Fanya haya ukitaka kuwa na mahusiano yenye furaha katika jamii

Fanya haya ukitaka kuwa na mahusiano yenye furaha katika jamii

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
USIMPIGIE MTU SIMU ZAIDI YA MARA 2 MFULULIZO
- labda kama ni jambo lenye haraka sana, subiri mpaka wakupigie.

UKIKOPA, LIPA!
-Rudisha kabla hata hujaoulizwa au kukumbushwa

UKITOLEWA DINNER AU LUNCH
-Usiagize vyakula vya gharama sana na mara nyingine ununue wewe

KUWA NA UTU
-Kwa wahudumu, wafanyakazi, madereva wa uber na watoa huduma wote

MFUNGULIE MLANGO ANAYEKUJA NYUMA YAKO
-Bila kujali umri, jinsia au hadhi

UKICHUKUA UBER/BOLT NA MWINGINE
-Akilipa wakati huo, wakati mwingine ulipe wewe!

HESHIMU MAWAZO YA WATU WENGINE
-Kwako ukiona 9, huenda kuna mwenzio anaona 6

USIINGILIE MWINGINE AKIONGEA

-Zamu yako itafika, subiri!

UKIMTANIA MTU
-Akionekana hajafurahishwa, acha mara moja na usirudie tena

SHUKURU
-Sema asante unaposaidiwa, kuwa na moyo wa shukrani

USIVUNJE AHADI

-Hilo ni deni, lazima lilipwe, kama huwezi usiahidi tafadhali

UKIAMBIWA JAMBO LA SIRI
-Kuwa na kifua na uadilifu hata kesho mkiamka maadui

UKIONESHWA PICHA KWENYE SIMU YA MTU

-Usikimbilie kuswipe kulia au kushoto, huwezijua utakalo kutananacho, tuliza macho na vidole vyako

JALI MUDA WA WATU
- Usipange muda wa jambo kama huwezi kutimiza, muda ni pesa

USIONGELEE SHIBE KWA WENYE NJAA
- Ukiwa Roma, fanya kama Warumi

Mna mambo yakuongezea Wakuu? Karibuni
 
Uko sahihi mkuu.

Sio kila tabia ni kuifanya kila sehemu
 
Kumbuka unapokuwa una kitu asiye nacho huwa anaumia kiasi kwamba anakuwa anakuombea ukikose ama ukipate.

Kumbuka hakuna anayemuonea wivu masikini na ndio haulizwi chanzo Cha umasikini Bali tajiri anaulizwa chanzo Cha utajiri wake.
 
Back
Top Bottom