ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,154
- 4,184
Mpendwa
Najua wote tunataka mafanikio na leo nataka niwashirikishe siri ndogo ya furaha kwa mwaka 2018
Mwaka unaenda kufika mwisho na kwa kuwa ninakujali napenda kukushirikisha ya kufanya ndani ya masaa machache yajayo
Kwanza nakushauri ufunge hesabu ya mwaka huu.Jiangalie ulipokuwa mwishoni mwa mwaka jana na ulipo sasa.
Jiulize je kipato chako kimekuwa au kimepungua,jiulize furaha yako imeongezeka au imepungua.Jiulize kuhusu mtindo wako wa maisha,marafiki je kuna lipi limeongezeka
Jiulize kwa mwaka uliosha ni jambo gani jipya ulilojifunza.Umejifunza nini katika fani yako,umejifunza nini katika maisha
Kama kuna makosa uliyofanya je umejifunza nini kutoka na makosa hayo.na kama kuna mambo mazuri pia uliyofanya yalikufundisha nin
Jiulize unajisikiaje kuwa hai leo.Ni nani watu waliocahngia katika kukufanya ujisikie jinsi ulivyo?
Je kuna uliyemkosea ambaye unatamani kumwomba msamaha?Mwambie mwombe radhi
Ukishamaliza kutafakari na kufanya hayo yote tafuta mtu mmoja ambaye ungependa ama kumwambia asante kwa jambo fulani au kumweleza hisia zako kama vile kumpenda n.k.Mtafute uwasiliane naye umweleza jinsi unavyojisikia kwa jambo alilokufanyia au kwa yeye kuwepo katika maisha yako.
Hatua inayofuata ni kuweka malengo ya maisha yako kwa mwaka ujao.Usiweke malengo ya kipuuzi.
Lengo lako la kwanza nikuwa na furaha,Amani na upendo katika Maisha Yako
Lengo lako la pili liwe ni wewe kuhakikisha unapata mahitaji yako ya msingi kwa kadiri ya uwezo wako
Lengo lako la tatu ni kugusa maisha ya watu kwa namna njema ili ufanyike kuwa baraka
Tumia masaa haya machache kufanya hayo na utakuwa umeuanza mwaka wako vyema