Familia za mateka lipeni ujira ndugu zenu wawe huru

Familia za mateka lipeni ujira ndugu zenu wawe huru

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Binadamu ana thamani zaidi ya fedha, kumnyima uhuru binadamu nikuzamisha ndoto zake nakumkoseha Uhuru wakufanya yale aliyopangwa kufanya hapa Duniani.

Mateka Duniani siku zote wamekuwa wakithaminishwa na fedha au Mali, kwamba unatekwa unafichwa then ndugu zako wanaitwa watoe kiasi flani cha fedha ndipo uachiwe.

Ukiwa mateka hakuna mahakama itakayoweza kusikiliza shauri lako, utachukuliwa kila baada ya siku kadhaa nakupelekwa kwa wakubwa kisha kurudi kwenye mateka au eneo lakizuizi. Upo uwezekano mateka wasiachiwe huru hata kama ndugu zao watataka kutoa ujira.

Kwa thamani ya uhai, kwa thamani ya utu ni bora na ni Bora Sara pale nduguyo anapowekwa mateka ukafanya liwezekanalo hata kwa kuuuza mali zake kisha ukawapa watekaji waweze kumwachia huru. Litabaki doa la kwamba aliwahi wekwa mateka lakini bora doa la kusarenda na kumpa ushindi mtekaji kuliko kumsubiria mtekaji akusikilize umweleze kwamba wewe huna hatia.

Mtekaji ana mambo mengi na watu wengi wanaomlilia kwa mengi, anakula na kunywa na familia yake hivyo hawezi kukutukiria, jipe muda umalizane naye maisha yaendelee.

Kama umetekwa kwenye elimu lipa ada upate elimu, kama umetekwa kwenye kodi lipa Kodi upate Uhuru wakufanya biashara, Kama umepakaziwa lipa gharama za kupakaziwa uwe huru. Kumbuka hakuna aliyetayari kukusikiliza kwa wakati nakukutendea haki. Waliopewa jukumu lakukusikiliza wameyapenda mashangingi kuliko utu, wanajali mshahara, wanajali familia zao na wanajali ndugu zao, walipe uwe huru.
 
Back
Top Bottom