Fanya hivi kunufaika na ongezeko la tozo katika miamala ya simu (M-Pesa, Tigo Pesa, Halo Pesa)

Kwa wale mnaosema mkimbilie safaricom changamoto ipo kweny exchange rate na hapo ndo wengi tunapigwa.

Chunguzeni kwa makini mtajionea rate iko 21.4 uku Safaricom wanakupa 20.8
 
Tuliamua kutumia mpesa, tigopesa etc kwa sababu ya mifoleni ya benki na conveniences za kutumia mitandao. Kurudi tena Benki kipindi Hiki cha korona ni risk na Haileti unafuu wowote. Suluhu ni kuenda mahakamani hizi tozo ziondolewe kwa sababu ziko kinyume na katiba

Kwa sasa kuna choice mbili tu! turudi banks tupange foleni au tuendelee na mfumo tuliowekewa tuwavimbishe vitambi wabunge na viongozi wetu. Kesi kuipeleka mahakamani inahitaji pesa na ushujaa. Ushujaa ambao watanzania hatuna, sie ni mabingwa wa kulalamika na kupiga domo tu. Kwa namna tunavyoishi na kufanya pirika zetu za kila siku, sio kama korona na foleni ndani ya bank kama ni issue kubwa.
 
Miccm ilivyojikausha utadhani hawaoni huu ujinga wa serikali yao.

Uko sahihi. Yaani kama uko na pesa kwa Tigopesa itume bank then nenda kwa Wakala kaitoe. Nimetoa 500,000 NMB wakala kwa takribani 4000 tu
Ungeenda kutoa kwny atm
 
Cut your Nose to Spite your Face....

Huwezi kwenda against technology in the end Mobile Network Providers will Come on top; Banking as we know it its a dying breed, wanahitaji kubadilika sana...., kumbuka pia Block Chain Technology is coming..., kwenye mikopo kuna kitu kinaitwa P2P lending..., kinachowafanya Benki wawe bado wapo hai na sio kwamba wangekufa jana ni BOT ambapo rules and regulations zinawabana Mobile Network Providers
 
IPO HAJA YA KUPIGA MARUFUKU HIZI LAINI ZA NGAMBO KUTUMIKA NDANI YA NCHI
 
Ni matumaini yangu mu buheri wa afya, Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi. kwa kuwa kam tujuavyo kumekua na kilio kikubwa kutoka kila kona nchini kutokana na ongezeko la gharama za kutuma na kutoa pesa kupitia simu zetu (Mobile Money Transactions). nikiwa ni muhanga mkubwa wa hili na kwa kugundua kulalamika au kulaumu serikali na watunga sera hakutanisaidia lolote nimeamua kuandika uzi huu ili ukusaidie na wewe angalau kupata mwangaza juu ya hili.

Kwa wakati kama huu tarajia watu wengi tuliozoea M-Pesa,Tigo,HaloPesa moja kwa moja tunahama na kurudi upande wa bank kwa sababu makato ni reasonable na kumtumia mtu pesa uliyonayo cash ni bure. Yaan leo niliwa na 100k nataka kuiituma Arusha nachukua tu account number ya muhusika namuwekea mzigo direct bila makato yoyote na nikiwa na kiwango hicho hicho na nikaamua kutoa kwa ATM makato si 1300 hadi 1000 kutegemeana na Bank unayotumia.

Nini kitatokea endapo watanzania wengi watarudi kutumia bank? La kwanza n kwamba bank zitapata wateja wapya wengi na wengine waliokua na dormant acc watazifufua, Hii itapelekea bank kupitia mawakala wake walio maeneo mengi nchini watafanya miamala mingi na kuoneza mapato/faida kwa bank husika.

Ikiwa bank zitatengeneza faida kubwa zaidi ni faida kwa stakeholders ambao ni wanahisa na kwa bank kubwa Tz serikali inamiliki asilimia kadhaa ya hisa katika bank hizo mf CRDB,NMB.

Hapa umeshajua faida itaenda kuongezeka na wanahisa wanaenda kupata Dividents kubwa na Capital gain itaongezeka sababu ya wawekezaji kuvutiwa na ukubwa wa faida inayotengenezwa na Bank.

Je nini ufanye uweze kuwa miongoni mwa wanufaikaji wa ongezeko la tozo hizi? Jibu ni rahisi tafuta Bank ambayo unaamini na umejiridhisha na mwenendo wake na hapo anza kuwekeza pole pole kwa kununua hisa zao online kwa kutumia App ya Hisa kiganjani. Ni rahisi na haihitaji uwe na pesa nyingi ili uweze kuanza kuwekeza katika sekta hii.

Sipati wala sikosi chochote kwa wewe kuwekeza katika hili ila ni kitu ninachokielewa na nimependa kushare nanyi siku ya leo. naamini uzi huu utamsaidia mmoja kati ya wasomaji wengi. Uwe na siku njema na Bwana akuongezee siku zako katika nchi aliyokupa.
Mwigullu & company wanawafanya watanzania ni wapumbavu. Tozo ni wizi wa dola. Sh 10000 ikihamishwa kwa simu 3 ie A akamtumia B, B akamtumia C na akaenda kuitoa kwa wakala, imekwisha! Mfumo mbadala ni kupitia bank japo vujijini watapata shida, mawakala wa bank ni wachache. Pamoja na makato ya bank kila mwezi ya service charge, yana nafuu kubwa.
 
Tuliamua kutumia mpesa, tigopesa etc kwa sababu ya mifoleni ya benki na conveniences za kutumia mitandao. Kurudi tena Benki kipindi Hiki cha korona ni risk na Haileti unafuu wowote. Suluhu ni kuenda mahakamani hizi tozo ziondolewe kwa sababu ziko kinyume na katiba
Kwenda mahakamani unajisumbua, hatuna mahakama huru. Folen bank hakuna, zimepunguzwa na wingi wa mawakala mitaani. Money transfer nmb ni bure, unaweza mwekea pesa mtu alie Mtaa wa tatu. Ndugu wa vijijini ndio wataathirika na Tozo.
 
Miccm ilivyojikausha utadhani hawaoni huu ujinga wa serikali yao.

Uko sahihi. Yaani kama uko na pesa kwa Tigopesa itume bank then nenda kwa Wakala kaitoe. Nimetoa 500,000 NMB wakala kwa takribani 4000 tu
Kuituma unazunguka na kuingia kwenye double transaction, lakini bado makato ni nafuu. Sijui mwalimu aliemfundisha Mwiguli uchumi anajisikiaje!
 
Hajawahi kusoma kwa kuelewa, aalisoma kwa kukariri na ndio matokeo yake hayo sasa
 
Watumiaji wa mitandao ya simu kwa kiasi ilibeba watu wengi kwa kuwa ni wa kipato cha chini na ni rahisi kumtumia 30000 bibi yangu kule kahama na akatoa bila hekaheka nyingi.

Bado mitandao ya simu ni muhimu hususa kwa watu tunaotima 5000 hadi 100000. Karibu kila mtu anamiliki line ya simu. Na kwa hili serikaki imepiga patamu. Yaani hapa watavuna si mchezo.

Kama kwa siku tu kima cha chini miamala mil1 inafanyika hiyo ni zaidi ya millioni miamoja wanakusanya.
Upo sahihi. Statistics on mobile telecom services in africa - global market, m-pesa, tigo-pesa, na airtel money, jan-mar 2020 zilifanya miamala 93.8bn, hiyo ni sawa na miamala 375.2 bn kwa mwaka. Hata kwa tozo la sh 30 serikali itapata sh 11.25 trn kwa mwaka. Bado kuna halotel, na kampuni zingine za simu ambazo huku mikoani tunazisikia tu.
 
Ilifaa kiwango cha juu kabisa cha tozo basi isizidi 5000
Cha chini huku hata wakiwa wanachukua mfano kwa 10000 wachukue 100. Kwa laki wachukue 1000 watu tusingekakama sana.
Ila ni kama serikali imefanya tamaa.
 
Ni matumaini yangu mu buheri wa afya, Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi. kwa kuwa kam tujuavyo kumekua na kilio kikubwa kutoka kila kona nchini kutokana na ongezeko la gharama za kutuma na kutoa pesa kupitia simu zetu (Mobile Money Transactions). nikiwa ni muhanga mkubwa wa hili na kwa kugundua kulalamika au kulaumu serikali na watunga sera hakutanisaidia lolote nimeamua kuandika uzi huu ili ukusaidie na wewe angalau kupata mwangaza juu ya hili.

Kwa wakati kama huu tarajia watu wengi tuliozoea M-Pesa,Tigo,HaloPesa moja kwa moja tunahama na kurudi upande wa bank kwa sababu makato ni reasonable na kumtumia mtu pesa uliyonayo cash ni bure. Yaan leo niliwa na 100k nataka kuiituma Arusha nachukua tu account number ya muhusika namuwekea mzigo direct bila makato yoyote na nikiwa na kiwango hicho hicho na nikaamua kutoa kwa ATM makato si 1300 hadi 1000 kutegemeana na Bank unayotumia.

Nini kitatokea endapo watanzania wengi watarudi kutumia bank? La kwanza n kwamba bank zitapata wateja wapya wengi na wengine waliokua na dormant acc watazifufua, Hii itapelekea bank kupitia mawakala wake walio maeneo mengi nchini watafanya miamala mingi na kuoneza mapato/faida kwa bank husika.

Ikiwa bank zitatengeneza faida kubwa zaidi ni faida kwa stakeholders ambao ni wanahisa na kwa bank kubwa Tz serikali inamiliki asilimia kadhaa ya hisa katika bank hizo mf CRDB,NMB.

Hapa umeshajua faida itaenda kuongezeka na wanahisa wanaenda kupata Dividents kubwa na Capital gain itaongezeka sababu ya wawekezaji kuvutiwa na ukubwa wa faida inayotengenezwa na Bank.

Je nini ufanye uweze kuwa miongoni mwa wanufaikaji wa ongezeko la tozo hizi? Jibu ni rahisi tafuta Bank ambayo unaamini na umejiridhisha na mwenendo wake na hapo anza kuwekeza pole pole kwa kununua hisa zao online kwa kutumia App ya Hisa kiganjani. Ni rahisi na haihitaji uwe na pesa nyingi ili uweze kuanza kuwekeza katika sekta hii.

Sipati wala sikosi chochote kwa wewe kuwekeza katika hili ila ni kitu ninachokielewa na nimependa kushare nanyi siku ya leo. naamini uzi huu utamsaidia mmoja kati ya wasomaji wengi. Uwe na siku njema na Bwana akuongezee siku zako katika nchi aliyokupa.
Mkuu maelekez kidogo jinsi ya kununua hizo hiss kupotia hy app
 
Back
Top Bottom