Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Momba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fanuel Siyame akiwa katika ziara ya kuwanadi wagombea wa Vijiji na Vitongoji wa chama hicho katika mikutano ya Kampeni, ameeleza namna Chama cha Mapinduzi kilivyoshindwa kutekeleza Ilani yake jimboni humo kwa kushindwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ukosefu wa maji safi na Salama, Ubadhirifu wa fedha za umma katika Ofisi za Vijiji na Vitongoji, ushuru kandamizi kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo katika Vijiji na Vitongoji, miundombinu mibovu ya barabara.
Pia Siyame amesema licha ya kuenguliwa kwa wagombea wao katika baadhi ya Vijiji na Vitongoji na huko kusikokuwa na wagombea kupiga kura za hapana ii uchaguzi wa huo uwe na Marudio.
Amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa siku ya tarehe 27/11/2024.