Zote Kibunango.
Walioanza karibu ikabidi mmoja asafiri ,pia walioanza tayari wakiwa mbali mbali.
Nina mifano kadhaa kuhusu yote hayo mawili, ila sitaweka conclusion. Itakuwa ni jukumu la msomaji kujudge.
Galawoso (sio jina halisi) aliamua kuanzisha mahusiano ya mbali, ilikuwa ni kipindi kile chat maarufu ya IRC ilipokuwa kitamba sana kwa kukusanya dunia nzima katika mkondo mmoja. Moja ya sehemu ya chat hiyo ilikuwa ni mahsusi kwa ajili ya wale wapendao kupata wapenzi wa mbali. Galawoso alijiunga na chat hiyo, na baada ya muda sio mrefu aliweza kupamta binti mmoja, ambaye baada ya kuwasiliana kwa muda mrefu walijiona wao ni wapenzi. Hivyo wakawa rasmi kama ni wapenzi.
Njia kubwa waliotumia kudumisha penzi hilo ni mawasiliano kupitia chat hiyo na emails, hata mambo yakipozidi kufana na kujiona wapo karibu, walihamia kwenye simu. Hii iliweza kuwafanya kuwa karibu kabisa. Kipindi hicho webcam ilikuwa bado kuanza. Hivyo sauti tu ilitosha.
Galawoso kipindi hicho alikuwa ni mwanafunzi na mpenzi wake alikuwa ni mfanyakazi katika chuo kama Secretary, na moja ya kazi zake ilikuwa ni kupokea maombi ya wanafunzi wapya. Kilele cha mapenzi yao yaliyodumu kwa mwaka mmoja na nusu, ilikuwa kwa Galawoso kujiunga na chuo hicho ili aweze kwa mara ya kwanza kuwa pamoja na mpenzi wake. Binti huyo alihakikisha kuwa ni lazima Galawoso apate chuo hicho. Hivyo akamtumia fomu za maombi, na baada ya taratibu zote kwisha, Galawoso alifanikiwa kupata chuo, ikiwa ni hatua ya awali ya kuweza kuonana na mpenzi wake bila chenga.
Miezi mitatu kabla ya Galawoso hajapanda ndege kwenda kumwona binti huyo, alipokea email toka kwake ambayo imemsumbua hadi leo hii. Katika email hiyo binti huyo aliamua kuvunja uhisiano nae na mbaya zaidi kufuta hata hiyo nafasi ya kusoma chuoni hapo.
Binti alimweleza kuwa amekuwa akikutana mara kwa mara na kijana toka Nigeria, ambaye amemwambia kuwa Watz ni waongo sana kwenye masuala ya mapenzi. Na ni watu wa kutumia long distance relationship kwa manufaa yao binafsi. Hivyo basi ameamua kusitisha uhusiano nae, na kumtaka samahani kabla ya kuongeza kuwa wanaweza kuendelea kama marafiki.
Huo ni mfano mmoja... mengine itafuata...