Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Magufuli alikuwa mtu wa kuendeshwa na hisia sana kuna uwezekano hilo jambo likawa lina ukweli ndani yake.
 
Magufuli alikuwa mtu wa kuendeshwa na hisia sana kuna uwezekano hilo jambo likawa lina ukweli ndani yake.
Rejea ya Qur'an:

Allah anasema katika Qur'an:

"Enyi mlioamini! Ikiwa fasiki anakuleteeni habari, ichunguzeni kwa makini, msije mkawaumiza watu bila kujua, na mkawa wenye kujuta kwa mlilotenda."
(Surat Al-Hujurat: 6)



Aya hii inasisitiza kwamba, kabla ya kuchukua hatua yoyote kwa msingi wa habari zilizopokelewa, inapaswa kufanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha ukweli wake.

Hadithi ya Mtume Muhammad (S.A.W):

Mtume Muhammad (S.A.W) alisema:

"Kuwa na tahadhari na uvumi, kwani uvumi ni maneno ya uongo."
(Bukhari na Muslim)



Mtume alisisitiza umuhimu wa kuwa na tahadhari na habari ambazo hazijathibitishwa, kwani zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

Mfano wa Tukio:

Katika kipindi cha Mtume, taarifa zililetwa kwake kuhusu baadhi ya watu wa kabila fulani waliodaiwa kusaliti ahadi zao. Mtume hakuchukua hatua ya haraka, bali alituma wajumbe wake kuchunguza ukweli wa madai hayo. Uchunguzi huo ulizuia maamuzi ya haraka ambayo yangeweza kusababisha madhara kwa watu wasio na hatia.

Funzo kwa Jamii:

1. Kujiepusha na haraka: Hakuna maamuzi yanayopaswa kufanywa bila uchunguzi wa kina.


2. Kusikiliza pande zote: Usikivu wa haki unahakikisha kila mtu anapewa nafasi ya kueleza upande wake.


3. Kudumisha amani: Uchunguzi wa habari huondoa fitina na uvumi ambao unaweza kusababisha mtafaruku katika jamii.
 
Story za Muhammad zinachanganya sana! Mpaka anaagiza uchunguzi alikuwa kiongozi wa kijamii au kidini? Na kama alikuwa kiongozi mbona jina lake si kati ya historia ya majina ya viongozi wa Maka/Madina?
 
Akili nyingine hizi hivi kitabu mpaka kitoke hakina ukaguzi? Jibu rahisi ni mpango madhubuti uliondaliwa kuwatoa watu kwenye uhalisia uliopo na kuwarudisha kwenye uhalisia wa kufikirika ,

kwa jicho la kawaida tu huo ni mpango uliopitishwa na waliopo ila waliopo nao wakati utaisha nao.
 
Tatizo la watu kama Kabendera huwezijua kama anaohuo ushahidi au Laa!

Familia inaweza kutamani kufanya ulichoshauri lakini ikiwa itabainika ni kweli. Nini kitatokea?

Hakuna ambaye yupo tayari kumvua Marehemu Baba au Mume nguo tena Akiwa kaburini
 
Eeghh kweli kabisa
 
Story za Muhammad zinachanganya sana! Mpaka anaagiza uchunguzi alikuwa kiongozi wa kijamii au kidini? Na kama alikuwa kiongozi mbona jina lake si kati ya historia ya majina ya viongozi wa Maka/Madina?
Profesa Michael H. Hart: Mwanafizikia na mwanaastronomia Mmarekani, aliyeandika kitabu "The 100: A Ranking of the Most Influential Persons in History". Katika kitabu hiki, alimweka Mtume Muhammad katika nafasi ya kwanza, akimuelezea kama mtu mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika historia ya binadamu kutokana na mafanikio yake katika nyanja za kidini na kisiasa.
 
Magufuli hakuwa rais muadilifu, hilo hata ukae uchi hapa jf huwezi kulibadili. Na Magufuli aliweza kuagiza unyama wa kila namna wafanyiwe wakosoaji, na hakuna uwezo wa vyombo vyetu kuweka ukweli huo wazi. Kama unataka ukweli wa Kabendera ufahamike, lije shirika la kijasusi la nje litaweka wazi hadi mahali alitupwa baada ya kuuwawa.
 
Mtume alikuwa kiongozi wa nchi gani?
 
If u keep silence , people have less question and many answers. Zingefanyika investigation za kina na kutoa majibu ya mauaji yote haya yasingekuwepo ,it like killers after assassination they dissapear in thin air.
 
Hii pia ilisemwa, na mimi nikaisikia kwamba jamaa alimpiga risasi kwa mkono wake, ni Kabendera tu ndio kaamua kuiweka katika kumbukumbu.
Kwahiyo ikisemwa kwamba wewe ni jamii ya LGBTQI nami nikaiweka kwenye kumbukumbu ya maandishi inakuwa kweli!?
 
Eric Kabendera sio mtanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…