MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Ziara ya mwana mfalme wa Uingereza William imezaa matunda baada ya mazungumzo aliyoyafanya kwa muda mchache na waziri wa michezo na utamuduni mh Harrison Mwakyembe. Katika mkutano mdogo uliofanyika pembeni,wawili hao walikubaliana na ombi la familia ya kifalme lililowasilishwa na William la kuwapatia walimu 5 kila mwaka ambao watakuwa na kazi maalum ya kuifundisha familia hiyo lugha hadhimu na tamu ya Kiswahili.
Waziri Mwakyembe amesema anafanya mazungumzo na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kupata wanafunzi waliofanya vizuri mwaka huu ili waende mara moja na kuanza kazi Uingereza, sambamba na hilo pia kutakuwa na ubadilishanaji wa wanafunzi kwa miezi 6 kati ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na wale wa familia ya kifalme watakaokuwa wwanasoma chuo cha mtakatifu Andrew Uingereza,ambacho kinaposomesha watu wengi wa familia hiyo.
Waziri alisema haitakuwa kitu cha ajabu miaka 5 baadae kukuta kiswahili kikizungumzwa katika korido la jumba la kifalme la Buckingham au hata mfalme ajaye kuongea Kiswahili kizuri kabisa.
Wanufaika wa programu hii mbali na kupata ajira bali pia watapata mishahara kwa viwango vya Uingereza ambacho kima cha chini ni zaidi ya mil 3.
Kila la heri vijana wa kitanzania huko Uingereza, sisi huku Kenya tunaenda Somalia kupambana na ugaidi