Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Fanta alizaliwa katika familia duni mno. Baba yake alikua mlinzi, katika harakati za kuhakikisha hawakosi chakula nyumbani mama aliuza matunda mchana.
Fanta alikua na uzuri wa ajabu alikua na akili pia lakini alipofika kidato cha tatu baba yake alipata maradhi, hali ya nyumbani ilibadilika. Mama alimtunza mgonjwa ilibidi Fanta auze matunda ili kuisaidia familia.
Siku moja Fanta akiwa na karai lake la ndizi na machungwa alikutana na kijana mmoja, yule kijana kuuona uzuri wa Fanta moyo wake ulipata hisia kali. Aliongea na Fanta kununua matunda yote na change alikataa. Aliomba na kesho aletewe matunda.
Yule kijana alikua amerudi kutoka masomoni na alikabidhiwa kiwanda na baba yake. Aliwapa wafanya kazi matunda wale. Siku ya pili alinunua matunda na kuomba kumrudisha Fanta nyumbani kwao.
Siku ya tatu aliomba kumpeleka Fanta kula, Fanta akiwa na mavazi yake ya hali ya chini alikataa, kijana Ali omba amnunulie nguo, Fanta alimueleza kuwa wazazi wake hawata muelewa. Ilibidi kijana akawaone wazazi. Mwisho wa siku Fanta aliolewa harusi ya kifahari.
Fanta alikua mama wa nyumbani, alijifunza kuendesha gari akawa anawapeleka watoto shule. Siku moja aliona tangazo la kazi, kuna sonara alitafuta muuza duka. Fanta aliomba ile kazi na aliipata. Mume wake alimuambia kama haita ingilia ratiba za familia yeye hana tatizo.
Sonara alimuamini sana Fanta na aliweza kufanya shughuli zake nyingine Fanta akiwa dukani. Fanta alianza kazi baada ya kupeleka watoto shule na alimaliza saa nane watoto wanapomaliza shule.
Fanta hakuugusa mshahara wake kwa miaka mitano. Hakuwa ana uhitaji na mume wake alisha wanunulia wazazi wa Fanta nyumba na aliwapa allowance kila mwezi iliyowatosha kuishi. Fanta aliweza kufungua duka na alifanya kazi na familia yake. Fanta aliweza kuibadilisha familia yake kwa akili zake mwenyewe.