Fanya hivi ili uweze kuperuzi mitandao iliyozuiwa (blocked) bila ya kudownload VPN kwenye Kompyuta yako

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Ni wazi kuwa matumizi ya mtandao yameminywa sana Tanzania kwa sababu za kisiasa zinazowekwa kwenye mtazamo wa kiusalamaua na kimaadili, tumefikia kipindi mtu anahitaji kutafuta mbinu za kuweza kupata taarifa kutoka kwenye majukwaa muhimu ya habari kama X na hata sasa Baada ya kusitishwa kwa muda kwa leseni JamiiForums hasa kwa watumiaji wa Tanzania.

Mamlaka zimeendambali zaidi hadi kufikia hatua ya kuzuia kuperuzi tovuti za kudownload huduma za VPN.

Kwasasa Matumizi ya VPN Tanzania yanahitaji kibali maalumu licha ya mazingira na maendeleo ya matumizi ya mtandao kuhitaji mtumiaji kuwa na VPN.... Mimi binafsi siwezi kumshauri mtu kujiunga na WiFi yeyote ambayo haimiliki yeye mwenyewe kama hatumii VPN. Ni hatari si tu kwa taarifa zako binafsi ila hata usalama wa fedha zako hasa katika kipindiki hiki sera nyingi za dunia zinahimiza cashless transactions.

Cha kushangaza ni kwamba huduma kama za VPN na huko tunapoelekea hazitakuwa za kuchagua au kutochagua kuwa nazo bali ni huduma za msingi katika kifaa chochote na hivi vikwazo vyetu vya kihafidhina havitakuwa na maana yeyote.

KWa mfano kwasasa hauna shida ya kupakua VPN kwenye kumpyuta yako ya Windows, Kila Kompyuta ya Windows inakuja na browser ya Microsoft Edge.

Edge ina VPN moja kwa moja, unachotakiwa ni kuiwasha tu na hutahitaji kuwa na VPN kutembelea tovuti zilikuwa zilizozuiwa katika nchi uliyopo..

Binafsi Uhafidhina kwenye mambo ya msingi huwa siupendi kabisa nadhani kuna umuhimu wa kujuzana juu ya hili hasa kwa Watanzania waliopo huko nyumbani ambao hawewezi kuingia JamaiiForums wala X kwasababu za Wajinga wachache.

Fanya hivi ili uweze kuperuzi tovuti zilizozuiwa bila kudownload VPN katika Kompyuta yako.
  • Fungua Microsft Edge kwenye Kompyuta yako, hakikisha unatoleo jipya ua umesasisha hivi karibuni. Upande wa kushota wa sehemu wa kuandika tofuta au kutafuta (search) utaona alama ya Ngao bonyenya hapo.
  • Ikifunguka utaona neno VPN na mbele yake kulia kuna toggle switch, Ibonyenye itakuwa ya blue. Chini yake utaona sehemu ya kutiki (Checkbox) hii itakuwezesha kuifanya Edge ikumbuke tovuti na kuwa inajiwasha yenyewe kila unapotembelea tovuti hiyo.


    ​
Inawezekana ukaiwasha na isiwe inafanyakazi moja kwa moja, kurekebisha hilo unapaswa kubadili DNS maana Edge huwa inatumia DNS ya Mtoa Huduma wako ambaye kwa watu waliokuwa kwenye nchi zinazofanya hila za kuminya uhuru wa matumizi ya mitandao huwa wanashirikiana na watoa huduma.
Kukwepa hili inapswa kubaonye vile vidoti vitatu mbele ya neno Secure Networks Utaona sehemu imeandikwa Manage Secure networks, bonyenya hapo kisha ikifunguka tafuta kipengele cha secure DNS, kiwashe (kupitia toggle switch), Kama ipo kwenye "Use current Service provider" chagua ya chini yake "Choose a Service provider" kwenye sehemu hiyo utabonye machaguo yaliyokuwepo bna kuweka Cloudflare.


​

Kwa kufanya hivyo utaweza kuperuzi tovuti zote bila ya kudownload VPN kwenye kompyuta yako na kimkatikati unakuwa umewapa la kati mamlaka.
 
Cha kushangaza ni kwamba huduma kama za VPN na huko tunapoelekea hazitakuwa za kuchagua au kutochagua kuwa nazo bali ni huduma za msingi katika kifaa chochote na hivi vikwazo vyetu vya kihafidhina havitakuwa na maana yeyote.
Nimepigia mistari hapa.....
Leo hii Windows Defender iko vyede hauhitaji kabisa kina McAfee.....
 
Kwa utundu wangu wooote sijawahi jua kama edge wanatoa free vpn. Mara zote nimekuwa niki download extensions tu ambazo nazo zimekuwa na changamoto ya speed.

Leo kupitia bandiko nimeongeza maarifa mapya na kwa kweli hii ni elimu nzuri iliyokuja katika muda sahihi mno. Tunashukuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…