Familia ya kifalme Uingereza kupatiwa walimu 5 wa kiswahili kila mwaka kutoka Dar

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Ziara ya mwana mfalme wa Uingereza William imezaa matunda baada ya mazungumzo aliyoyafanya kwa muda mchache na waziri wa michezo na utamuduni mh Harrison Mwakyembe. Katika mkutano mdogo uliofanyika pembeni,wawili hao walikubaliana na ombi la familia ya kifalme lililowasilishwa na William la kuwapatia walimu 5 kila mwaka ambao watakuwa na kazi maalum ya kuifundisha familia hiyo lugha hadhimu na tamu ya Kiswahili.
Waziri Mwakyembe amesema anafanya mazungumzo na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kupata wanafunzi waliofanya vizuri mwaka huu ili waende mara moja na kuanza kazi Uingereza, sambamba na hilo pia kutakuwa na ubadilishanaji wa wanafunzi kwa miezi 6 kati ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na wale wa familia ya kifalme watakaokuwa wwanasoma chuo cha mtakatifu Andrew Uingereza,ambacho kinaposomesha watu wengi wa familia hiyo.
Waziri alisema haitakuwa kitu cha ajabu miaka 5 baadae kukuta kiswahili kikizungumzwa katika korido la jumba la kifalme la Buckingham au hata mfalme ajaye kuongea Kiswahili kizuri kabisa.
Wanufaika wa programu hii mbali na kupata ajira bali pia watapata mishahara kwa viwango vya Uingereza ambacho kima cha chini ni zaidi ya mil 3.
Kila la heri vijana wa kitanzania huko Uingereza, sisi huku Kenya tunaenda Somalia kupambana na ugaidi
 
I had a dream only to be woken up by the smell of coffee
 
Ili ukiite Kiswahili kuwa FURSA ni lazima ufahamu na lugha nyingine (hasa ile inayomshindaga mkuu). So vijana wa BA Kiswahili acheni kuota ndoto mbaya huko vijiweni muwaachie Wakenya fursa yao.
 
Mmh ntakuwa wa mwisho kuamini haya

Yaani hii ni fursa pia?
Waalimu watano labda wangepelekwa bunge la UK kujifunza
 
Waingereza "wanahaha". Brexit imewachanganya sana. Viongozi wao wengi hawakuitegemea na hawakujiandaa.
 
Hizi chai za huyu bwana inabidi nizifanyie research kabla ya ku digest
Siku hizi kila kona upo kwaajili ya kukebehi na kutoa matusi kwenye nchi yetu tukufu ya Tanzania. Unadhani utaweza au unajipa stress tu ambazo hazina sababu.
Nimekuona kwenye mtandao wa Kenya Talk, ukirusha maneno ya kebehi na kujikomba kwa wakenya. Huenda mwenzetu upo na chembechembe za nchi adui wa Tanzania.

Haiwezekani kila kitu kurusha matukano na maneno ya kebehi kwa watu waliokuzidi umri. Ninauhakika karma itakufuata kokote.
 
Mkuu mpe vidonge huyo msaliti au labda ni nyang'ao!
 
🙏🏾
 
Kwanini kuna English ya UK, America, Nigeria n.k

ila linapokuja suala la kiswahili tusiseme kuna Kiswahili cha Kenya na cha Tanzania??
 
Mbona ninasifia ujenzi wa Chato International Airport hata na Chato Stadium au huoni
 
Kwanini Chuo kikuku cha Dar es Salaam tu?

Wanaosoma vyuo vingine hii fursa itawapitia kushoto?
 
Mboga ninadifia ujenzi wa Chato International Airport hata na Chato Stadium au huoni
Nimemalizana na wewe. Kwani Chato hawataki maendeleo!? Are you stupid or something!? Mbona huongelee uwanja wa ndege Songwe!? Mbona huongelei flyovers za Dar es salaam!? Mbona huongelei barabara zinazojengwa Arusha!?
Tabia za kueneza chuki hazikusaidii chochote. Unapandikiza mbegu za chuki ili watu wa Geita wachukiwe!?

Huo ni wehu na roho za kichawi. Wewe unaona ni vitu simple tu unafanya. Labda uwe unatumikia adui wa nchi yetu.
 
Ili ukiite Kiswahili kuwa FURSA ni lazima ufahamu na lugha nyingine (hasa ile inayomshindaga mkuu). So vijana wa BA Kiswahili acheni kuota ndoto mbaya huko vijiweni muwaachie Wakenya fursa yao.
Bora fursa imeangukia tz, wakenya kama umefanya kautafiti hakuna lugha wanayo ijua vuzuri (english+swahili) zote pumba. labda wakafundishe kijaluo au kikuyu
 
Hahahahhhhh.duuuh .viva magufuli.ila hiz ziara zao,kun vitu in return wanavipata.naskia malkia,anamilki hifadhi nying tu hapa bongo.ndo maan kin prince William ,kifua mbele kulinda maslah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…