Familia ya Ndikumana yasema iko tayari kumsaidia mtoto kufikia malengo yake

Familia ya Ndikumana yasema iko tayari kumsaidia mtoto kufikia malengo yake

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Dogo.jpg

Familia ya marehemu Ndikumana ambaye alikuwa mume wa muigizaji wa filamu Tanzania, Irene Uwoya, imesema iko tayari kumsaidia mtoto wao aliyeachwa na marehemu Hamadi Ndikumana, Krish Ndikumana, ili kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa mcheza soka maarufu

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, mdogo wa marehemehu Hamadi Ndukaman, Laddy Ndikumana, amesema wao kama familia wako tayari kuhakikisha ndoto hiyo inatimia, kwani kipaji cha soka kipo kwa familia yao nzima.

"Tutajaribu kumsaidia kwa sababu kama familia nzima ni wanasoka, na hiyo ni kipaji ambacho yuko nacho tayari, tutamsaidia kufikia malengo yake", alisikika Laddy Ndikumana akimwambia Big Chawa.

Marehemu Ndikumana ameacha watoto wawili akiwezo Krish ambaye amezaa na muigizaji Irene Uwoya, na aliwahi kusikika akisema nataka kuwa mcheza soka maarufu kama baba yake.
 
Back
Top Bottom