Fanikisha mahusiano ya mbali. . .

Fanikisha mahusiano ya mbali. . .

Hahaha,huyo Juma ni hatari.
Asante tena Kibunango. . . mifano yote ina mafunzo ndani yake.
 
Hapo kwenye bold ndo kunanifanya niseme "I don't trust anybody and I don't demand to be trusted either."

Hubby akiniletea za kutoniamini nachukua muda wangu ku explain wala sikasiriki kwani I feel same kwake pia. Lazima kuishi kimachale. Kuusemea moyo wa mtu mwingine utaishia kuzimia siku ukikuta ulichosema sicho.

Umeona sasa Lizzy,

Ndiyo maana nikasema kuwa mahusiano yanawahusisha watu wawili, na kila mtu ana kichwa chake mwenyewe na akili zake zinamtosha mwenyewe...Ni vigumu kujua analilowaza.

Halafu kwenye hii story,...huyo dada anaomboleza hadi leo kwani alitema wachumba kibao kwa kumsubiri mtu ambaye hakustahili kupewa hiyo share!!
 
Watu hawaishi kuuliza kama inawezekana kuwa na mtu ambae yuko mbali nae na mahusiano yao yakasurvive.
Jibu ni NDIO, ila kuna mambo ambayo mnatakiwa mzingatie ili mfanikishe mahusiano yenu.

First things first...
1.Kama wewe ni mtu ambae una "commitment issues" this is not for you.Kuweza kuvumilia kutokuwepo kwa mwenzio karibu kunahitaji kujitoa kwa hali ya juu na dhamira iliyonyooka.
2.Kama humpendi mwenzako (unamtamani tu) this is not for you. Ukiwa unatamani kitu ambacho hukipati kwa wakati ni rahisi kuangalia kile kilichopo karibu yako.
3.Kama humwamini mwenzi wako/mwenzi wako hakuamini wewe au wewe mwenyewe hujiamini this is not for you. Bila kuaminiana mtakua na mtafaruku kila siku. Umbali utasababisha maneno/kuwekana hatiani na kuhisiana vibaya kuwepo sana.Kitu ambacho kitasababisha ugomvi mara kwa mara na kusababisha mrudi nyuma kimahusiano badala ya kusonga mbele.
4.Kama huna malengo ya mbali na mwenzako this is not for you. Ikiwa huoni ukiwa na huyo mwenzako miaka miwili mitatu mbeleni mwache aende tu. Hamna haja ya kumfunga mwenzako na mahusiano ya mbali wakati hana umuhimu sana kwako.
5.Kama ni mwepesi wa kuchukua maneno ya watu bila kuyafanyia kazi this is not for you.Utaishia kupata presha bure na kugombana na mwenzio kila siku.
6.Kama ni mvivu wa mawasiliano this is not for you. Kitu pekee kinachoweza kukuweka karibu na mwenzako wakati mko mbali mbali ni mawasiliano.E-mail, Simu, Texting, Skype n.k ndivyo vinavyoweza kupunguza umbali uliopo kati yenu walau kidogo.Hivyo kama hili huliwezi basi jua fika ni muda tu haujafika wa mahusiano yenu kuanguka.

Kwa wale ambao wanafikiria kujiingiza kwenye mahusiano ya mbali jua inawezekana ikiwa tu una nia ya kuyawezesha mahusiano yenu.Kama huna bora uende uendako siku ukarudi na kumkuta mwenzako bado yuko yuko ndio ujaribu.

Kwa wale ambae ndio wanahangaika nayo sasa hivi muhimu ni uwe mwaminifu,uwe na imani na mwenzako,ujitume kwenye swala zima la mawasiliano na msisahau kuongelea "them good times".Hii inasaidia kukumbushana umuhimu wenu kwa kila mmoja na kwamba japo mnakosana kwa muda, mtakapoweza kuwa karibu tena maisha yenu yatapendeza. Mjali mwenzako kwa maneno mazuri, epuka kuanzisha maugomvi yasiyo na pembe wala mkia, usimpe sababu ya kufurahia umbali wako.

Mwisho. . . kama ni kucheat hata unaelala nae kitanda kimoja kila siku, unaekunywa nae chai kila asubuhi na kubebana kazini kila jioni anaweza kucheat, hivyo hili haliletwi na umbali bali tabia binafsi. Hivyo kama wewe ni mvumilivu go ahead and give it a try huku ukiomba na kuamini kwamba mwenzako nae yuko hivyo hivyo pia kama hajakupa sababu ya kufikiria vingenevyo.

Nawatakieni LDS(s) zitakazovuka na kukwepa vikwazo. Kila la heri wote mnaohusika.

PS
Mawazo zaidi na experience zinakaribishwa.
Hapo kwenye red,mawasiliano sometimes yanaboa we hujui tu
 
experience zinakaribishwa.

Xperience yangu ndio inanihukumu kuamini tena mahusiano ya mbali....
Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kukaa mbali na GF wangu kipindi hicho secondary na ndio ilikuwa mara ya kwanza kufanywa mjinga......
Kibaya zaidi marafiki zangu walinicheka sana na hawakuni-support toka mwanzo mimi kuwa na mahusiano ya mbali na huyo binti,
hii naomba nikiri kuwa imeniathiri sana coz nilishindwa kuwa prove wrong watu wangu kuwa "mapenzi ya mbali yanawezekana"....
Ila sihukumu mabinti wote nadhani nina nafasi nyingine for the next experience "labda"...

Hehehehe. . .pole jG.
Ila huoni kwamba umri unaweza ukawa ulichangia kwa kiasi kikubwa? Maana hua nasikia (mwenyewe sijaexperience) kwamba sekondari na vyuoni ndio wengi hua wanawasaliti wapenzi wao kwa ulimbukeni. So usikate tamaa, there is still hope for you.Na usisahau kwamba wa kukisaliti hata uwe nae beneti masaa ishirini atakusaliti tu.
 
Ah inawezekana pia....
Basi toka hapo sijawa tena na wa mbali tena...
Suala la kucheat ni pana sana ila kidogo mtu ukiwa nae karibu bwana unaweza kujidanganya kuwa "wako peke yako"
Ila akiwa mbali afu ukiwa mtu wa miwivu kama mimi ah kila saa roho juu juu lol.....
Ila sikomi tu!
Siwezi na sipendi ku-generalize.
 
Hahahaha. . . wako peke yako atakua wako peke yako hata awe miles away. Na wakushea hata akienda kibandani, au ukiingia bafuni tu imekula kwako.

Ila nafurahi kusikia bado una imani japo hujajaribu tena.
 
Lizzy, Thanks for the useful thread! Indeed you have touched my mind from A - Z including the gamma, betta, alpha ect. I have my GF who is in Dar and I am in a foreign country. I got to know the girl while when I was living in dar but we didn't have any kind of serious relationship. Soon when I left to this foreign country, I proposed to her and she agreed and we moved on well with almost everyday communicating and enjoying our love during the first year of which was also her last year of study in one of the Tz varsity.

Soon after she completed her study, things turned around! Its about three - four months now communication is a big problem! she just say " I am trying my best, and you know now am working so its not easy for me to be online everytime". But in reality, even when I expect her to be online like on weekend days, she don't be. She only communicate with me every 2 ~ 3 days sometimes even after a week. I have tried to convince her to improve her communication but not any significant improvement.

Yaani ni pasua kichwa sasa, natamani nisingekuwa kwenye relationship kwani naona kama hayuko tena committed. Ushauri cha kufanya pls.
 
Heey. . . pole kwa kupasuliwa kichwa.Lolzz

Neway swala la mawasiliano kubadilika linaweza kuwa limesababishwa na mengi. Kwanzia kukuchoka, yeye kua na mambo mengi sana, yeye kupoteza interest/hisia na wewe, kuona mtu mwingine anaemvutia zaidi, kupoteza matumaini na mahusiano yenu. . . yani kwa ujumla yapo mengi. Na huwezi kurekebisha tatizo usilolijua hivyo ningekushauri next time ukipata hiyo bahati ya kuongea nae umuulize kama bado hisia zake kwako ni kali? Bado anataka muendelee kuwa pamoja? Kama kuna mtu mwingine anamvutia n.k Ila sasa kabla ya kumuuliza uwe umejiandaa kwa lolote maana anaweza akakwambia kuna mtu amevutiwa nae alikua hajapata tu namna ya kukwambia, hivyo ujiandae kuwa disappointed maana uwezekano huo upo. Alafu nadhani unaweza ukawa unawafahamu baadhi ya marafiki zake, ongea nao.Ask around, ili ujue kama akili yake imehamia kwa mtu mwingine usonge zako mbele badala ya kusubiria kitu kosichopo.

Good luck.
 
Nilibahatika kupata udhamini wa kusoma nje ya TZ kwa miaka miwili. Sikuwa peke yangu, tulikuwa ni wengi na ni wengi sana. Tofauti miongoni mwetu ilikuwa ni muda wa masomo. Wapo waliopata udhamini wa miaka mitatu, miwili na miezi tisa.

Kundi la miezi tisa wengi wao walikuwa tayali wana mahusiano ya kindoa, uchumba na uhusiano wa kawaida wa kimapenzi. Wengi tuliona kwa miaka miwili/mmoja ama miezi tisa ni muda mfupi sana. Zaidi waliokuwa kwenye mahusiano walipenda kusisitiza kuwa huo ni muda mfupi sana na utakwenda haraka pasipo kujua. Mie niliyekuwa single sikuwa na chochote cha kujadili katika hilo, kwani ndoto zangu zilijiweka zaidi katika kukutana na marafiki wapya wa kike.

Baada ya miezi mitatu ugenini mambo yalianza kubadilika. Hapa napenda kuweka wazi kuwa mwezi wa kwanza huko ugenini, ulikuwa ni mwezi Mtukufu, Jiji lilikuwa limepoa na utulivu usio kifani. Mwezi uliofuata ulikuwa wa kuzoea shule mpya na kujaribu kupata hili na lile katika mazingira ya ugenini.

Vituko vilianza mapema baada ya kumalizika kwa miezi mitatu, ingawa dalili za kupotoka zilianza mapema kidogo ya hapo. Ni siku ambayo kijana mmoja aliposhauri kufanyike party nyumbani kwake, akinadada wakiandaa vyakula mbalimbali na akina kaka wakiingia madukani kutafuta kila aina ya vinywaji kwa party hiyo. Huu ulikuwa ni mwanzo wa kuona ni jinsi gani long relationship inavyoweza kutofanikiwa kwa sababu mbalimbali ... Hapa chini naweka mifano kadhaa kwa yale niliyoweza kuyaona baada ya watu kufunguka baada ya party hiyo.

Ashura
Ni mke wa mtu wa kawaida hapo nyumbani (TZ). Mumewe ni fundi mkubwa wa magari na wamejariwa watoto wawili katika ndoa yao ya miaka sita. Ashura ni mfanyakazi serikalini na ni msichana mwenye kujipenda sana. Sio mimi ama mumewe ambaye alikuwa anajua nini Ashura anapenda siku zote. Kumbe binti huyu anapenda sana watu maarufu.

Kupitia party hiyo na baadae baada ya party hiyo alianzisha uhusiano wa kudumu na kijana moja ambaye alikuwa ni maarufu sana huko nyumbani (TZ). Hakuona aibu yoyote ya kumsaliti mume wake. Alifanya kila alichoweza kumweka karibu kijana huyo kwa muda wote wa miezi tisa aliyokaa hapo.

Fatuma
Hakuwahi hata siku moja kuamwamini mume wake. Mume wake ndie aliyemchongea mchongo wa kwenda kusoma nje ya Tanzania. Siku zote alikuwa kwenye simu akiongea na mume wake, hatukujua ni mapenzi ama ni wivu tu. Wiki moja kabla ya party hiyo alionekana kuwa ni mnyonge sana. Shoga zake walisema kuwa mume wake ameondoka TZ na kwenda nje ya nchi kikazi.

Fatuma kwa upande wake aliona kuwa mume wake atakuwa ameenda kufanya ufuska kwa kimada mmoja ambae alikuwa nje ya TZ lkn nchi tofauti na yetu. Tokea siku hiyo nae akaona isiwe shida, wenye bahati wakabahatika

Mwaka mmoja baada ya kurudi Tanzania ndoa yao iklivunjika.

Grace
Baada ya kudumu katika ndoa kwa miaka zaidi ya sita, alijikuta hana hamu tena na mume wake. Na zilipotekea nafasi za kusoma nje aliona ndio wakati pekee ambao ataweza kurejesha upendo kwenye ndoa yake iliyoweza kutoa watoto wazuri wawili. Akiwa ni afisa mkubwa serikalini na mume akiwa ni afisa katika idara ya nje ya serikali maisha yao yalikuwa ni mazuri sana.
Aliwabeza sana wale wote ambao wameshindwa kuvumilia katika kipindi hicho kifupi cha kwa na wapenzi hao. Alijiangalia matatizo yake kwenye ndoa yake na nafasi yake aliyokwa nayo, na akaona bado anaweza kuhimili mahusiano ya mbali.

Miezi sita baada ya ile party, alionekana kapendeza sana, kulikoni? Kumbe nae tayali kesha ingia kundini! Uzalendo ulimshinda na kuamua kutafuta kijana... Baada ya kurudi nyumbani aliamua kujitenga na mume wake.. dhamiri imemponza?

Juma
Huyu ndie aliyekuwa kinara wa kuchambua wale wote walioshindwa kuwa wahaminifu kwenye mahusiano yao ya mbali. Zaidi umaarufu wake ulizidi kwa kuwa ndie Mtz pekee aliyekuwa analeta mawasiliano ya simu kwa watz.(Mobile phone in early 90's ilikuwa issue)

Akiwa ameacha watoto watatu na mke nyumbani, alijikuta akiingilia ndoa ya mtu kwa kujihushisha na mke wa mtu. Uhusiano wao ulidumu kwa muda mrefu sana, kabla ya mwanamke huyo kujua kuwa hakuwa peke yake.

Mwanamke amepoteza ndoa yake na Jamaa sasa ana wake watau.

Zuhura
Hakuwahi kuwa kwenye serious relationship, Hata hivyo kabla ya kuondoka TZ alikuwa engaged! Na siku zote mdomo wake ulijaa jina la kijana mtarajiwa. Mwaka mmoja baadae kaishia kwa mnajeria

Sasa anaishi Marekani na ana watoto watatu.
Kibunango huyu bwana Juma ni balaa...lol
 
Heey. . . pole kwa kupasuliwa kichwa.Lolzz

Neway swala la mawasiliano kubadilika linaweza kuwa limesababishwa na mengi. Kwanzia kukuchoka, yeye kua na mambo mengi sana, yeye kupoteza interest/hisia na wewe, kuona mtu mwingine anaemvutia zaidi, kupoteza matumaini na mahusiano yenu. . . yani kwa ujumla yapo mengi. Na huwezi kurekebisha tatizo usilolijua hivyo ningekushauri next time ukipata hiyo bahati ya kuongea nae umuulize kama bado hisia zake kwako ni kali? Bado anataka muendelee kuwa pamoja? Kama kuna mtu mwingine anamvutia n.k Ila sasa kabla ya kumuuliza uwe umejiandaa kwa lolote maana anaweza akakwambia kuna mtu amevutiwa nae alikua hajapata tu namna ya kukwambia, hivyo ujiandae kuwa disappointed maana uwezekano huo upo. Alafu nadhani unaweza ukawa unawafahamu baadhi ya marafiki zake, ongea nao.Ask around, ili ujue kama akili yake imehamia kwa mtu mwingine usonge zako mbele badala ya kusubiria kitu kosichopo.

Good luck.

Thanx, ngoja nisubiri hiyo bahati nitakapoipata nitaongea naye.
 
Back
Top Bottom