Fanya haya kila ununuapo mtungi wa gesi ya kupikia majumbani

Unafaham majiko ya pinetech?
Yale yanatoa moto mwekundu na ni too hot.

Haina flame ya blue kamwe ile jiko.

Naomba ueleze hii case kwenye pinetech.
 
Basi nishapigwa sana, japo orxy huweka seal leak ni nikiweka mtu bila kuutikisa kwanza moto hauwaki na gesi inatoka. So nachofanya ni kuutikisa Kwa sekunde kadhaa kama naulaza baada ya hapo moto huwaka lakini njano always IPO.

Napata somo hapa inawezekana oxygen ni nyepesi zaidi ya gesi inayowaka, hivyo hukaa juu ya mtungi.
 
Serikali kupitia tbs watoe elimu kuhusu hizi gesi zinazouzwa kwa mangi zinapaswa ziweje. Watu wanaibiwa mno!

Au wenye makampuni ya gesi watoe elimu gesi zao zinaponunuliwa kwa mangi kama zina rangi tofauti basi zirudishwe. Uone kama uswahili utakuwepo tena.


au raia wasusie duka/ brand za mitungi ya gesi zenye mapungufu hayo afu tuone nani atakufa kibudu.

Hii nchi kila mtu mwizi si ccm si wafanyabiashara.
 
Pia chini ya jiko lako la kupikia (PLATE) kuna Sehemu ya ku regulate uwiano wa kiwango cha gas na oxygen,ukiona moto bi njano au sufura zinakuwa na moshi inawezekana kabisa uwino wa gas na oxygen sio mzuri,inua jiko rekebisha.
Hii inategemeana na aina ya jiko unalotumia kwa wale wa plate zingatia hili
 
Asante, ila sasa kama siyo wa buluu ninatakiwa nifanye nini? Niupeleke TBS? Au Tume ya Ushindani?
 
Halafu utasikiakwenye majukwaa na siasa zao za tutumie nishati safi ya kupikia wakati wameshindwa kushughulikia kwanza upatikanaji, ubora wake na gharama za hiyo nishati safi hasa sehemu za vijijini hasa kule Kantalamba na Kizuramimba, Nyathorongo, Nyamunga,Mirare, Mkoma
 
Niwe mkweli tu mara ya mwisho kuuona huu mwangaza wa blue ni enzi hizo gesi inaingia ingia na nilijua sababu ndio kitu kigeni hivyo nikawa natazama kwa makini nikihofia kulipuka


Sasa hivi sioni kitu hiko na natumia kampuni inayoanza na O na rangi yake ni msimbazi, kuhusu hewa mzigo hata nikiuwasha hapa nje kabisa bado rangi ni ya pili


Sisemi kitu ila Ok🤣, kama ni kweli sishangai maana TZ janja janja nyingi faida kwanza mengine baadae

Na Mlaji wa mwisho ndio mtaji mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…