Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

Familia ya Rais Magufuli mkiliachia hili jambo lipite bila ya kumburuza mahakamani Kabendera itakuwa ni usaliti wa karne!

I’m all for it. Ila Kabendera naye ni lazima atoe ushahidi na awataje waliomwambia.
Ili iweje? Mwenzako ameandika kwa reference nyingi sana. Wewe unapiga mayowe tu. Unaweza andika kitabu chako pia kwa upande unaona unafaa
 
Sijui hili wazo limetoka wapi, lakini kisheria marehemu hawezi kuwa DEFAMED kwasababu hana reputation ya kuilinda. Libel and Slander suits zinafanya kazi Inter-vivos (between living persons) tu.

Familia ya Raisi Magufuli wataweza kupata Locus Standi (Legal Ground) ya kumshitaki Bwana Eric Kabendera pale ambapo watathibitisha kwamba hiki kitabu kimechafua heshima waliyo nayo mbele ya jamii au kuwasababishia hasara fulani ya kiuchumi, ila haya mengini ni mapendekezo na hisia kali tu.

IKUMBUKWE: kwenye Libel na Slander Suits, The Burden of Proof inashift na kwenda kwa anayeshitaki. Hivyo familia ya marehemu Raisi Magufuli lazima iwe tayari kuthibitisha mbele ya mahakama kwamba haya yaliyoandikwa na Bwana Eric Kabendera ni uzushi ambao unalenga kuchafua taswira ya familia pamoja na kuwasababishia hasara ya kiuchumi.
Rafiki yako Chige yupo wapi siku hizi??..
 
Magufuli alikuwa kichaa na mlevi wa madaraka aliyependa kusifiwa sana. Hizi tuhuma sio mpya na kwa mtu anayemjua vizuri huyo shetani wa Chato, hilo tukio alilifanya na mengine mengi kama hilo
kwa akili zako hz kwan civil warswar zisiwepo Africa , kuchuja habari kwako mtihani , na hamjiiww athari ya hz porojo zenu?
 
Magufuli alikuwa mtu wa kuendeshwa na hisia sana kuna uwezekano hilo jambo likawa lina ukweli ndani yake.
alifikaj ikulu bila watu kujua ? mbona ya samia yamevuja kwann ya Jpmkati hayakuvuha kipind akiwa hai
 
Ubaya ni deni litakalolipwa, mwisho wa ubaya ni aibu. Wakati Ben anapotezwa Magufuli alikuwa na uwezo wa kuamuru uchunguzi huru kujua nini kilimpata Ben lakini licha ya kelele nyingi hakufanya hivyo. Sasa unapopush familiya yake imtetee kwani wanajua matendo yote aliyofanya Magufuli alipokuwa hai? au vipi familiya yake ika disclose ukatili wa Magufuli utakaokuwa wa kutisha kuliko tuhuma za kumuua Ben Saanane kwa mikono yake mwenyewe. Kwenye utawala wa Magufuli kulikuwa na mambo mengi ya kutisha huenda hata alichosema Kabendera likawa moja wapo.
umeandika vzr ila utawala wa Sa100 umekuwa na mauaji ya kutisha kuliko awamu zote huko awali , ss hv kila taasisi inavimba sabab mama yupo nao , polis wanataka na kuua wajisikiavyo hakuna wa kuwahoji
 
umeandika vzr ila utawala wa Sa100 umekuwa na mauaji ya kutisha kuliko awamu zote huko awali , ss hv kila taasisi inavimba sabab mama yupo nao , polis wanataka na kuua wajisikiavyo hakuna wa kuwahoji
Sure, Bi mkubwa ni silent killer siyo mropokaji kama Baba J. Tena kuelekea uchaguzi watu wawe makini sababu atakula vichwa vya kutosha iwapo atagombea. Lakini kila mtu atalipwa kadiri atendavyo, auaye kwa upanga naye atakufa kwa upanga.
 
Huelewi mambo wewe. Kwanini unafikiri hili jambo ni la familia ya Magufuli? Na kwanini unafikiri Magufuli hawezi kuuwa mtu?! Ulikuwa unamjua Jiwe vizuri kweli?
Katika madai yote dhidi ya Rais Magufuli, hili dai la huyu mwandishi Eric Kabdendera, kuwa Rais Magufuli alimuua Ben Saanane kwa kumpiga risasi ya kichwa hapo Ikulu [nasadiki ni Ikulu ya Dar], ni dai kubwa na zito sana.

Ni kashfa kubwa sana. Kwa mtu tu wa kawaida, kutuhumiwa kuua mtu mwenzio si jambo dogo. Seuze Rais wa nchi?

Wengi wetu kwa sasa tutakuwa tumeshaiona hii excerpt ya hicho kitabu:
View attachment 3190381

Napata wakati mgumu sana kuamini kuwa Rais Magufuli anaweza kumuua kijana wa Kitanzania, ambaye ni mtu mdogo sana, in the grand scheme of things, kwa mikono yake mwenyewe tena kwenye nyumba ya wananchi, Ikulu.

Tumeshawazoea akina Lissu na wenzake kuropoka na kutoa tuhuma za ajabu ajabu bila kutoa wala kuonyesha ushahidi wowote ule zaidi ya kusema ‘nimeambiwa’ au ‘niliambiwa’.

Lissu keshawahi kusema mara kadhaa kuwa baada ya Magufuli kufariki, eti nyumbani kwake yalikutwa mabulungutu ya mahela, dola za Kimarekani, kwenye mamilioni.

Bila ushahidi wowote ule zaidi ya ‘kuambiwa’, tuhuma hizo zinabaki kuwa ni porojo tu za Lissu.

Na ndo maana pengine hata familia ya Rais Magufuli haijawahi kusema wala kufanya chochote dhidi ya madai hayo.

Ila hili la Magufuli kutuhumiwa kuwa ni cold-blooded murderer, si la kawaida na halipaswi kupuuziwa.

If not true, what Kabendera did is libelous and should sued.

Mimi si mtaalamu wa sheria za Tanzania. Lakini naamini sheria za libel zipo.

Licha ya kwamba Rais Magufuli alikuwa ni public figure, kuna vitu huwezi kuvisema dhidi yake bila ushahidi.

Tuhuma za mauaji kwa mtu yeyote yule, humtia doa kubwa sana kwenye jamii, mtu huyo.

Majuzi hapa tumeona kituo cha televisheni cha Marekani, ABC, kilikubali kumlipa Rais Trump $15 milioni kwa sababu mmoja wa watangazaji wake alisema kimakosa kuwa Trump alipatikana na hatia ya ubakaji wakati si kweli.

Kubaka ni moja ya makosa yanayompa mtu doa la maisha.

Uuaji, kwangu mimi, ni kosa lililo juu ya ubakaji.

Sasa huyu jamaa Kabendera anakuja na tuhuma nzito namna hiyo tena kwa Rais mzima bila hata ushahidi wowote ule zaidi ya kusema kaambiwa na vyanzo vyake.

Hapana kwa kweli. Tuhuma kama hizo ni nzito sana kuachwa hivi hivi tu, la sivyo kama ni za ukweli.

Familia ya Rais Magufuli ikimwacha huyu jamaa bila kumburuza mahakani akatoe testimony yake huko under the penalty of perjury, itakuwa ni usaliti mkubwa sana kuwahi tokea nchini.

Yaani kabisa Rais Magufuli ampige risasi ya/za kichwa huyo Ben Saanane hapo Ikulu, halafu watu wa Magufuli waichukue maiti yake na kwenda kuitupa kwenye moto Rufiji?

Vigumu sana kuamini hilo.

Familia ya Rais Magufuli ni lazima ichore mstari mchangani na kuchukua hatua.

La sivyo, mtatufanya watu kama mimi tuamini kuwa yanayosemwa ni ya kweli.
 
Back
Top Bottom