MC RAS PAROKO
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 623
- 606
Ni matumaini yangu mu buheri wa afya, Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi. kwa kuwa kam tujuavyo kumekua na kilio kikubwa kutoka kila kona nchini kutokana na ongezeko la gharama za kutuma na kutoa pesa kupitia simu zetu (Mobile Money Transactions). Nikiwa ni muhanga mkubwa wa hili na kwa kugundua kulalamika au kulaumu serikali na watunga sera hakutanisaidia lolote nimeamua kuandika uzi huu ili ukusaidie na wewe angalau kupata mwangaza juu ya hili.
Kwa wakati kama huu tarajia watu wengi tuliozoea M-Pesa,Tigo,HaloPesa moja kwa moja tunahama na kurudi upande wa bank kwa sababu makato ni reasonable na kumtumia mtu pesa uliyonayo cash ni bure. Yaani leo niliwa na 100k nataka kuiituma Arusha nachukua tu account number ya muhusika namuwekea mzigo direct bila makato yoyote na nikiwa na kiwango hicho hicho na nikaamua kutoa kwa ATM makato si 1300 hadi 1000 kutegemeana na Bank unayotumia.
Nini kitatokea endapo watanzania wengi watarudi kutumia bank? La kwanza n kwamba bank zitapata wateja wapya wengi na wengine waliokua na dormant acc watazifufua, hii itapelekea bank kupitia mawakala wake walio maeneo mengi nchini watafanya miamala mingi na kuoneza mapato/faida kwa bank husika.
Ikiwa bank zitatengeneza faida kubwa zaidi ni faida kwa stakeholders ambao ni wanahisa na kwa bank kubwa Tz serikali inamiliki asilimia kadhaa ya hisa katika bank hizo mf CRDB, NMB.
Hapa umeshajua faida itaenda kuongezeka na wanahisa wanaenda kupata Dividents kubwa na Capital gain itaongezeka sababu ya wawekezaji kuvutiwa na ukubwa wa faida inayotengenezwa na Bank.
Je, nini ufanye uweze kuwa miongoni mwa wanufaikaji wa ongezeko la tozo hizi? Jibu ni rahisi tafuta Bank ambayo unaamini na umejiridhisha na mwenendo wake na hapo anza kuwekeza pole pole kwa kununua hisa zao online kwa kutumia App ya Hisa kiganjani. Ni rahisi na haihitaji uwe na pesa nyingi ili uweze kuanza kuwekeza katika sekta hii.
Sipati wala sikosi chochote kwa wewe kuwekeza katika hili ila ni kitu ninachokielewa na nimependa kushare nanyi siku ya leo. naamini uzi huu utamsaidia mmoja kati ya wasomaji wengi. Uwe na siku njema na Bwana akuongezee siku zako katika nchi aliyokupa.