipo kiduchu wafanyakazi kwa kuwaingizia hela kwenye account zilizopo nchini India, Malipo yakiwa ni rupia elfu 10 kwa mwezi sawa na shilingi laki 3, toauti na utaratibu wa nchi nyingi za ulaya wa kuwalipa wafanyakazi za ndani kwa saa (per hour) na nchini switzerland kima cha chini cha mshahara kwa kazi yoyote ni CHF24. 32 (shilingi elf 71 kwa saa)

mmoja wa waendesha mashtaka maarufu wa Geneva, Yves Bertossa, alilinganisha karibu kiasi cha dola 10,000 (shilingi milioni 26) kwa mwaka alizodai familia ilikuwa ikitumia kwa ajili ya mbwa wao na malipo kiduchu ya watumishi wao.

Mahakama ya Uswisi imewahukumu Prakash na Kamal kifungo cha miaka minne na miezi sita gerezani. Ajay na Namrata miaka minne, Pia waliamriwa kulipa takriban $950,000 (shilingi bilioni 2.4) kama fidia.
 
Tanzania beki tatu hukipwa
40,000, kazi masaa 19, matusi ya kuja umekonda Leo umenenepa, kulazwa sebuleni na kuitwa majina ya ajabu kama beki tatu, Binti, dada, nk bila kusahau kuliwa na faza hausi na vijana wake.

Msako ukiputa bongo wote mnaishia segerea, keko na butimba.
 
Familia ya Hinduja ni raia wa uingereza wenye asili ya kihindi inayothaminiwa kuwa na utajiri wa takribani dola bilioni 47 (shilingi trilioni 123)

View attachment 3023133
L to R: Prakash. P. Hinduja, Chairman, Hinduja Group (Europe); Srichand. P. Hinduja, Chairman, Hinduja Group; Gopichand.P. Hinduja, Co-Chairman, Hinduja Group; Ashok. P. Hinduja, Chairman, Hinduja Group (India)

Watu wanne wa familia ya bilionea Hinduja wamepatikana na hatia ya kuwanyonya wafanyikazi wa nyumbani katika jumba la kifahari huko Geneva nchini Uswisi.

Inadaiwa kuwa wafamilia Prakash Hinduja na Kamal Hinduja, pamoja na mtoto wao wa kiume Ajay na mkewe Namrata walikuwa wanawaleta wafanyakazi za ndani kutoka India na kuwaleta wawafanyie kazi za nyumbani.

Katika moja ya jumba lao la kifahari wanalomiliki nchini uswisi, imebainika wafanyakazi walikuwa wanapitia manyanyaso haya:

  • Kuwanyanganya pasi za kusafiria
  • kuwaminya uhuru wa kutoka nje ya nyumba
  • kuwatumikisha masaa 16 hadi 18 kwa siku
  • Kuwalipa malipo kiduchu wafanyakazi kwa kuwaingizia hela kwenye account zilizopo nchini India, Malipo yakiwa ni rupia elfu 10 kwa mwezi sawa na shilingi laki 3, toauti na utaratibu wa nchi nyingi za ulaya wa kuwalipa wafanyakazi za ndani kwa saa (per hour) na nchini switzerland kima cha chini cha mshahara kwa kazi yoyote ni CHF24. 32 (shilingi elf 71 kwa saa)

mmoja wa waendesha mashtaka maarufu wa Geneva, Yves Bertossa, alilinganisha karibu kiasi cha dola 10,000 (shilingi milioni 26) kwa mwaka alizodai familia ilikuwa ikitumia kwa ajili ya mbwa wao na malipo kiduchu ya watumishi wao.

Mahakama ya Uswisi imewahukumu Prakash na Kamal kifungo cha miaka minne na miezi sita gerezani. Ajay na Namrata miaka minne, Pia waliamriwa kulipa takriban $950,000 (shilingi bilioni 2.4) kama fidia.

Kwa hiyo ndiyo wanaenda kunyea ndoo humu ndani?
Wapeni pole sana.
IMG_2105.jpeg

IMG_2106.jpeg

IMG_2107.jpeg
 
Niliwah kufany kazi ya pastrier hoteli flani hiv bosi muhindi. Unaambiwa akikuona kwemye kamera unaonja fruits mara zaidi ya tatu unakatwa mshahara. Hata vyakula vilivyobakia kutoka kwenye buffet hutakiwi kuvimalizia.. bora umwage au ukalie cold room. Akikubamba mkuu umekwisha
😄😄Cold room wanazingua sana me waliniajiri ndani ya siku 6 nikafukuzwa.
 
Back
Top Bottom