Kwema Wakuu!
Nimeona vijana wengi wakilalamikia mabinti kunuka Uke/nyuke Zao. Uke kunuka sio tuu ni aibu kwa Mwanamke bali inamshushia thamani na heshima yake.
Uke kunuka utakufanya ukose Mume.
Uke kunuka utakufanya usiwe comfortable ukikaa mbele za Watu au ukienda kusuka.
Au hata kwenye Daladala, unakuta binti mrembo na kajipamba vyema kabisa. Lakini mara unashangaa unasikia harufu fulani hivi yenye ukaribu na usaha au Kibudu(mnyama aliyeoza), inakuja na kupotea. Ni aibu.
Sasa warembo, sipo hapa kumlaumu yeyote. Najua tonatofautiana uelewa, akili, elimu na malezi.
Unapoambiwa uoshe Uchi/Uke wako haimaanishi uchukue masabuni usugue kama unasugua kikwapa. Nop.
Usitumie maji ya moto au yenye sabuni kuoshea Uke wako.
Wala usiingize kitu chochote ambacho sio kwa maelekezo ya wataalamu hasa wa mambo ya uzazi.
Uke wako utanuka usaha nakuhakikishia.
Kwenye Uke kuna wadudu maalum kwaajili ya kiungo hicho. Unapotumia madawa(sabuni) au maji ya moto au kemikali zozote kusafisha Uke wako unapelekea hao wadudu kupoteana, kuangamia, kufa na hiyo itafanya ujio wa wadudu ambao sio mahususi kwa eneo hilo kama Fangasi na jamii zingine za bacteria.
Usiingize vidole vyako Ukeni wakati wa kujisafisha. Osha eneo la nje la Uke na maji baridi. Kisha tumia kitambaa kikavu kilichokisafi kujikaushia. Hakikisha pawe pakavu. Kisha vaa chupi ambayo umeipiga Pasi vizuri. Na kama hauna pasi. Basi hakikisha unaitunza mahali safi na salama.
Usijioulizie marashi Ukeni.
Ukitoka kujisaidia haja ndogo hakikisha unajisafisha (maji ya baridi) vizuri na kujifuta ujikaushe vizuri.
Epuka kuvaa pedi muda mrefu. Wastani wa pedi angalau masaa matano mpaka nane. Hivyo kwa siku ni vizuri ubadilishe Pedi sio pungufu ya Tatu.
Kunywa maji Mengi ili kuufanya mwili uwe sawa. Kuepuka kunuka nuka hovyohovyo. Kunywa maji mengi hufanya mifumo wa mwili kuwa safi na kufanya kazi vizuri. Ikiwemo mifumo ya utoaji takamwili.
Wastani wa maji itategemea na umri na uzito. Lakini kikawaida usipungue lita mbili na nusu na isizidi tano.
Ni aibu kunuka Uchi. Na kutibu uchi unaonuka ni mchakato mrefu.
Hakuna kitu kitamkera mwanaume kama kukutana na Mwanamke mwenye uchi unaonuka. Ni vizuri kujisafisha kwa njia sahihi.
Huwezi ukajiamini kama Uke wako unanuka. Utaishi kwa stress, utaachwa kila mara, hakuna mwanaume atakuvumilia.
Mimi nimemaliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam