Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Inawezekana ulikua naye muda mrefu lakini akakuacha.
Inawezekana hamkuachana rasmi lakini alikupotezea tu lakini saivi anarudi.
Inawezekana mlikua mnapendana lakini ukajikuta umebweteka, au umekua bize sana mpaka mwanamke akakuacha.
Alikuacha sababu mvuto wako kwake ulipungua kiasi kwamba hakutaka kuona sura yako tena. Lakini baada ya ukimya ameanza kurudi. Anarudi aone kama bado kuna mvuto kati yenu.
Sasa anarudi lakini humwelewi.
Anakutext, anakupotezea mara anakuambia amekumisi alafu anakupotezea.
Au anakutafuta kwa sababu yoyote ile. Kisha anapotea.
Anataka aone utampokeaje, anataka ajue kama bado unamtaka sana au la.
Ukionesha kumtaka sana, atakupotezea.
Ukionesha kumpenda sana, atakupotezea pia.
Ukionesha kuumia sana, kwamba alikuacha, atakupotezea.
Ila ukimuonesha kutokujali kwamba arudi au asirudi we unasonga na maisha yako, atatafuta sababu mrudiane.
.
Ukiona humwelewi, mpe muda zaidi.
Kama mlichati vizuri jana ukiona anaelekea lakini amekua kimya tena, mpe muda.
Kama mlikutana na mkaongea vizuri na ukafurahia lakini amekupotezea tena mpe muda.
Kama alikuomba mrudiane (akakulilia kabisa), lakini sasa humwelewi, mpe muda zaidi.
Kama mlikutana na mkafanya mambo ya wapenzi, lakini sasa hajibu SMS yako, mpe muda.
Pengine alikufanyia hadi vitu unavyopenda, lakini sasa amekupotezea tena, mpe muda.
Mpe muda, usiwe na haraka.
Mwanamke anatumia muda mwingi kufikiria mambo, kujiuliza kama amefanya maamuzi sahihi au la. Mpe muda ajishawishi kwamba alifanya kitu kizuri kurudi kwako. Ukimlazimisha kwenye huo muda kwamba afanye maamuzi haraka, maamuzi atakayofanya ni kujiweka mbali na wewe mana haumpi uhuru wa kufikiri.
Pia usimjibu maswali yake moja kwa moja.
Mfanye ye ndo aongee zaidi kwa kumuuliza maswali.
Mfano, anakuuliza “ivi imekuaje umepokea simu yangu alafu ukasema tukutane?” we usimjibu kwamba ulimmisi na vitu kama hivyo. Bali mgeuzie swali “kaone kwanza, ebu nkuulize, nini kimekufanya ukubali kukutana?”