Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
FANI ZENYE AJIRA KWA SASA NA MKWANJE MREFU
Na, Robert Heriel
Leo sina maneno mengi, watu wengi wamekuwa wakilalamika ajira hakuna, sijui maisha magumu, wengine imefikia hatua ya kujidhuru kwa kutumia madawa ya kulevya, pombe, kujiuza na kudanga kisa tuu hawana mbele wa nyuma, hawana lila wala fila, yaani wapo wapo.
Wapo wanaonipigia simu kuomba ushauri kuwa wafanye nini kwani kila wafanyacho hakiendi, sasa nimeona niwaandikie ushauri wa kimajumui, kila mtu apate kujua ni ninni anapaswa kufanya ili maisha yasimpige TKO.
Anyway kama nilivyosema leo sitaki kuchosha mtu hapa, maana kuna wadau wangu wavivu wa kusoma makala ndefu. Sitaki kugombana nao.
Wasomi kwa wasiosoma, Vipanga kwa Vilaza, wajanja kwa vibushuti, wahitimu kwa waliohitiishwa shule, zifuatazo ni fani ambazo ukizisomea au ukipata ujuzi wake utakula bata mpaka uchoke;
Unatafuta ajira, huna haja ya kusumbuka wapi utapata ugali na pesa za kubadilisha malapa. Fani ya uchawa na Uking'asti kwa sasa ina soko kubwa ndani na nje ya nchi. Fani hii inakuhitaji ujipendekeze kwa watu mashuhuri, unachopaswa kufanya ni kutafuta mtu mashuhuri unayempenda au kama humpendi basi jigeze hivyo hivyo kuwa unampenda, anza kumshabikia, mposti uwezavyo, chora tattoo mwilini mwako, bandika picha zake chumbani kwako, vaa nguo zenye picha yake. Hapo tayari utakuwa umeweka Guard ya kumsogelea maana muda huo utakuwa upo mbali naye. Kisha siku akiwa na mkutano au tamasha basi jipeleke kwake hakikisha umejiseti vya kutosha na jina lako mtaani linnatambuliwa kuwa wewe ni mshabiki mkubwa wa fulani(huyo star). Mseme kwa mema hata kama anafanya vibaya. Baadaye unageuka kuwa chawa wake kama wewe ni mwanaume kwa mwanaume. Kama wewe ni mwanaume unamnyemelea Star wa kike, basi utakuwa King'asti wake.
Hapa utakula vihela mshenzi, hela za vocha, sijui nguo, na hata kigari cha kutembelea utapata kwani utapewa. Fani hii inahitaji usiwe na aibu sana, yaani weka pembeni kabisa.
Hii fani kwangu naiona ndio the best kwa sasa kutokana na shida na ugumu wa maisha kuongezeka. Ulozi ni sanaa, na uganguzi ni sayansi, hauhitaji kwenda shule bali kutumia tuu akili yako. Jikite zaidi kwenye propaganda, jifanye hugusiki, Destroyer, mnyama mnyambisi. Unda hila na njama za kilozi kisha gangua kwa uganga bandia ulionao. Andaa scripts na waigizaji wenye vipaji ambao watakusaidia kujenga jina lako.
Ulozi kwenye ndoa na mapenzi, hapa utapata wateja wengi, ulozi kwenye biashara na utajiri hapa utaondoka na kijiji. Hakikisha watu wanakuamini, yaani kabla hujaanza kazi ya ulozi na uganguzi basi anza kazi ya kuwafanya watu wakuamini. Tengeneza matukio makini yasiyo na dalili ya kushtukiwa na watu wengi, najua wapo wachache watakushtukia.
Wale watakaokupinga mbele za watu hakikisha uwe umewaseti wewe ili baadaye ujifanye wamepata madhara kisha watakuja kwako utawagangua, hii itajenga imani kwa watu wengine wenye imani haba.
Fani hii ni tamu sana na nzuri kwa sababu jamii yetu wajinga ni wengi hivyo kutajirika ni rahisi. Ajira hiyoooo
Nenda Gym, piga zoezi kata tumbo mapande manne, au sita ukiweza sana mapande nane. Kuwa sex-body, nenda kariakoo, au karume kama sio Ilala, kachukue viwalo vya mtumb vei chee, chukua Raba, usisahau spray au marashi hata ya buku mbili. Nyuka pamba, jipige maunyunyu harufu unukie, nenda sinza, tabata au kinondoni tafuta Star piga naye picha mbili tatu. Rusha insta na Facebook. Tongoza mademu wazito kistaa, ninaposema mademu wazito namaanisha wenye vipato vya uhakik sio hawa kina mwajuma wa Buza. Kama domo zege tafuta connection ya sangoma wa uhakika, ingia mjini na ndevu/ kibabe. Kula pesa kilaini. Hakikisha unakuwa mtanashati muda wote. Hiyo ni kozi ya umario.
Kudanga kwa kina dada, chukua mkopo kwenye vikoba kama laki tisa, hiyo nunua viguo vya bei nafuu walau nguo kumi na mbili za juu na chini. Bahati nguo za kike bei rahisi. Chukua viatu, chukua spray au marashi ya buku mbili. Usisahau kununua shumizi ya mazoezi. Laki tano kalipie Gym ya kisasa kwa mwezi ambayo watu wenye pesa huenda kufanya mazoezi huko. Laki moja tafuta hoteli ambayo kila siku utatumia elfu tano kunywa kinywaji kwenye hiyo hoteli, hakikisha hushobokei tu, jitenge kwenye meza yako pekeako, azima simu kali. Usisahau kutumia code switch na code mix unapoongea na danga kwani hiyo ndio official language ya kazi yako. Ajira ndio hiyo, pesa utakula mpaka ukimbie
Post picha za kipuuzi, andika upuuzi, rekodi upuuzi iwe ni video au audio. Hakikisha hugusi wakubwa wala usijiingize kwenye kumi na nane zao. Kwa maana nao hawatakuwa na muda na wewe kwani watajua umejiajiri kwenye fani yako ya Postology.
Fani hii soko lake ni kuwa na linagusa makundi yote na tabaka zote za kiuchumi, dini zote na kabila zote, yaani utapata hela mpaka ulie.
Jifanye mserikali kama upo CCM, kama upo Upinzania jifanye mharakati. Usikubali macho yako yatulie kuepusha kushtukiwa kama wewe ni mpambe na huna lolote basi vaa miwani nyeusi😀😀😀😀.
uwapo kijiweni jifanye Mserikali, yaani jifanye unajua kutoa ufafanuzi wa kina, usisahau kuweka uso wa kiserikali. Kuwa mtu wa Ilani, nashauri tembea na ilani kila mahali. Chambua mambo kwa kukisifia chama chako. Utashangaa pesa inaanza kukujia polepole, jasho lako halipotei bure.
Wimbo wako uwe kusifia alafu kiitikio pongezi.
Ukiwa upinzani, jifanye wewe ni mpiganaji usiye ogopa, unapoongea kunja uso panua mdomo kwa nguvu hakikisha misuli pembeni ya jicho(kwenye magacha) imetokea, geza sauti za kipinzani. Taratibu utaanza kujulikana.
Kumbuka kila kazi ina matokoe chanya na hasi, hivyo kuwekwa ndani pia utarajie
Kuwa mfuatiliaji, soma historia za timu, kesha usiku na mchana ukiangalia mechi, kuwa Youtuber kila video ya mpira uwe ushaiona kwenye Youtube duniani. Anza kubet kama mtaalamuna. Weka buku upate laki mbili, beti uwezavyo, jikite huko, penda kubet, ukilala bet, ukiamka bet, ukiota bet.
Huwezi kosa pesa
Mwisho, natumaini umefurahia na kuburudika
Wito, Fanya kazi halali zisizodhuru mtu yeyote au mazingira kwani kwazo hutavunja sheria.
Ulikuwa nami
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam

Hapa upo mkwanja nje nje, ni wewe tuu na ushapu wako wa kupata habari, kuzipika na kuzipakua, kupika majungu, kuyaanika na kuyaanua maumbeya ya watu. Fani hii zamani ilifanywa na kujulikana kama fani ya uandishi wa habari au utangazaji, lakini hauhitaji kusoma mpaka degree na kusumbuliwa na vi-coursework chuoni, fani hii inahitaji tuu kujichanganya mtaani na kuseti mingo na ving'amuzi vitakavyokunasia habari za moto. Hakikisha ziwe habari za kufarakanisha watu, kugombanisha watu, kuweka ligi baina ya mtu na mtu, hapo utapata hela. Lakini ukijifanya unaleta habari sijui za umbeya wa kuelimisha, fani itakudodea hapo. Fani hii kwa sasa vijana wa Dsm wamejiajiri sana, na miji ya Morogoro, pwani, na Tanga.1. Fani ya Umbeya, unoko na Uzandiki
Hii sijui tuiite Bachela ya Udalali na Ukuwadi 😀😀😀 wajuvi wa kingereza mtusaidie kuitranslate hii fani kwa kingereza. Hii ndio fani yenye mkwanja mrefu kwa sasa.Nafikiri ndio yenye heshima hapa Afrika. Fani hii haupaswi kwenda sijui UDSM au MZUMBE. Wewe ukishamaliza kidato cha nne, ukajua kusoma na kuandika, tena ukijua kingereza cha kuombea maji, baaasii! Wengine wakienda sijui kidato cha sita na chuo kikuu wewe wadere tuu, kisha ingia kazini. Bachela hii ina uwanja mpana sana hivyo kujiajiri ni wewe tuu unaamua uspesholaizi kwenye kitengo gani. Ipo kozi ya Udalali wa vyumba na nyumba, udalali wa mashamba na viwanja, udalali wa magari, udalali wa pikipiki, udalali wa vitu used, udalali wa simu, laptop na accessories, yaani hii kozi ukisomea kitaa hulali njaa. Uwanja wake ni mpana. Haya kuna Ukuwadi wa wanawake wazuri, kuna ukuwadi wa masupastaa,. Vijana wa kitaa hizi fani zinawalipa na wanaendesha maisha kitajiri sana.. 2. Fani ya Udalali na Ukuwadi
Hii ni Bachela ya Chawa with Uking'asti.3. Fani ya Uchawa na Uking'asti
Unatafuta ajira, huna haja ya kusumbuka wapi utapata ugali na pesa za kubadilisha malapa. Fani ya uchawa na Uking'asti kwa sasa ina soko kubwa ndani na nje ya nchi. Fani hii inakuhitaji ujipendekeze kwa watu mashuhuri, unachopaswa kufanya ni kutafuta mtu mashuhuri unayempenda au kama humpendi basi jigeze hivyo hivyo kuwa unampenda, anza kumshabikia, mposti uwezavyo, chora tattoo mwilini mwako, bandika picha zake chumbani kwako, vaa nguo zenye picha yake. Hapo tayari utakuwa umeweka Guard ya kumsogelea maana muda huo utakuwa upo mbali naye. Kisha siku akiwa na mkutano au tamasha basi jipeleke kwake hakikisha umejiseti vya kutosha na jina lako mtaani linnatambuliwa kuwa wewe ni mshabiki mkubwa wa fulani(huyo star). Mseme kwa mema hata kama anafanya vibaya. Baadaye unageuka kuwa chawa wake kama wewe ni mwanaume kwa mwanaume. Kama wewe ni mwanaume unamnyemelea Star wa kike, basi utakuwa King'asti wake.
Hapa utakula vihela mshenzi, hela za vocha, sijui nguo, na hata kigari cha kutembelea utapata kwani utapewa. Fani hii inahitaji usiwe na aibu sana, yaani weka pembeni kabisa.
Bachela ya ulozi, uganga na Uganguzi.4. Fani ya Ulozi, uganga na uganguzi
Hii fani kwangu naiona ndio the best kwa sasa kutokana na shida na ugumu wa maisha kuongezeka. Ulozi ni sanaa, na uganguzi ni sayansi, hauhitaji kwenda shule bali kutumia tuu akili yako. Jikite zaidi kwenye propaganda, jifanye hugusiki, Destroyer, mnyama mnyambisi. Unda hila na njama za kilozi kisha gangua kwa uganga bandia ulionao. Andaa scripts na waigizaji wenye vipaji ambao watakusaidia kujenga jina lako.
Ulozi kwenye ndoa na mapenzi, hapa utapata wateja wengi, ulozi kwenye biashara na utajiri hapa utaondoka na kijiji. Hakikisha watu wanakuamini, yaani kabla hujaanza kazi ya ulozi na uganguzi basi anza kazi ya kuwafanya watu wakuamini. Tengeneza matukio makini yasiyo na dalili ya kushtukiwa na watu wengi, najua wapo wachache watakushtukia.
Wale watakaokupinga mbele za watu hakikisha uwe umewaseti wewe ili baadaye ujifanye wamepata madhara kisha watakuja kwako utawagangua, hii itajenga imani kwa watu wengine wenye imani haba.
Fani hii ni tamu sana na nzuri kwa sababu jamii yetu wajinga ni wengi hivyo kutajirika ni rahisi. Ajira hiyoooo
Yaani ushindwe mwenyewe, waache waende shule wewe anzisha kanisa jiite nabii wa nyota ya sabini na saba au jiite sheikh sharifu wa Muscat. Wakimaliza shule watakuja kwako uwaombee ili wapate kazi, waambie wamelogwa na wanamikosi ya ukoo. Unda watu wa kuigiza kwenye kazi yako hiyo wajifanye umewaombea na wamefanikiwa kuajiriwa kwenye makampuni na kazi zenye heshima. Piga pesa kilaini.5. Fani ya Upako, Upakozi,unabii wa bwana
Hii ni Bachela ya mario na dangazi.6. Fani ya Umarioa na Kudanga
Nenda Gym, piga zoezi kata tumbo mapande manne, au sita ukiweza sana mapande nane. Kuwa sex-body, nenda kariakoo, au karume kama sio Ilala, kachukue viwalo vya mtumb vei chee, chukua Raba, usisahau spray au marashi hata ya buku mbili. Nyuka pamba, jipige maunyunyu harufu unukie, nenda sinza, tabata au kinondoni tafuta Star piga naye picha mbili tatu. Rusha insta na Facebook. Tongoza mademu wazito kistaa, ninaposema mademu wazito namaanisha wenye vipato vya uhakik sio hawa kina mwajuma wa Buza. Kama domo zege tafuta connection ya sangoma wa uhakika, ingia mjini na ndevu/ kibabe. Kula pesa kilaini. Hakikisha unakuwa mtanashati muda wote. Hiyo ni kozi ya umario.
Kudanga kwa kina dada, chukua mkopo kwenye vikoba kama laki tisa, hiyo nunua viguo vya bei nafuu walau nguo kumi na mbili za juu na chini. Bahati nguo za kike bei rahisi. Chukua viatu, chukua spray au marashi ya buku mbili. Usisahau kununua shumizi ya mazoezi. Laki tano kalipie Gym ya kisasa kwa mwezi ambayo watu wenye pesa huenda kufanya mazoezi huko. Laki moja tafuta hoteli ambayo kila siku utatumia elfu tano kunywa kinywaji kwenye hiyo hoteli, hakikisha hushobokei tu, jitenge kwenye meza yako pekeako, azima simu kali. Usisahau kutumia code switch na code mix unapoongea na danga kwani hiyo ndio official language ya kazi yako. Ajira ndio hiyo, pesa utakula mpaka ukimbie
Bachela ya Ubodigadi. Kazi ni ninyi ndugu zangu. Nyanyua chuma, nunua miwani nyeusi, tafuta na vibode vyeusi, kisha tafuta viatu vikubwa vyeusi vya kijeshi au buti la jeje. Kisha nenda kwa Star yeyote mwambie uwe mlinzi wake binafsi. Fani hii inapendeza za kwa watu wakubwa kwa mwili, weusi na wenye sura mbaya isiyovutia. Lakini wale wenye sura za mama zao hapa msithubutu.7. Fani ya Ubodigadi
Bachelor of Postology. Fungua page facebook, instagram, website, au Blog. Usisumbuke kupost vitu vya maana utakufa njaa ndugu. Post upuuzi kwa kadiri ya uwezavyo ukivunja sheria za nchi shauri yako na yao, posti uwezavyo upuuzi ndio ujikite huko. Usisome sana comment utakosa upuuzi wa kupost.8. Fani ya Kuposti
Post picha za kipuuzi, andika upuuzi, rekodi upuuzi iwe ni video au audio. Hakikisha hugusi wakubwa wala usijiingize kwenye kumi na nane zao. Kwa maana nao hawatakuwa na muda na wewe kwani watajua umejiajiri kwenye fani yako ya Postology.
Hii ni fani ambayo soko lake ni kubwa, hapa ukijikita hakuna atakayekufikia kwa utajiri hata huyo Mo dewji atakuja kukopa kwako. Tafuta bidhaa ya Vumbi la Kongo, Mundende ganzi mujarabu, puturii na musinula munula. Tangaza unatibu nguvu za kiume, wateja watamiminika mpaka uwafukuze. Raha ya biashara hii hakuna cha TRA wala manispaa watakaokusogelea. Tena unaweza kuwa rafiki mkubwa wa watu wazito. Jiite Mundende mutu ya Kivu ya kaskazini, watu watakuja kununua dawa si unajua watanzania wanapenda sana ngono wengi wao. Hiyo ni kozi ya kwanza inayowahusu wanaume. Ukiwa na tamaa sana na mroho wa hela basi malizia na mradi wa chura mnesaji, wanawake waongeza makalio na hipsi, huko mjini wanasema nyumba ni choo. Wametaka wenyewe, wewe wape tuu wao wakupe pesa yako ukale bata.9. Fani ya Mkongo na Chura mnesaji
Fani hii soko lake ni kuwa na linagusa makundi yote na tabaka zote za kiuchumi, dini zote na kabila zote, yaani utapata hela mpaka ulie.
Bachela ya decorate singing😀😀😀. Tafuta chama ukipendacho cha siasa, iwe ni CCM au chama chochote Cha upinzani, jifanye wewe ni mshabiki lia lia wa chama hicho. Kitetee hata kama hakihitaji kutetewa, kisemee hata kama hakihitaji kusemewa, jifanya mchambuzi na muandishi wa makala za kupongeza na kusifia, hakikisha unajua birthday ya viongozi wa chama chako wote waliowakuja, wa-wish kadiri uwezavyo, msiba ukitokea kwenye familia ya moja ya viongozi wa chama chako, hakikisha unakuwa kwenye top10 ya waliompa pole mtandaoni ikiwezekana kufika kwenye msiba, hakikisha kama utapata nafasi unahudhuria kwenye mazishi kama sio kubebe jeneza. Sifia kwa kadiri uwezavyo. Usikubali kupitwa na wenzako pindi usifiapo.10. Fani ya Uimbaji wa mapambio
Jifanye mserikali kama upo CCM, kama upo Upinzania jifanye mharakati. Usikubali macho yako yatulie kuepusha kushtukiwa kama wewe ni mpambe na huna lolote basi vaa miwani nyeusi😀😀😀😀.
uwapo kijiweni jifanye Mserikali, yaani jifanye unajua kutoa ufafanuzi wa kina, usisahau kuweka uso wa kiserikali. Kuwa mtu wa Ilani, nashauri tembea na ilani kila mahali. Chambua mambo kwa kukisifia chama chako. Utashangaa pesa inaanza kukujia polepole, jasho lako halipotei bure.
Wimbo wako uwe kusifia alafu kiitikio pongezi.
Ukiwa upinzani, jifanye wewe ni mpiganaji usiye ogopa, unapoongea kunja uso panua mdomo kwa nguvu hakikisha misuli pembeni ya jicho(kwenye magacha) imetokea, geza sauti za kipinzani. Taratibu utaanza kujulikana.
Kumbuka kila kazi ina matokoe chanya na hasi, hivyo kuwekwa ndani pia utarajie
Bachelor of Betting with Kamaring.11. Fani ya Kubet na kamari
Kuwa mfuatiliaji, soma historia za timu, kesha usiku na mchana ukiangalia mechi, kuwa Youtuber kila video ya mpira uwe ushaiona kwenye Youtube duniani. Anza kubet kama mtaalamuna. Weka buku upate laki mbili, beti uwezavyo, jikite huko, penda kubet, ukilala bet, ukiamka bet, ukiota bet.
Huwezi kosa pesa
Ukishindwa hayo hapo juu ingia kwenye fani ya motivation Speaker, moto-visheni spika, yaani kutia moto watu kwenye jambo fulani kwa kutoa sauti. Hamasisha watu wapate utajiri, waambie walime maembe, mananasi ni biashara nzuri, hamasisha kilimo cha matikiti na nyanya, waambie heka moja unaweza pata milioni hamsini. Wapigie hesabu ya magazijuto, wazidishie bila kugawanya, wajumlishie bila kutoa. Waambie faida ni ndefu. wauzie vitabu na Cd zinazoelezea utajiri wa mayai ya kware, waambie jinsi mkono wa sunngura ulivyobadilisha maisha ya tajiri fulani(tafuta jina la kizungu la uongo liwe case study watanzania hawawezi kufuatilia ni wavivu wa kusoma) , usisahau kuvaa suti za soko la Meimoria ulizopeleka kwa fundi maiko azimodoe. Jiweke sopu sopu, hakikisha kingereza kisikuache mara kwa mara, nukuu hata nukuu za kujitungia ziweke kwa kingereza sema mwanafalsafa Taikon vIgert mwaka 1832 alisema '" To be Reach is a individua decision" ipambe hiyo nukuu kisha sema kwa wasioelewa Taikon alimaanisha " Kutajirika ni uamuzi wa mtu" Kumbe hakuna cha Taikon wa ndugu yake Taikondo. Maneno ya kutunga. Ukitaka uwamalize kabisa nenda ukiwa umebeba vitabu kama vitatu, viwili vya kingereza, kimoja cha kiswahili. Hakikisha unanukuu nukuu moja kutoka kwenye kitabu ulichobeba kisha nukuu zingine unaweza kujitungia tuu na nukuu za uongo mfano; Katika Kitabu cha Bujibuji, chenye jina la "DIE RICH" alichoandika mwaka 1930 ukurasa wa sita anaeleza namna mtu anavyoweza kutajirika. Kumbe Bujibuji hajawahi kuandika kitabu, tena yupo Jamii Forum hana hili wala lile. Hakikisha jina hilo wasikilizaji wako hawapo aware nalo usijeshtukiwa.12. Fani ya Moto-visheni spika