Fanya hivi kuondoa Nuksi/Mikosi kwa kutumia Biblia

Fanya hivi kuondoa Nuksi/Mikosi kwa kutumia Biblia

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Nuksi ni neno la Kiarabu lenye maana ya machafuko, maharibiko, mivurugano katika maisha.

Ni hali inayomfanya MTU kuwa na ugumu katika kutenda mambo yake. Hii unaweza kusababishwa na mambo kadhaa.

1: Ukosefu wa Maarifa sahihi.
2: Kulogwa,laana au majini.
3: Mitihani ya mwenyezi Mungu ili ukifuzu akutunuku kile unachokitaka ukiwa umekomaa.

Kwa sababa 1 na 3 Biblia inasema watu wangu wanaangamizwa kwa ukosefu wa maarifa. Ukisoma neno kwa maombi, Kufunga na kukesha. Ukiaminj Yuko roho mtafsiri mkuu. Mungu atakufunulia nini cha kufanya. Atakupa Nguvu ya kuvumilia Darsa.

Namba 2: KAMA UMELOGWA AU LAANA.
1: Kama umejisababishia mfano umemvunjia heshima mzazi. Tubu kaombe msamaha.

2: Kama umelogwa. Tubu.

Kisha chukua biblia kila siku Mara tatu Asubuhi, mchana na usiku.

Tafuta ahadi za Mungu kuhusu tatizo ulilonalo. (Unaweza kugugo mistari).

Anza kujitamkia hilo neno.
Mfano:
Sitakufa Bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo makuu ya Bwana.
Zaburi 118:17

KISHA
1: Jitamkie hilo neno kwa sauti, na kwa kurudiarudia.
2: Malaika wanaotendea kazi neno la Mungu watalichukua na kuligeuza kinyume na maneno uliyotamkiwa huko kwa adui.
3:Ukifanya kwa imani bila kusita, Nguvu zote zinazokuletea hizo nuksi au balaa zitaachia.

4: Kama ni ugonjwa au umauti utakimbia.

Kila tatizo la kichawi, Liko neno ambalo ni ufunguo wa hilo tatizo.

Fanya haya, utanishukuru.

ANZA KUNUFAISHWA NA BIBLIA YAKO. USITEMBEE NAYO TU KAMA KITABU CHA KIADA NA ZIADA. BIBLIA NI MAISHA.
 
Malaika wanaotendea kazi neno la Mungu kwa majina yao wanaitwa nani vile?
mitale na midimu
Psalms 103:20
[20]Bless the LORD, ye his angels, that excel in strength, that do his commandments, hearkening unto the voice of his word.
Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.

Hapo juu ndicho ninachofundisha.

Ukitamka neno LA Mungu, Malaika wanalitendea kazi.

Malaika yoyote aliyekuwa assigned na Mungu katika hicho kitengo husika.

Kwa imani
 
Back
Top Bottom