Familia zaamua Bobbi Kristina afe siku aliyokufa mama yake Whitney Houston (11/Feb)

Familia zaamua Bobbi Kristina afe siku aliyokufa mama yake Whitney Houston (11/Feb)

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
mom n daughter.jpg
Bobbi Kristina akiwa na mama yake mzazi,
Whitney Houston enzi za uhai wake.


FAMILIA za Bobby Brown na marehemu Whitney Houston zimekubaliana kumwondolea Bobbi Kristina mashine inayomsaidia kupumua kesho, Jumatano ili afe tarehe sawa na ile ambayo mama yake mzazi, Whitney Houston alifariki.

bobbikristinabrown.jpg

Bobbi Kristina Brown

Mjukuu wa Bobbi, Cissy Houston alitoa wazo hilo la Februari 11 wakati wa majadiliano yaliyofanyika wikiendi iliyopita kati ya familia ya Whitney Houston na Bobby Brown kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory huko Atlanta nchini Marekani.

attachment.php

Bobbi Kristina Brown akiwa na mpenzi wake Nick Gordon

Brown alitoa baraka zake kuruhusu binti yake huyo aondolewe mashine ya kupumua wakati wa usiku ili afe tarehe moja ya Februari 11 sawa na mama yake aliyefariki Februari 11, 2012 katika Hoteli ya Beverly Hilton.

Maamuzi hayo yamefikiwa ili kuweka kumbukumbu ya mama na binti yake ili wote wapumzike kwa amani, familia ya Brown ilieleza.

Bobbi Kristina, 21, binti pekee wa Houston na mwimbaji Bobby Brown, amepoteza fahamu tangu alipokutwa bafuni hakiwa hajitambui Januari 31, mwaka huu.

Chanzo: GPL
 

Attachments

  • bobbinampenziwake.jpg
    bobbinampenziwake.jpg
    30.3 KB · Views: 3,659
Oh dear God!Inauma sana kiukweli!
 
dah jamani inauma sana watoto wetu hawa duh!
 
Ina maana anaishi kwa msaada wa mashine ya kupumulia si wamuache tu anaweza kupona jamanii huyu nae ni madawa ndio yamemfanya hivyo jamaniii
 
Hizi ndio Last Posts ya Bobbi kristina alizozitoa 'bout a week ago(week ago).
Bobby Krist Week Ago.jpg

Bobby Krist Week Ago1.jpg
 
Hii nimeipenda sana,kwamba vichwa ngumu wajifunze ubaya wa madawa ya kulevya.
 
Ina maana anaishi kwa msaada wa mashine ya kupumulia si wamuache tu anaweza kupona jamanii huyu nae ni madawa ndio yamemfanya hivyo jamaniii

Ingekua bongo muda mrefu tushazika tushasahau. Kumbe wenzetu hadi siku ya kufa wanajipangia
 
Kumbe binti nae alikuwa anapata unga? Jamani inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom