Fanya haya kuongeza thamani ya ibada yako katika mikusanyiko ya kiroho

Sijaelewa unachotaka ni nini, au mkanganyiko uko wapi.

Point yako ya kwanza imesema tuingine na mahitaji yetu katika maombi,ila pia maandiko yanasema mungu anajua mahitaji yetu hata kabla hatuja yaomba,sasa kwa muji wako kuna haja gani ya kupeleka maombi wakati yanafahamika hata kabla hayajafikishwa kwa mtoaji.
 
Maombi ni mazungumzo kati yako na Mungu kama mtoto anayoongea na Baba yake. Yeye anayejua ndio anaruhusu tuongee naye chochote ikiwemo na mahitaji hata kama anayajua.

Anasema leteni hoja zenu za nguvu, anawaita watoto wake wahojiane naye (Reason together Isaya 1:18). LAKINI KUMBUKA HATA PUMZI ALIYOKUPA HUJAOMBA. NA MENGINE UNAOMBA ANAJUA YATAKUUMIZA ILA KARUHUSU MAANA KATIKA KUZUNGUMZA NAYE UTAFUNDISHWA PIA.

Pia mtu aliye na ukaribu sana na Mungu ajenda zake nyingi katika maombi ni Shukrani. SHUKRANI KWA ALIVYOPEWA NA ASIVYOPEWA AMBAVYO ATAPEWA. MAOMBI YA KUHITAJI VITU NI HATUA YA AWALI YA MAHUSIANO NA MUNGU. KIKUBWA UENDE NA HOJA KATIKA MAWASILIANO YAKO NA YEYE. UKIITWA IKULU UKAE NA RAISI SIKU NZIMA WAWILI PEKE YENU, UKAENDA BILA POINTS NA HOJA UTAKUWA UMEJINYIMA NAFASI KUBWA. SISI TUMEITWA KUKAA NA RAIS WA MALINMWENGU YENYE TRILLIONS Za sayari enye viumbe matrillion na serikali zisizohesabika. Huyo ndiye tunayemuendea kuzungumza naye kila siku.
 

Maombi ni ishara ya kutokuwa na imani na ni ubinafsi.
 
Hoja yangu Kubwa itakua kutawala hasa uchumi kuanzia Leo na dili na hii agenda akuna ibada safi kama ujatawala Hasa uchumi na Mazingira yake
 
Sawa mtumishi umeeleweka
 
Hoja yangu Kubwa itakua kutawala hasa uchumi kuanzia Leo na dili na hii agenda akuna ibada safi kama ujatawala Hasa uchumi na Mazingira yake
Hizi ndio hoja za nguvu Mungu anataka.
Huwezi kumcha Mungu kwa adabu na heshima ukiwa financially slave. Pray for financial freedom.

Mungu akutendee.
 
Ahsante, kuna vitu ! Umeniongezea Leo.

Nami nasisitiza " kaa sehemu ambayo, mwingine akija asipate usumbufu."
Mf: kwenye safu ya viti/mabenchi kaa katikati
 
Nowadays naona wazee au wachungaji badala ya kutoa mafundisho/mahubiri ni full vichekesho na mizaha mimbarani.
Hilo ni kosa baya sana. Maana mizaha inamfukuza roho mtakatifu. Wengi hawasomi maandiko kama zamani. Huo udhaifu unafichwa kwa vichekesho na mizaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…