..family conflict vs future of our children..

..family conflict vs future of our children..

kama una uwezo wa kumsaidia fanya hivyo tafadhali., tusiwe watu wa kulaumu kwa mambo ambayo yashatokea na hatuwezi kuyarudisha nyuma. Najua wenye shida kama hiyo ni wengi ila unapopata opportunity ya kumsaidia japo huyo mmoja itumie na mungu atakubariki sana.

Kama ni mkristu utakua umetimiza kwaresma yako vizuuri..
 
msaidie ukiweza. . Asomee hata cherehani ajiondoe kwenye ubaamedi
 
mmh, hapa kazi ipo.

Mie huwa najiambia, si kila mtu ana uwezo wa kuwa mzazi.
Ukijitafakari ukaona huwezi kuwa mzazi usizae.

Watu wanakataa watoto, wanatelekeza familia. Vurugu tupu!

Most of us are mare females and males.....not mother or fathers....
Hawana tofauti na jogoo....
 
kama una uwezo wa kumsaidia fanya hivyo tafadhali., tusiwe watu wa kulaumu kwa mambo ambayo yashatokea na hatuwezi kuyarudisha nyuma. Najua wenye shida kama hiyo ni wengi ila unapopata opportunity ya kumsaidia japo huyo mmoja itumie na mungu atakubariki sana.
Well said Husny.
 
Inauma sana aisee kuwaona watoto wanateseka kwa ujinga uliofanywa na wazazi/mzazi wao lakini yakishakumwagika hayazoleki. Muhimu kama alivosema husninyo hawa watu hawakutaka wakuwe hivo, mtu kama una msaada tafuta mmoja au wawili na saidia kadiri ya uwezo wako. Mtoto sio lazima umzae, hata ukimlea pia atakuwa mwanao.
 
sasa ndugu yangu ww huwez kumsaidia kidogo? kama uwezo unasoma msaidie tu
 
Its painful sana ila na wewe ndugu baada ya kusikia that story ulifanya nini ktk kumsaidia huyo binti?Au ndo uliomba appointment nae .....................!
 
Ladies and gentlemen, habari za asubuhi!
Jana wakati naianza w'end yangu, nilikua napata 'the lager' maeneo flan. Bar maid aliyekua ananihudumia ni bint wa miaka 17. Nikawa interested nae nikamkaribisha, tukapiga stori mbili tatu hivi. Nikamuuliza kwa nini ameamua kufanya kazi hiyo(barmaid) akiwa bado teenager?
Akanijibu ni kufarakana kwa familia.
"Bro, nimemaliza form 4 mwaka jana, nimesoma kwa shida, baba aligoma kunilipia ada, ananiambia mfate mama ako, mama anaishi na bwana mwingine na hana uwezo".. Mwisho wa kunukuu!
Ikabidi nimtafute meneja wa bar kupata ukweli coz watu hawakawi kujitungia stori. Meneja akaniambia ni kweli..
Nilihuzunikia 'maua' machanga yanaanza kunyauka kwa kukosa kumwagiliwa maji wakati maji yapo.
Nilipomuuliza matokeo, aliniambia ana D tatu..
Ama kweli what goes around comes around! Wanajamvi hali hii mpaka lini? Kwa nini dhambi hii ya wanandoa kugombana inawapata hata hawa wasio na hatia? It real pains kila kukicha street children, wanaojiuza, madanguro n.k yanaongezeka for the same reason. What genenation are we going to have in some near future? Tubadilike wajemeni.. Hayo ndio yangu kwa leo
...
Asubuhi njema!

SI aksante sana kwa mada nzuri sana. Mimi ni victim wa mahusiano yaliyovunjika hata kabla hayajakomaa kufikia kwenye ndoa. Nililelewa na Baba yangu mlezi ambaye kusema ukweli ninajisikia vibaya sana kila nikifikiria kuwa yeye ni mlezi (Ingawa mwenyewe nimempasisha YEYE ndiye BABA yangu). Ni wababa wachache sana ambao wana moyo kama wa huyu BABA yangu..alinichukua nikiwa na umri wa miaka mitano, akanilea kama mwanaye, akanisomesha kama mwanaye na kunibatiza jina la FIRST BORN wake pamoja na kuwa first born wake ni mwanaume!.

Kutokana na ukweli kwamba mafarakano ndani ya ndoa hayaepukiki, nadhani ni vema wazazi tukajifunza kuwaweka wenenu katikati ya magomvi yetu, yaani kila tunapogombana tuwafikirie wenetu. Lakini inaposhindikana basi tujifunze kuwa responsible........Baba wajibu wako kwa wanao hata kama umekorofishana na mkeo bado uko pale pale, haya ya nenda kwa mamako, sijui nini hayana tija. Mbona wakifanikiwa kutoka huko mbeleni mnnajitokeza na kutangaza ubaba ambao hamkuupractice??

Mimi mpaka leo simjui babangu mzazi ila ninayo hamu sana ya kumjua, nimtizame tu usoni nilione tabasamu lake au kama ndo alishafariki bari nilione tu kaburi lake, nimweleze ye moyoni mwangu.
 
MwanaJ,pole kwa hilo na hongera kwa kutokuwa na kinyongo na baba yako usiemjua.Muombe mungu kila siku kwa kukupa baba wa kukulea mwenye utu na mapenzi ya kweli.Mungu ambariki sana baba yako mlezi.
 
Back
Top Bottom